Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe,Mhe. Adadi Rajabu akitoa hotuba yake mkutano wa watanzania waishio Zimbabwe uliofanyika kwenye ukumbi wa Tanzania Club,mjini Harare.Mhe. Balozi Adadi alisisitiza sana umuhimu wa umoja, ukaribu na mawasiliano ya mara kwa mara ya watanzania hao akihusisha na umuhimu wa sera ya Diaspora.Jambo jingine muhimu alilozungumzia Mh. Balozi ni haja ya watanzania hao kuwa na uzalendo na nchi yao hususan katika kipindi hiki cha kusheherekea miaka 50 ya uhuru wa Tanzania, huku maazimio ya watanzania hao yanakusudia kufanya sherehe hiyo.
Baadhi ya Watanzania waishio nchini Zimbabwe wakisikiliza kwa makini hotuba iliyokuwa ikisomwa na Balozi wa Tanzania nchini humo,Mh. Adadi Rajab (hayupo pichani).
Jamani wana tatizo gani? mbona wako kama msibani? Maskini wanahuzuni?
ReplyDeleteJamani Wadau wenzangu, nina hamu ya kutembelea nchi hii ya Zimbabwe na naomba anayejua taratibu za kupata viza ya nchi hiyo anijulishe (nipo Iraq).
ReplyDeleteJe, nahitaji kujaza zile fomu za kuomba hiyo viza kama vile wafanyavyo Balozi za Marekani na nchi za Ulaya?
Abalalha Massoud, IRAQ
Hivi kuwa kishi nje ya nchi ni sifa? Hapa naona bora wangerudi nyumbani plate yake imejaa kidogo, maana wanaonekana kuchoka kama wakimbizi jamani rudini tu kuna mahindi na mchele wa kulima.....
ReplyDeleteWatanzania wanasikitisha sana jamani maana wapo kila sehemu utasema nchi yao ina vita wamekimbia vita
ReplyDeletekila sehemu duniani wapo tena asilimia kubwa wapo nchi za ulaya na america wanaishi kama wakimbizi
alafu tunasema nchi ina maendeleo serikali hata haijali ni kwanini watanzania wanakimbia makwao
maendeleo yapo kwa wenye hela tu na wenye uhusiano na viongozi au familia za viongozi
walalahoi maisha magumu sana mpaka wanajaribu kukimbia nchi na kujipakiza ukimbizi wa nchi nyingine
shame on viongozi wa tanzania
Hivi kwani ulikuwa ni msiba? mbona wanasikitika hivyo. Duh! au walikuwa wanapokea habari mbaya
ReplyDeleteHongereni watanzania mlioko huko Zimbabwe.Inaonyesha kuwa ninyi ni watafutaji na wengi wanaitamani fusra hiyo.Kuweni mabalozi wetu huko.
ReplyDeleteHongera Balozi Adadi kwa kuweza kuzungumza na Watanzania wenzako.Ni ofisi chache za ubalozi zinazotoa muda wao kujumuika na watanzania waishio katika nchi husika,
Mimi niko nje ya nchi kwa miaka kadhaa sasa lakini bolozi wetu hajajishughulisha na watanazinia tuishio hapa.