Taarifa ya pamoja baada ya mkutano huo wa siku mbili Ikulu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Kikwete (kulia) akiwa katika mazungumzo na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mh. Freeman Mbowe.Katikati ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mh. Bernard Membe.
Ujumbe wa  Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakipitia kwa makini taarifa ya pamoja iliyotolewa leo mwishoni mwa mkutano wa siku mbili wa chama hicho na Rais Jakaya Kikwete Ikulu. Leo kikao kilidumu kwa takriban masaa matano.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Kikwete akiagana na Prof. Safari mara baada ya Mazungumzo yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Kikwete (katikati) akiwasindikiza viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mara baada ya kufanya nao Mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Kikwete akiagana na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mh. Freeman Mbowe mara baada ya Mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Mh. Tundu Lissu akiagana na Rais Kikwete.
Prof. Baregu nae akiaga.
Prof. Abdallah Safari na Mh. John Mnyika wakitafakari.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mh. Freeman Mbowe akifunga mlango wa gari yake wakati akiondoka Ikulu jijini Dar leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. Hongereni sana CHADEMA kwa kufanikisha azma ya kukutana na Rais kuitetea jamii ya Tanzania.big up endeleeni kukaza mwisho maendeleo yatapatikanaHongereni sana CHADEMA kwa kufanikisha azma ya kukutana na Rais kuitetea jamii ya Tanzania.big up endeleeni kukaza mwisho maendeleo yatapatikana

    ReplyDelete
  2. Chadema aka CCM C kwishaney.

    ReplyDelete
  3. Mh Dk J. Kikwete, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa TANZANIA. Tunatoa shukrani za dhati kwa kuto kuweka sahihi katika makubaliano ya EAST AFRICAN COMMUNITY yanayohusu ARDHI, MALIASILI NA MALIGHAFI YETU WATANZANIA. Kwasababu watani zetu wanazimezea mate na SIKU MTAKAYOKUBALI NA HAYO MAFUTA YALIYOGUNDULIKA UGANDA na TANZANIA BASI SISI HATUNA CHETU BALI (UGOMVI NA VITA)...(KUNATIMU/KAMATI KABAMBE NA MABILLIONI YA DOLLAR KUTOKA NCHI JIRANI IMEPANGA MKAKATI WA HALI NA MALI)..!! TUNAKUSHUKURU NA SAMWELI SITTA !! VYAMA VYA UPINZANI HAKIKISHENI VIPENGELE VYA ARDHI, MALI ASILI NA MIPAKA YETU TANZANIA VIKO KATIKA KATIBA MPYA KAMA MALI YA WATANZANIA NASIO EAST AFRICA AU NCHI JIRANI. [MAFUTA NA MADINI WANAYATAFUTIA UGOMVI KILA KUKICHA ILI WAYAPATE KIURAHISI/BURE NA MIFANO TUNAYO]

    ReplyDelete
  4. ilivyo bendera ya Taifa, kijani, buluu

    ReplyDelete
  5. Tanzania yagoma kutia saini sera ya ardhi EAC
    Monday, 28 November 2011 21:22

    Mwandishi Wetu, Bujumbura
    WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta amegoma kusaini mikataba ya Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) unaohusu sera za ardhi, ulinzi na mambo ya nje.Sitta ambaye anaongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano wa Baraza la Mawaziri wa EAC unaofanyika hapa Burundi, aliwaambia waandishi wa habari kuwa suala hilo wamelikataa ili lirejeshwe kwa wakuu wa nchi kwa uamuzi.

    Hali hiyo ilifanya mkataba huo kusainiwa na nchi nne tu za Afrika ya Mashariki, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda hivyo kuiacha nafasi ya saini ya Tanzania kubakia wazi.

    Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki, Stragomena-Tax Bamwenda alisema jambo hilo ni nyeti, lakini akaweka bayana kuwa ujumbe wa Tanzania utapaswa kutoa taarifa kwa baraza kufafanua msimamo wao.

    Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Lazaro Nyalandu aliweka wazi kwamba suala la ardhi halipaswi kuwa sehemu ya EAC.Alionya kwamba kuna mazingira yanayoashiria kuwa baadhi ya wajumbe wa nchi za jumuia hiyo wamekuwa wakiangalia ardhi ya Tanzania kwa jicho la husuda.

    Mbunge huyo wa Singida Kaskazini alisema Tanzania ina ardhi kubwa ambayo inawapa nafasi Watanzania kuchagua eneo la kwenda kuishi.Lakini akasisitiza kuwa ardhi hiyo lazima ibakie kwa ajili ya Watanzania na vizazi vijavyo.

    Tanzania imekuwa ikilalamikiwa na baadhi ya wanachama wa Jumuia kwa msimamo wake kuhusu ardhi hivyo kukwamisha juhudi za kuimarisha EAC.

    http://www.mwananchi.co.tz/habari

    ReplyDelete
  6. this is what i call development milestone.badala kusinzia na kupiga makelele tuu.chadema wameonesha ukomavu kumvaa mkuu wa nchi na kukata naye ishu serious za kitaifa...si kisiasa. sasa wengine fuateni mfano. na kina nape,mwigulu na january leteni mtazamo mpya ccm suyo kila kitu kutoka upinzani ni vuta. igeni mifano ya nchi nyingine ishu zinajadiliwa na kupitishwa kwa makubaliano si mabavu...bravo to jk na chadema.

    ReplyDelete
  7. I say hiyo TANZANIA YETU leo inashaini sana leo! baada ya picha hiyo ya amani na peace
    God Bless tanzania na watu wake....JK you are the best president...who want peace na Amani in the our country...keep up the good work...POA SANA...

    ReplyDelete
  8. Nimefurahi sana kwa Rais wetu wote kukubali kukutana na wananchi wake bila tatizo, nakupa Big up Rais wetu mpendwa.
    Na ni vizuri kwa sababu huwezi kujua wanakuja na jambo gani? hiyo inapendeza sana.

    ReplyDelete
  9. jamani, mwenzenu naona kama 'changa la macho vile'!

    ReplyDelete
  10. Lazima kila wakati tuangalie maoni ya wenzetu, si kila jambo wanalosema wapinzani ni jambo baya au halifai, au halina mafanyikio. tuangalie kila jambo wakati mwingine tunakuwa tunawalalamikia bure na wenyewe pia wajitahidi kuwa na nidhamu wakapokuwa Bungeni wakumbuke kuwa wanawawakilisha wananchi wao, si kufanya mambo ya mitaani. Wanajivunjia heshima

    ReplyDelete
  11. hiyo gari ya Mbowe....duh ngoja ninyamaze

    ReplyDelete
  12. Bravo JK! 'Mnyonge mnyongeni haki mpeni' katika masuala ambayo JK na washauri wake wameshanya maamuzi sahihi ni kukubali kuonana na CHADEMA, angekataa angewaongezea umaarufu sana! na walikuwa wanasubiri kwa hamu sana wakataliwe ili wapige makelele wapate umaarufu zaidi. Mchawi dawa yake mpe mwana alee! kiko wapi, kelele zote zile kumbe shida ni kuonana na Rais!!?? Haya sasa Rais mmemwona mlichobadilisha ni nini??!! Muswada wa katiba imeshapitishwa na Bunge, na hakuna shaka Rais atauisaini na hakuna jipya! Kumbe kikubwa kilichokuwa kinaliliwa ilikuwa ni kupata 'attention' ya Mheshimiwa Rais!!!. Hoja zote zile za kuleta maandamano iwapo Rais akisaini muswada huu zimeishia wapi? Umaarufu wa CHADEMA unaongezwa na watendaji wa serikali kwa kuendelea kuwazuia na kuwakatalia vitu vidogo vidogo - lakini ukiwaruhusu utashangaa maisha yatakavyokuwa ya kawaida sana. Ndugu wanananchi akili ni nywele kila mtu ana zake vichwani mwetu na macho pia tunayo, basi tuyatumie kujua mchele ni upi na pumna ni zipi.

    ReplyDelete
  13. Jmani mie nauliza hivi chadema wamekwenda kumuona nani kule ikulu? kama nakumbuka vizuri walisemaga hawamtambui rais JK na hata slaa hakusign kukubali kushindwa uchaguzi,nipo gizani hebu nitoeni huko,ni sahihi walichofanya kutokumtambua then kumtembela ikulu? hata sijui lakini mie ni mpita njia tuu!!!

    ReplyDelete
  14. walikuwa na hamu sana kumwoona hahahahaha maana wakati anaapishwa hawakwenda alivyoenda bugeni wakatoka hhivyoo wametumia hiyoo njia kweenda kumwona walifikiri kutoka kwao wangebebelezwa. CHADEMA JAMMNI JAMII Msipokuwa macho mtapotoshwa sana na hawa jamaa hawana lolote wanataka umaarufu tu kichwani maji matupu.

    ReplyDelete
  15. walikuwa wanampeleka Mnyika akapajuee ikulu maana anaweza ondoka adaarakani hajafika Ikulu. Maana hakafanyi chochote haka Bungeni kanapiga porojo tu babara mbaya ile ya kweenda ubungo msasani duu tunabusiana bila hata kutaka, maana waweza kaa kweenye kiti gari ikayuba haddi busu la gari

    ReplyDelete
  16. Vitz ikulu......
    Ni escot ya Mh Mbowe tena Vogue ama ni wanachama wengine? ni mtazamo tu wa maisha bora kwa kila mtanzania.

    Hatumtambui Rais kwa kuwa matokeo si halali, Leo tunaomba kukutana nae na kujadili mabo ya msingi katika nchi yetu.
    Je chadema wangefanya mambo haya tangu mwanzini si nchi ingekuwa mbali? Wivu wa maendeleo ni mzuri,lengola vyama vingi sio kuhamasisha migogoro bali ni kutoa changamota katika mitazamo tofauti na kwa jicho la nje.
    Chadem Hoyee..CCM Hoyeee...Tanzania Hoyeee.

    ReplyDelete
  17. anony wa 09.12 am, jenerali wa ukweli ni yule ambaye huwa ana mibadala akiwa katikati ya uwanja wa vita. sheria iliyoanzisha chadema kama chama cha siasa haikustipulate kuwa ni chama cha vurugu ... mkataba wa chadema ni kwa DEMOKRASIA na MAENDELEO....

    kuna vilaza wengi wa design yako hudhani kuwa vurugu ni agenda ya chadema, ndio maana siku zote tunasema, vurugu zitaletwa na mtawala..kwa maana hii CCM....

    ni ukweli kuwa safari bado ni mbichi...tunamshukuru Kikwete na tunamsisitiza azingatie haya aliyoletewa na chadema, kwani bado chadema ina umma.kwa maslahi ya Tanzania. kukataa kusikiliza sauti hii ya umma kutaileteza sana shida nchii hii na itaongeza maumivu sana kwa wanyonge!

    naomba kuwakilisha!

    ReplyDelete
  18. hongera sana chadema na ccm. Hivi kwa nini kuna watu siku zote wanapenda malumbano yasiyo na msingi? sina uhakika sana mchangiaji wa kwanza anamaanisha nini ila kwa tafsiri ya haraka ni kama alipenda kuona mgongano mkubwa sana...ni kama vile kitendo cha rais kukubali kukutana na chadema yeye hajafurahia..ili malumbano yangeendelea...tuache ushabiki usio na faida kwa watanzania. sasa demokrasia naona inakuwa..BIG UP SANA PANDE HUSIKA

    ReplyDelete
  19. me nampenda sana huyo J. Mnyika, je ameoa? namlike kinoma

    ReplyDelete
  20. CCM B macho yanawatoka....nendeni sasa maana na nyie si mlitaka mkutano....ahahahah

    ReplyDelete
  21. CCM na CHADEMA nawaomba U-TANZANIA uwatawale!!! bado nawatafakari, sioni tofauti ya kikao kule bungeni na hicho cha Ikulu....... Natamani kikao cha Ikulu kingekuwa 'LIVE' ili watanzania tunaowatafakari wanasiasa wetu tupate nafasi ya kuwajua zaidi kuliko kuwa washabiki zaidi!!. Kumbukeni Katiba sio yenu wanasiasa ni yetu watanzania wote....tunasubiri kwa hamu kutoa maoni yetu na nitoe utangulizi... tunaendelea kutafakari nafasi zenu katika katiba ijayo.......

    ReplyDelete
  22. mtachonga sana ila ndio hivyo tena JK mwenyewe ameshasalimu amri na kuona bora yaishe, mazungumzo ya amani yamefanyika tunangoja utekelezaji tu. manake ingekuwa ndivyo sivyo anajua mshike mshike wa hawa makamanda wakianza kuzunguka nchi nzima! sio kila wakati mnachukulia upinzani ni kupinga tu hovyo hovyo, kuna mambo ya msingi ya kuongea hivyo hongera JK kwa kukubali kusikiliza maoni ya watu wengine. mliotaka ugomvi yamewashuka shu! hapo inaonyesha nani ni mchochezi wa vurugu.

    ReplyDelete
  23. Ahhh wamekwenda talii Ikulu tu...msimamo upo pale pale JEMBE na NYUNDO!....unajua unapokuwa shambani unalima Jembe lina mpini wa mti ambapo ktk maungano ya jembe na mpini pana fundo, sasa kwa tekniki za shamba ukiwa unalima ukikuta kisiki au magugu au nyoka ....unapiga kwa kutumia lile fundo unafanya kama ni nyundo...kumdhoofisha adui halafu adui akilainika ,una piga JEMBE LA NGUVU kungóa kisiki, magugu au kumuua nyoka kabisaa....sasa sanaa hii ndio imefanyika ikulu..... KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

    ReplyDelete
  24. Juhudi za kuimarisha Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) zitaimarika kwasababu ya huu msimamo wa Tanzania kuhusu ardhi. Kwa wanajumuia wa EAC kuweni patient kidogo, muda unakuja na mtausifia kabisa huu msimamo wa Tanzania. BIG UP MKUU Sitta.

    ReplyDelete
  25. Wewe mdau uliyeshangaa kuona gari la Mh. Mbowe, ni mkimbizi nini? Au unaishi ile mikoa ambayo Chadema inaipigania ili kuwe ingawa na mawasiliano na sehemu nyingine za dunia? Pole sana.

    ReplyDelete
  26. Angalia TZ bado tulivyo na amani. Viongozi wanaondoka hakuna cha polisi kutapakaa kila kona, kweupeee. Kwa nini wasituonee gele!

    ReplyDelete
  27. Kulalekkk....kuonana na Raisi sio mchezo babake, jamaa CDM wameingia nyuso zimewaporomoka wametoka wakitabasamu!

    ReplyDelete
  28. Mbowe ana hela zake kitambo tu,,,imejengeka imani kuwa kila anaeingia ktk siasa hana kitu ndio anatafuta mtaji...Freeman siasa ni sehemu tu ya maisha kwake, ebo!

    ReplyDelete
  29. CHADEMA MMEONA USTAARABU HUO?:::

    Jamani nauliza tazameni jinsi Raisi alivyo wapa ukarimu akawahudumia kwa juisi kwa mkono wake kila mmoja wakati mnaendesha mazungumzo, Je kiwango hicho cha ustaarabu unaweza kipata kwa mwendesha BAR kama BILLICANAS?...hivi Mbowe ingetokea ukapanga miadi na mtu mkutane bar Billicanas ,ungeweza kwenda Kaunta ukambebea mgeni wako kinywaji?...THUBUTU, ungemwagiza Meneja wa bar au Mhudumu!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...