Waziri kivuli wa Wizara ya Habari,Vijana ,Utamaduni na Michezo na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini,Mh. Joseph Mbilinyi (a.k.a. MR. SUGU) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo (hawapi pichani) kuhusu shoo aliyoiandaa ijulikanayo kama Anti Virus wakati wa Tamasha la Burudani kwa washabiki wake litalaofanyika jijini Dar mnamo tarehe 26 mwezi huu na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi.Kushoto ni Msanii Fred Malaki (a.k.a- MKOLONI) na Kulia ni Mwanadada Zainab Lipangile a.k.a ZAY –B, Katika tamasha hilo Wasanii mbalimbali watatumbuiza.
Waziri kivuli wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini,Joseph Mbilinyi (a.k.a Mr. SUGU) akionyesha kitabu ambacho ameelezea maisha yake kitakachopatikana wakati wa Shoo ijulikanayo Anti Virus katika Tamasha la Burudani kwa washabiki 2011 litaakalofanyika Nov. 26,2011 jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na wadau wa michezo.Kushoto ni Msanii Fred Malaki a.k.a. MKOLONI. ( Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO.)
Ndio Mhe. Mbunge Mr.Sugu umefanya vizuri kubakia ktk fani licha ya madaraka uliyonayo, tofauti na baadhi ya wanataaluma Madaktari waliodiriki kukata mguu Hospitalini baada ya kuukwaa Ubunge!
ReplyDeleteNampongeza Mh. Sugu kwa jitihada yake katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya.... Ila nnachoouliza na kushangaa jinsi alivyovaa hapo anaongelea mziki na burudani sasa vazi la chama linaingiaje nafikiri vazi la chama lina stahiki yake na heshma kwa mahala pake...... Asante naomba kuwasilisha.
ReplyDeletemsije mkafanyiwa zengwe nyie na You-Know-Who! Muda upo mpaka jumamosi kufanyiwa mandundu, shauri yenu!!!
ReplyDeleteSorry honourable. Your attire I don't like it. U remind me of the ilala municipal mgambo.l
ReplyDelete