Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni
Mh. Tundu Lissu.

MAONI YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI, WIZARA YA KATIBA NA SHERIA, MHESHIMIWA TUNDU A.M. LISSU (MB.)KUHUSU MUSWADA WA SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA, 2011
(Kanuni ya 86(6) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2007)

UTANGULIZI


Mheshimiwa Spika,
Tarehe 11 Machi 2011, Serikali ilichapisha Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 katika Gazeti la Serikali la tarehe hiyo. 

Muswada huo ulipelekwa katika Mkutano wa Tatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa Hati ya Dharura. Hata hivyo, baada ya upinzani mkubwa dhidi ya Muswada huo kujitokeza karibu nchi nzima, Bunge lililazimika kuondoa Hati ya Dharura na hivyo kufanya Muswada kushughulikiwa kwa mujibu wa utaratibu wa kawaida wa kutunga sheria uliowekwa na kanuni za 80, 83 na 84 za Kanuni za Kudumu za Bunge la Jamhuri ya Muungano, 2007. 

Katika kufanya hivyo, Bunge – kwa kupitia Spika - liliiagiza Serikali kufanya mambo yafuatayo kwa mujibu wa Taarifa Rasmi ya Majadiliano Katika Bunge (Hansard) ya Kikao cha Nane cha Mkutano wa Tatu cha tarehe 15 Aprili 2011:


(a) “Muda zaidi utolewe kwa Kamati na wananchi kuufikiria Muswada huu. Katika kufanikisha hili, “... iandae Muswada huu kwa lugha ya Kiswahili ili wananchi wenyewe waweze kusoma yaliyomo kwenye Muswada huo badala ya kupewa tafsiri tu na watu wengine;


(b) “Muswada uchapishwe kwenye magazeti na kutangazwa kwenye vyombo mbali mbali vya habari ili kutoa fursa ya kutosha kwa wananchi wengi kuuelewa na kuutolea maoni;

(c) “Utangulizi wa Muswada huu uwekwe vizuri zaidi ili wananchi waelewe madhumuni ya Muswada huu, kwani imeonekana wazi wananchi wengi wanadhani tayari tumeanza kuandika Katiba, kumbe lengo la Muswada huu ni kutunga Sheria ya Kuunda Tume ya Kukusanya Maoni tu.” (uk. 31-32)

Mheshimiwa Spika,
Katika kutoa maagizo haya, Bunge lilisitiza kwamba “... Muswada huu uko ndani ya Bunge, hauko serikalini.” (uk. 33) Hii ni kwa sababu, kwa mujibu wa kanuni ya 84(1) ya Kanuni za Bunge,Muswada ulikwishasomwa kwa mara ya kwanza na kupelekwa kwenye Kamati inayohusika kwa ajili ya kuanza kujadiliwa. 

Aidha, kwa mujibu wa kanuni ya 84(2) Kamati ilikwishaanza kupokea maoni ya wadau “... kwa lengo la kuisaidia katika uchambuzi wa Muswada huo.” Kazi iliyokuwa imebaki kwa Kamati ilikuwa ni kutumia mamlaka yake chini ya kanuni ya 84(3) “... kufanya marekebisho katika Muswada wa Sheria kwa kumshauri Waziri ... anayehusika na Muswada huo kufanya mabadiliko....” Ni baada tu ya kupata ushauri wa Kamati kuhusu mabadiliko ndio Serikali ingeweza kuleta Jedwali la Mabadiliko kwa lengo la kufanya mabadiliko katika hatua hii kabla Muswada haujaletwa Bungeni kwa ajili ya kusomwa mara ya pili na kwa mjadala wa Bunge zima.

Mheshimiwa Spika,
Hakuna hata moja ya maagizo haya ya Bunge ambalo limetekelezwa na Serikali. Tafsiri ya Kiswahili ambayo imeletwa Bungeni – pamoja na kuonyesha imesainiwa tarehe 8 Machi 2011 sawa na Muswada wa Zamani uliopigiwa kelele sana na wananchi – ililetwa kwenye Kamati wiki mbili zilizopita, ikiwa ni wiki moja baada ya Kamati kukataa kuujadili Muswada Mpya kwa vile ulifanyiwa mabadiliko na Serikali bila kupata ushauri wa Kamati kama inavyotakiwa na kanuni ya 83(4) ya Kanuni za Bunge. 

Badala ya kutekeleza maagizo ya Bunge, Serikali imeleta Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 ambao ulichapishwa katika Gazeti la Serikali la tarehe 14 Oktoba 2011.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. porojo za siasa

    ReplyDelete
  2. Katiba, ndio suala la muhimu zaidi kwa sasa.

    ReplyDelete
  3. Katiba, ndio suala la muhimu zaidi kwa sasa.

    ReplyDelete
  4. Akuna Uzalendo kila mtu anaangalia jinsi gani katiba itamnufaa yeye tu . Mngekuwa na uzalendo kitu cha katiba mpiya wala si cha kulumbana !
    mdau paris

    ReplyDelete
  5. CCM someni alama za nyakati hiki si kipindi cha zidumu fikra za mwenyekiti wa chama

    ReplyDelete
  6. Pongezi nyingi Lisu. Wasiojua maana ya maendeleo wanaziita porojo. Lakini kwa wanaofahamu katiba iliyokubaliwa na watu wote ndio msingi wa maendeleo kwa taifa.

    ReplyDelete
  7. Mdau Tue Nov 15, 08:29:00 AM 2011naona umeshindwa kuelewa nini kinaongelewa ukaishia kusema porojo za siasa. waachie wenye kuelewa wachambue kuliko kutuma kitu kinachokudhalilisha hata kama ni Anonymous

    ReplyDelete
  8. Read Bwetween lines acha unazi wa kisiasa utaelewa vyema..

    ReplyDelete
  9. usemacho ni cha ukweli tupu km mchangangiaje wa kwanza haelewi maaana basi usimueleze maana mtaishia hivyo kupotoshwa na wajinga km ..........wacha wachambuzi wachambue bwana hapa hakuna unazi ni ukweli mtupu ulioongelewa na Lisu

    ReplyDelete
  10. ukiona mtu anabisha ya tindu lisu,ana lake jambo, ajue yule ni mtaalam wa katiba na sheria,anazungumza kwa vifungu,hakurupuki.yuko ktk mstari,utabisha lakini mwisho wa siku utakubali.mawazo mgando ondoa tunaenda na muda(nyakati)katiba ndiyo hiyo,yaja,andaa hoja.

    ReplyDelete
  11. Wtanzania sometimes maboga kweli kweli yaani tangu Anonymous wa kwanza mpaka mimi hamna aliyechangia point kuhusu katiba bali kusemana tu

    ReplyDelete
  12. Kazi kweli kweli: Ujinga ni gharama; Watu ni wavivu kusoma; Hata Mbunge wangu wa Ilala bado hajasomo muswada ulio Bungeni kwa sasa, napia yule wa Mafia na wengine kama hao: Watu wakishindwa kusoma na kuchambua wanita hizi Porojo: Asante Lisu na wasaidizi wako kwa kukesha kuweka bayana haya yote: UZALENDO JUU, UBINAFSI NA UJINGA PIGA CHIN

    ReplyDelete
  13. Nakubaliana kabisa na bwana lisssu. Mimi ni CCM damu damu lakini hii katiba lazima ibadilike saaana haswa masuala ya power anayopewa Rais kufanya maamuzi bila kushirikiana na vyama vingine. Tukumbuke kuwa hii katiba ilikuwa ya chama kimoja sasa tuna vyama vingi na viongozi wa vyama vingine lazima wapewe nafasi katika maamuzi mazito kama haya ya katiba kama wote malengo yetu ni kujenga Demokrasia! We need more wasomi na wapigania haki kama Tundu Lissu! Haya hayakuanza leo tangu tukiwa chuo kikuu Tundu alikuwa ni mpenda haki! Go Tundu wale tunayoisoma katiba tunaelewa unachosema wengine ni lugha chafu na hata haki zao hawazijui

    ReplyDelete
  14. kweli Tanzania itajengwa na wenye moyo Tundu Lissu tunakutakia kila la kheri katika kusaidia Taifa letu tukipata watu kama wewe katika Bunge najua Taifa letu litasonga mbele.

    ReplyDelete
  15. A leader is like a decisionmaking machine .to manufacture any thing they need raw material in reaching creative thinking,the ideas and suggestions of others.Big man do not lough on big ideas because he knoes that it is possible but small individuals will lough because they know that it is impossible Tundu usijali tupo nyuma yako hapotoshwi mtu hapa watanzania tunaelewa chadema mnachokifanya

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...