Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina A. Chuwa akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu zoezi linaloendelea la uingizaji wa taarifa za sensa ya majaribio kwenye mfumo kwa kompyuta mara baada ya kumalizika hivi karibuni katika maeneo mbalimbali nchini. Kulia ni Mwakililishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu(UNFPA) DKt. Julitta Onabanjo.
Mwakililishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) DKt. Julitta Onabanjo (kulia) akiongea na waandishi wa habari kuhusu zoezi la uingizaji wa taarifa za sensa katika mfumo wa kompyuta mara baada ya kumalizika kwa sensa ya majaribio hivi karibuni. katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina A. Chuwa (kushoto)
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina A. Chuwa (kushoto) akiwa na Mwakililishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu(UNFPA) DKt. Julitta Onabanjo wakiangalia dodoso katika NBS lililotumika katika sensa ya majaribio iliyomalizika hivi karibuni.
Mtaalamu wa Kampuni ya DRS,Gabriel Kago (katikati) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu uingizaji wa taarifa zilizopo katika dodoso la sensa la majaribio katika mfumo wa kompyuta mara baada ya kumalizika hivi karibuni katika maeneo mbalimbali nchini. Kulia ni Mwakililishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu(UNFPA) DKt. Julitta Onabanjo na kushoto ni Mtaalamu wa Mifumo ya Komputya (IT) wa NBS Mwanaidi Mahiza.
Mtaalamu wa Mifumo ya Komputya (IT) wa NBS Mwanaidi Mahiza akimwonyesha Mwakililishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) DKt. Julitta Onabanjo (kulia) sehemu wa shughuli wazifanyazo.
Kamisaa wa Sensa Ofisi ya Taifa ya Takwimu,Paul Kimiti (katikati) akielezea kuhusu jinisi sensa ya majaribio iliyomalizika hivi karibuni itawawezesha kuimarisha maandalizi ya sensa hapo mwakani.Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO- Dar es salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...