Mwenyekiti wa chama cha demokrasi na maendeleo (Chadema),Freeman Mbowe akiwasili kwenye Ofisi za Jeshi la Polisi Mkoani Arusha leo asubuhi kwa ajili ya kujisalimisha kufuatiwa kusakwa na Jeshi hilo kwa tuhuma za kuvunja sheria.
Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe akiingia katika ofisi za mkoa za Jeshi la Polisi mkoni Arusha leo,aliyevaa nguo nyeusi ni Mbunge wa Viti Maalumu wa Chadema,Joyce Mukya akiwa amemsindikiza mwenyekiti wao kujisalimisha Polisi.
Mkuu wa Operation wa Jeshi la Polisi Mkoani Arusha,Saimon Pilo (kulia) akiwa amempokea Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe (katikati) katika Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kufanya nae Mazungumzo,wakati Mwenyekiti huyo alipofika Kituoni hapo Kujisalimisha leo asubuhi.Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalumu wa Chadema,Joyce Mukya alieongozana na Mwenyekiti wake.
Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe akiwa anatafakari jambo ndani ya Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa Arusha leo.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Freeman Mbowe akitoka kwenye Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha na kuelekea katika Ofisi ya Upelelezi Wilaya ambapo alielekezwa aende huko na Mkuu wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Mkoani Arusha.Picha zote na Woinde Shizza,Arusha.
Mimi si mshabiki wa chama chochote cha siasa, ila vitendo vinavyofanywa na viongozi wa CHADEMA ni ubabaishaji kutokujipanga na kukurupuka.. Kwa sababu polisi kuwafanyia fujo ni kuwapa umaarufu mkubwa kisiasa!kama walijipanga wasingekimbia polisi na kujificha bali wangekuwa bega kwa bega na wafuasi wao wakidai wanachokidai hadi kieleweke... Kinyume chake wao wamekimbilia kusikojulikana huku wakiwaacha wafuasi wao wakihangaika na kuumia wasijue la kufanya.. Jamani WaTZ wenzangu hapo ndipo mtajua kwamba likitokea la kutokea ndugu zangu mtapoteza familia zenu mkijuta msijue pa kukimbilia wakati wenzenu wameshapanda ndege na familia zao na kuwaacha mkiangamia... someni alama za nyakati ndugu zanguni.. CCM naichukia SANA, Lakini siwezi ipa kura yangu CHADEMA kamwe! mpaka sasa miaka 50 ya uhuru bado sijamuona kiongozi wa kutupeleka tunapopataka waTZ, Kuna angalau watu 2 ninaowaona CCM wenye uchungu na nchi hii ANGALAU, Wakianzisha vyama vyao ama wakisimamishwa na CCM kugombea naweza kufikiria kusimama kwenye mstari wa kupiga kura 2015.. I LOVE U TANZANIA.
ReplyDeleteENHEEE, Baada ya kuwasili ktk Ofisi ya UPELELEZI YA WILAYA?....
ReplyDeleteKwa nini nae asikamatwe?
Siku zote viongozi hawapati shida hata sasa wakati wananchi watanzania wanalalamika maisha ni magumu kwa viongozi wao si magumu. Kuhusu kuumia mpaka sasa familia zetu zinaumia kwa kukosa huduma muhimu za matibabu ukienda hospital daktari hatoi huduma mpaka utoe rushwa. mamia ya watanzania wanakufa hospitalini na wengine wanapata ulemavu wa kudumu kutokana na huduma mbovu za hospitali.
ReplyDeletendugu yangu uliyechangia mwanzo siku zote kuna watu ujitolea kwa ajili ya wengine ndio maana leo tunadai tupo huru kuna watu walipoteza ajira kipindi cha ukoloni na wengine kufungwa na baadhi yao kuuliwa. PAFUKAPO MOSHI UJUE KUNA MOTO.
MTOA MAONI WA KWANZA HUNA LOLOTE MAONI YAKO YAKO FINYU PIA YAMEKAA KICCM ZAIDI BADALA YA KUWA HURU MAANA HAYAKO HURU HATA KIDOGO WALE VIONGOZI WA CHADEMA KUKESHA KWENYE MKUTANO WA HADHARA WAKITAKA LEMA AFUNGULIWE NI KOSA? KATAFAKARI TENA ELIMU YAKO ULIYOSOMA CHINI YA MWEMBE
ReplyDeletemtoa maoni wa kwanza namshangaa saana kwani hakuna mabadililiko bila maumivu hata wewe ukitaka kutoka katika hali uliyonayo lazima upambane wewe unakua mtoto wa mama naaapa hakuna mtu wa ccm atakae leta mabadiliko unasahau ccm sio mtu ni institution na inaongozwa na misingi na misingi yake ndiyo hiyo ya mwendo wa kono kono angalia kilimo kwanza inavyokufa hata haina miaka 2 tafakari UWOGA WAKO NDIO UMASKINI WAKO NA NDIO UNATAKAO KULIMIT kwenda beyond ur potential
ReplyDeletewatakaoikomboa tanzania sio hao kina slaa wala mdoe watanzania kukosa elimu nani wa kumlaumu?tunajua sana huku tukijua wazi hatujui utajiri mkubwa mungu aliotupa ni mdomo watanzania mnaboa na mnatia aibu
ReplyDeleteCHADEMA NI CHAMA CHA WACHAGA HII IKO WAZI KABISA. MAFISADI NA UFISADI MKUVBWA UMEFANYWA NA VIONGOZI WA KABILA HILI. WENGINE WAMEPANDA HILO BANDWAGON KWA MASLAHI YAO. NA NYERERE ALITUONYA MSIJE MKAMUINGIZA IKULU MCHAGA NA............. .. WATANZANIA TUKAE MACHO.
ReplyDeleteNani asiyekufahamu we mchangiaji wa Kwanza..wewe si Anko wa Blogu au? nani asiyekujua unatetea ugali wako..mwaga mboga uone ccm watakavyomwaga ugali..Safari na Jk za kupiga picha zote zitaisha
ReplyDeleteWewe Ankal hayupo hivyo hujamsoma,,,huyo ni mchangiaji tu kama wewe na mimi.
ReplyDeletemdau wa kwanza wewe usipowapa kura sisi tutawapa, ushindi hauji bila maumivu labda uwe wa kifisadi, na maumivu yake yatafuata baadae tena makali.
ReplyDeleteCHADEMA=UCHAGGA + UKRISTO
ReplyDeleteUADILIFU UNA NGAZI 3 KUBWA:
ReplyDelete1.KWA MUNGU
2.KWA SERIKALI
3.KWA WAZAZI
Sasa je Daktari wa Kanisa Slaa alishindwa kuwa mwadilifu kwa MUNGU kwa kushindwa masharti ya Upadri.
Je atakuwa mwadilifu akipewa kuongoza serikali?
Jibu hapana, hawezi kuwa mwadilifu akipewa mamlaka ya serikali na pia kama hakuwa mwadilifu kwa Mungu na Serikali hata kwa Wazazi wake hawezi kuwa mwadilifu!
CHADEMA:::::
ReplyDelete1.Ijifunze kutofautisha kati ya UPINZANI WA KISIASA na UVUNJAJI WA SHERIA.
2.Ijifunze FAIDA ZA UPINZANI WENYE MALENGO KISIASA na MADHARA YA UVUNJAJI SHERIA.
Angalieni sasa ARUSHA na MBEYA ni miji ya kibiashara na ki pesa lakini sasa imekuwa ni vita tupu,hapakaliki,hapaliki, meter hazisomi,mizani hazipimi,ma droo ya maduka hayaingii pesa, shughuli za kiuchumi zime simama na njaa mtindo mmoja!.
Msikurupuke tu na kama mtashindwa hayo hapo juu ni BORA WACHAGGA na WANYAKYUSA M RE-NEW LESENI ZENU ZA BIASHARA na SIASA ITAKUWA IMEWASHINDA!