Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiwa na Balozi wa Tanzania Nchini Marekani, Ombeni Sefue alipomtembelea ofisini kwake mjini Washington DC, juzi.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiwa na Mzee Samwel Malecela na mkewe Anne Kilango Malecela pamoja na Mdau nchini Marekani, juzi.(Picha: Itikadi na Uenezi CCM).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Nape baada ya kusikiliza interview voice of America, I have a confession to you! I used to challenge you kwasababu sijawahi kuusoma moyo wako. Lakini sasa hivi nimeusoma moyo wako and I found you are a true leader and visionary! You really love your country and your people. I liked you from the beggining and I will continoue to pray for you and support you. I need our friendship back please! You will always have my support and prayers and worry not God is with you no one will harm you! whomever trying or planning doing evil against you GOD will provide army from heaven and destroy all your enemies! I really like the interview was tough and you answer all questions with great wisdom. May God bless you and your family. You gat my support brother.

    ReplyDelete
  2. Shomari, maswai ulyoyauliza ni kama vile ulikuwa unaniuliza mimi kuwa uulize nini halafu mimi ndio nakupa hayo maswali nawe unampa Nape. Kweli wewe mkali, umeuliza vizuri sana.

    Nape nilikuwa simjui vizuri zaidi ya kumuona kwenye magazeti mitandaoni, lakini anaonekana nae pia si kidogo ingawa kuna maswali mengine hakuyajibu vyema. Anasema sana mpaka wakati mwingine anapoteza maelezo ya swali aliloulizwa na kuonekana kama ameshindwa au anakwepa kujibu swali. Lakini kwa asilimia kubwa ameongea vizuri na anaweza kuwa kiongozi mzuri baadae.

    ReplyDelete
  3. Huyu ndugu nami sijawahi kukutana naye wala kusikia hotuba zake zaidi ya postings anazoweka pale JF (ambapo huwa anatumia lugha isiyolingana na wadhifa wake). Kwa kusikiliza mahojiano haya nimeamini ni kijana mweledi wa siasa na anasimamia anachokiamini. Nimefurahi sana kuona kwamba ndani ya CCM kuna watu kama hawa wanaoona ukweli na kuusimamia kwa nguvu zao zote. Wasiwasi wangu ni huo huo anaoeleza mwenyewe: utamaduni wa siasa za Tanzania wa kuwa na 'miungu watu' katika vyama vya siasa na hatimaye katika utawala wa serikali. Hiki ni kisiki kama sio kigingi kikubwa ambacho kinaweza hata yeye mwenyewe kumsababishia mweleka. Vinginevyo amefafanua hoja zake vizuri sana na nimebadilisha mtazamo hasi niliokuwa nao kwake.

    ReplyDelete
  4. Hivyo viwanja unavyosema vya michezo unavyosema ni vya CCM? una uhakika huo? Pili unavyosema wanasiasa wasijihusishe na biashara, je hiyo migodi mnayomiliki ni vipi? Si biashara hiyo?

    ReplyDelete
  5. Balozi Sefue ni Permanent Representative kwenye Permanent Mission Of Tanzania to the United Nations, New York, sio Washington DC. Balozi wetu Washington DC ni Hon. Mwanaidi Maajar

    ReplyDelete
  6. hiki ni kichwa ambacho wana CCM wanatakiwa kijivunia nacho. Mimi siipendi CCM yaani siipendi ila sina la kufanya ila huyu bwana akisimama katika uraisi naweza kumpa kura yangu, ila naamini yupo peke yake CCM nzima, sasa sijui atatawalaje. Nape nakushauri hamia vyama vyingine vyenye misimamo kama yako huko CCM wataku-sokoine

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...