Wazabuni
wanaowania kujenga Daraja la Kigamboni leo wamekutana katika kikao maalum
kuangalia michoro ya daraja iliyochorwa na msanifu wa kazi hiyo kutoka nchini
Misri.
Wazabuni hao ni
kutoka makampuni 7 ya kimataifa ambayo yameteuliwa kuingia mchakato rasmi wa
kondrasi ya kujenga daraja hilo.
Msanifu huyo Bw.
Mohamed Shohayeb (pichani) kutoka Arab Consulting Engineers aliwaonyesha Wazabuni hao
michoro ya jinsi daraja litakavyokuwa. Shughuli hiyo ilikuwa chini ya Mkurugenzi
wa Mipango na Uwekezaji wa NSSF Bw. Yacoub Kidula na ilihusisha watalaam kutoka
NSSF na Serikalini.
Baada ya zoezi
hilo, Wazabuni walipelekwa kwenye eneo litakapojengwa daraja hilo huko
Kigamboni kujionea wenyewe hali halisi. Kilifuata kipindi cha maswali na majibu
ambapo Wazabuni waliuliza Msanifu maswali ili kupata ufahamu zaidi wa kazi hiyo
kabla ya kurudi makwao na kuwasilisha gharama zao za ujenzi.
Tarehe ya mwisho ya kuleta maombi ya kazi
hiyo ni 15 Desemba 2011 ambapo maombi hayo yatafunguliwa hadhrani na mshindi
atakaejenga daraja hilo
kutangazwa rasmi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...