Askari Polisi wakijalibu Kutuliza Ghasia katika eneo la Mwanjelwa jijini Mbeya wakati wa kuwatawanyisha Wamachinga waliokuwa wameanzisha vurugu leo.hali bado ni tete jijini humo mpaka hivi sasa na inasadikiwa kuwa watu kadhaa wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa.
Baadhi ya Wamachinga wa jijini Mbeya wakiwa Tayali kwa ajili ya Kupambana na Askari Polisi kikosi cha FFU wakati wa tukio hilo leo.Wamachinga hao wamefika katika ofisi za Watendaji wa Kata ya Sinde na ile ya Uyole na kuziharibu haribu ofisi hizo kwa madai kwamba hazina sababu ya kuwepo,kwani wao wanataabishwa kwa sababu ya watendaji hao.
Baadhi ya Wamachinga Mbali mbali wakikimbia katika eneo la tukio wakati machafuko hayo yamepamba moto.
Baadhi ya wananchi wakiwa wameokoka katika eneo hilo.
Watu Mbali Mbali wakiwa wanakimbia ili kujiokoa na Hatari katika eneo hilo.Picha na Latest News Blog.
Serikali ya Tanzania na Polisi wenu jifunzeni alama za nyakati. Huu si wakati wa ubabe tena. Tunakoelekea kutakuwa kubaya zaidi kwani watu hawaogopi polisi tena.
ReplyDeletehuyu mweshimiwa kandoro hana plan anawapa watu hasara huku hawajui wataenda wapi wala watakula nn.anachojua nikutumia polisi na kuwapa hasara wananchi wanaojitafutia riziki.mm nawaunga mkono wamachinga haki haitoki mbinguni ila inadaiwa ukienda kwenye madini ni hivyo hivyo hivyo mnawafukuza wananchi waende wapi na mungu aliwapa madini hayo?huoni ni onevumabadiliko yanakuja hatujalala kama miaka iliopita mungu wabariki wamachinga mungu bariki tanzania.,
ReplyDeleteeh! muziki huu wa kina Ras Makunja sasa unechezeka mbeya? kweli bongo tambarare
ReplyDeletePolisi na viongozi wa Tanzania wana mentality za kizamani sana, hawaelewi kuwa siku hizi mambo no tofauti.
ReplyDeleteSiku hizi hata waziri haheshimiwi kama zamani, mnapishana tu barabarani kama vipi hakuna cha 'salamu mheshimiwa', kama vipi aanze yeye kusalimia.
Iko siku,,,na siku inakuja,,,ambapo nguvu ya umma itachukua nafasi yake! Mwenye sikio na asikie!
ReplyDeleteWachina wao ruksa kuwa wamachinga, watz no tena kwa bakora, nawaunga mkono halafu waseme chadema wamewatuma
ReplyDelete