"Karibuni jamani..." Rais Kikwete akimkaribisha Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Mbowe aliyeongoza kamati ya uongozi ya chama hicho kwenda Ikulu na kufanya maongezo juu ya mchakato wa kupata katiba mpya. 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wa Serikali yake leo, Jumapili, Novemba 27, 2011, amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Mazungumzo hayo, yaliyofanyika Ikulu, Dar Es Salaam, yamefanyika katika mazingira ya urafiki na ujumbe wa CHADEMA umewasilisha mapendekezo yake kuhusu mchakato wa kuandika Katiba Mpya ya Tanzania. Serikali imepokea mapendekezo hayo.

Hata hivyo, pande zote mbili zimekubaliana kukutana tena asubuhi ya kesho, Jumatatu, Novemba 28, 2011 kuanzia saa nne kamili, ili kuipa nafasi Serikali kutafakari mapendekezo hayo.

Lakini pande hizo mbili zimekubaliana kuwa Katiba ya sasa ni Katiba nzuri iliyolilea Taifa kwa miaka 50 iliyopita kwa sababu ni Katiba ya sasa iliyoliwezesha Taifa la Tanzania kuwa na amani,  utulivu na kupata maendeleo makubwa ambayo nchi yetu imepata mpaka sasa.

Pia pande zote mbili zimekubaliana kuhusu umuhimu wa kutunga Katiba Mpya kama Mheshimiwa Rais Kikwete alivyoliahidi taifa wakati wa salamu zake za mwaka mpya Desemba 31, mwaka jana, 2010, Katiba ambayo italiongoza Taifa la Tanzania kwa miaka mingine 50 ijayo.

Katika mazungumzo hayo, Mheshimiwa Rais aliwahakikishia wajumbe hao wa CHADEMA wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Mheshimiwa Freeman Mbowe, kuwa ni dhamira yake na ya Serikali yake kuhakikisha kuwa Tanzania inapata Katiba mpya.

Katika mkutano huo, pande zote mbili zimekubaliana kuwa ni jambo muhimu sana kwa mchakato mzima wa kutungwa kwa Katiba Mpya kuendeshwa kwa namna ya kulinda na kudumisha tunu za taifa za amani, utulivu na umoja wa kitaifa.

Aidha, pande zote mbili zimekubaliana kuwa mchakato huo uendeshwe kwa kuzingatia misingi ya mambo mengine muhimu kwa taifa la Tanzania kama vile kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani, kuligawa Taifa kwa misingi ya udini na ukabila ama kutugawa kwa misingi ya maeneo.   

                                      IMETOLEWA NA:
 KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
NOVEMBA 27, 2011
DAR ES SALAAM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Tunashukuru sana kwa taarifa yenye kutia moyo

    ReplyDelete
  2. mavuvuzela wapo wapi?pale sio ukumbi wa bunge nisehem nyingine wenyewe wanaelewana macho mtoke wengine siasa sio uadui fitina wala chuki vijana mpo?endelezeni mapambano ya kinafiki waarabu ni watu wengine sio sisi wabongo wala msijifananishe na waarabu wenye msimamo wao

    ReplyDelete
  3. kwa kweli hapo rais amekuwa muungwana na natumaini ataelewa nia njema waliyo nayo CDM tofauti anavyopotoshwa na wasaidizi wake. kwa kweli rais ameonyesha kuwa ni mtumishi wa watanzania na sio mtawala. ndio Tanzania tunayoitaka maana tulikokuwa tunaelekea ni pabaya nashukuru rais ameliona hili mapema.

    ReplyDelete
  4. Mimi nipo nje ya Bongo na si shabikii chama chochote cha siasa Duniani bcoz wanasiasa wotw siwaamini.CCM siipendi coz sioni wnachokifanya lkn nataka kusema kitu1 tu.Huyu kikwete anashutumiwa kwamba ni mshikaji sana na serikali yake pia ni yakishkaji,huenda ikawa nikweli lkn naona sio mara zote kwamba ushkaji ni tatizo.Angalia sasa kwa ushkaji wake amkubali kuonana na Wapinzani au mahasimu wake wakuu CHADEMA,hivi angekua MKAPA angefanya hivi?Hivi mkapa aliwahi kuongea na upinzani hata mara1 katika utawala wake wa miaka10 au ndo kusema mtutu wabunduki ndo solution na ndio utawala makini na shupavu..Just maswali tu najiuliza loudly..

    ReplyDelete
  5. Nampongeza rais Kikwete kwa kukutana na CDM tunaelewa kila mmoja wetu ana nia nzuri na nchi yetu...let agree to disagree. Rais kuwa na uamuzi wake wa kukutana na CHADEMA ni hatua kubwa sana katika kuwasikiliza watu wake. Nafurahi kuwa hakupotoshwa na NEC au CC waliotaka aonane na vyama vyote ilhali CDM ndiyo walioomba. Big up president Kikwete hiyo ndivyo inavyotakiwa uwe na uamuzi wake pia.

    ReplyDelete
  6. Sote tunampongeza JK kwa busara hizi. Hivi ndivyo tunavyoweza kuwa na taifa lenye demokrasia na ndio maendeleo yatakapopatikana.

    Naungana na mdau hapo juu kwamba ingekuwa Ben pasingekalika hapo. Wala asingekubali kuonana na CHADEMA

    ReplyDelete
  7. JK hongera kwa busara zako.
    Sasa muwasikilize CHADEMA kwani madai yao ni ya msingi nasi wananchi tunayakubali. Ila kura tutaendelea kuwapa CCM. CCM msiwe na wasiwasi ulaji utaendelea kuwa wenu. Tunachotaka mbadilike tu.

    ReplyDelete
  8. I told you all, JK is smart.

    ReplyDelete
  9. UUNGWANA NI VITENDO!!!...Hongera JK kwa kuvunja kuta zilizopo...kwa vile kigezo cha uongozi bora msingi wake ni mabadilishano ya hoja na rai kwa njia isiyo na urasimu.

    ReplyDelete
  10. Mmemwona tundu lissu alivyoweka 4 mbele ya rais ndio nini?. Huyo ni mwanasheria, akina sisi tutafanya nini. Sheria inasema lazima kuheshimu madaraka, pale Ikulu sio kwa yeye kikwete ila ni sehemu ya dola ya Tanzania. Sasa mbona haiheshimu dola? Just observing. CDM haina makosa, baadhi ya watu wanakiharibu chama.

    ReplyDelete
  11. Jamani hivi huyu mbowe na kila lisu sindio walioongoza kutoka bungeni kwa madai kuwa hawamtambi Jk kuwa ni rais sasa leo wameenda kumuona , halafu hivi mbona vyama vingine vikienda kuongea na serekali chadema wana waita wasaliti? Au kwa upande wao ni sawa ila kwa wengine ni noma? Tumeona chadema hakikubaliani na cuf hata swala la kule znz wakidai kuwa cuf wamehongwa madaraka je jk akikubali mapendekezo yao tuwaiteje?

    ReplyDelete
  12. Kikwete amekubali kuonana nao kwasababu anajua amekosea. Anajua CHADEMA wana point na wananchi walio wengi wanajua hilo. Ila amekubali kupunguza tension na ku-buy time. Ni mchezo wa kisiasa tu.

    Ni kama CUF kule ZNZ: sio kwamba CCM walitaka kuwa nao, ni kwamba walifika mahali wakaona CUF wanaweza wakashinda siku moja, itakuwaje?. Wakaona bora nusu shari kuliko shari kamili. Baada ya mapambano ya miaka mingi, wakasema tuunde SERIKALI YA PAMOJA. Ina maana hata CUF siku wakishinda, bado CCM watakuwa kwenye serikali. Hawatoki. Hata huku bara, siku ukiona CHADEMA wanaelekea kushinda, tegemea wazo la SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA kutoka CCM.

    ReplyDelete
  13. Mh! Kwani kuweka 4 ndo makosa gani kukosa heshima kivipi??? We Anon wa Nov28,08:39:00am umechemka.

    ReplyDelete
  14. Nchi wahisani ndio wameshinikiza huu mkutano. Wahisani wanahofia Taifa litatumbukia kwenye vurugu na matokeo yake watapoteza investments zao.

    ReplyDelete
  15. Wewe Anonymous wa 12:47:00 mshamba, ndiyo wale wale wachochezi. Unamhusisha Mkapa na mkutano huu wa Rais na CDM kwa vipi? Kwa wakati wake hakukuwa na jambo lolote wapinzani waliloomba kukutana. Sasa unahukumu vipi kwa kipimo kilichopita? Acha Rais Kikwete atimize wajibu wake kwa wakati huu, na siyo kurejea mambo ya nyakati za enzi za mawe. Kama huna cha kuandika si ukae kimya na kusoma waandikayo wenzako wakomavu wa fikra!!

    Kwanza wewe hutufai maana umekimbia nchi uko nje kwa mujibu wa maelezo yako mwenyewe.

    Kabebe mabox upate mlo, Siasa huiwezi. Huna mchango wowote na nchi hii, tunataka utulivu sasa, na siyo chokochoko na uchochezi.

    Ankel, mwekee asome ili ajifunze. Hatuwataki wanafiki Tz.

    ReplyDelete
  16. Hongera Rais wetu! Ni aibu iliyoje au ni chuki binafsi ya mchangiaji wa kumi? Hata hamfahamu Tundu Lissu kwa sura maskini! Kamuona Mzee wetu Affi amejikalia kwa nidhamu ya kiutu uzima tayari anamshambulia Tundu Lissu...Shame on you!

    ReplyDelete
  17. Hawa chadema wali susa hata kumsikiliza jk aoipoenda kuhutubia bunge wakidai hawwmtambui nakumbuka jk aliwajibu akasema waacheni waende wakiwa na shida watakuja kwangu kwani mimi ndie mlezi wa taifa leo tumeyaona, pili hawa chadema wanachekesha sana vyama vingine wakienda kukutana na serekali wanawaita kua ni ccm B sasa wao tuwaiteje? Tumeona mpqka leo wanawatukana Cuf kuwa muungano wa serekali iule znz ni usaliti sasa je kama ccm wakikubali mapendekezo yao tuuite usaliti?

    ReplyDelete
  18. he mwe! thatha inji hii inaelekea kule watu tunapenda "laithi" anakaa kitako kuthikiridha wapindhani wake ili tu KUJENGA TANZANIA TUNAYOITAKA LEO NA KESHO; MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU MBARIKI KIKWETE!
    heshima
    umoja
    na
    amani

    ReplyDelete
  19. Dai michuzi, matukio ya mkutano wa leo yako wapi usituache roho juu juu!! Tuna hamu tujue muafaka walioufikia. Hata hivyo shukurani kwa kutuhabarisha. Keep it up!!1

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...