Jamani, hivi mnalikumbuka hili shairi?
kama mlisahau basi enjoy!!!
Mdau
-------------
 
Hadithi inayokuja, ni ya sungura sikia
hadithi uliyongoja leo ninakuletea
Alitoka siku moja njaa aliposikia
njaa aliposikia sungura nakuambia

Siku hiyo akaenda porini kutembelea
akayaona matunda mtini yameenea
sungura akayapenda mtini akasogea
Mtini akasogea sungura nakuambia

sungura karuka ruka lakini hakufikia
matunda hakuyashika mikononi hakutia
hakika alisumbuka nguvuze zikapungua
nguvuze zikapungua sungura namwambia

SIZITAKI MBICHI HIZI, sungura akagumia
naona nafanya kazi bila faida kujua
yakamtoka machozi matunda akalilia
Matunda akalilia Sungura nakuambi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 33 mpaka sasa

  1. Tuma salamu kwa watu watatu.............

    ReplyDelete
  2. Vema sana mdau kwa kutukumbusha mambo ya shairi la sungura.Tupe na ile ya Karudi baba mmoja na lile la Azimio la Arusha.

    ReplyDelete
  3. kamili hii hapa

    Hadithi inayokuja, ni ya Sungura sikia,
    Hadithi uliyongoja, leo ninakuletea,
    Alitoka siku moja, njaa aliposikia,
    Njaa aliposikia, Sungura nakuambia


    Siku ile akaenda, Porini kutembelea,
    Akayaona matunda, mtini yameenea,
    Sungura akayapenda, mtini akasogea,
    Mtini akasogea, Sungura nakuambia.


    Sungura karukaruka, lakini hakufikia,
    Matunda hakuyashika, mikononi hakutia,
    Hakika alisumbuka, nguvuze zikapungua,
    Nguvuze zikapungua Sungura nakuambia.


    Mtazame hapo juu Sungura amelegea,
    Mtazame na miguu, matunda anarukia,
    Atafanya sikukuu, matunda akifikia,
    Matunda akifikia, Sungura nakuambia.


    Karuka tena karuka, matunda akarukia,
    Mwisho Wave akachoka, kachoka hata mk-Ia,
    Penye mti akatoka, pembeni akasogea,
    Pembeni akasogea, Subgura nakuambia.


    “Sizitaki mbichi hizi” Sungura akagumia,
    “Naona nafanya kazi, bila faida kujua”,
    Yakamtoka machozi matunda akalilia,
    Matunda akalilia, Sungura nakuambia.


    Sio kama hakutaka, sasa nakupasulia,
    Matunda aliyataka, ndiyo kisa akalia
    Tunajua hakufika, alichoka kurukia,
    Alichoka kurukia, Sungura nakuambia.


    Hadithi nimemaliza, nimekwisha simulia,
    Jambo moja sikiliza, rafiki yangu sikta,
    Usikose kujikaza, mazuri kukazania,
    Utamshinda Sungura, utapata mbivu hizi.

    ReplyDelete
  4. DUUUUUUUUH UMETUKUMBUSHA MBALI SAAAAAAN

    ReplyDelete
  5. Karudi baba mmoja toka safari ya mbali
    kavimba yote mapaja na kutetemeka mwili
    watoto wake wakaja ili kumtaka hali
    wakata na kauli iwafae maishani

    Akatamka mgonjwa ninaumwa kwelikweli
    hata kama nikichanjwa haitoki homa kali
    roho naona yachinjwa kifo kinanikabili
    kama mwataka kauli semeni niseme nini

    endeleza ...

    ReplyDelete
  6. Da kweli watu mna hazina - umenifanya nikumbuke mengi na watu wengi waliotutangulia mbele ya haki. Mara baada ya CCM kuzaliwa kuna wakati tulikuwa tukiimba kibwagizo cha "CCM,CCM, CCM...!" kwenye huu mwimbo. Jamani nyimbo za mchaka mchaka vipi, hasa JKT tukumbushane jamani...

    ReplyDelete
  7. Wao, mnanikumbusha darasa la nne n shule ya msingi ya Jamuhuri DSM. Pia inaleta kumbukumbu ya waliotutangulia kama mwalimu wangu kipenzi Salama Thabit/Salama Mfamau, Mwl Tausi Mchopanga, Classmate wangu John Njakale.
    Mila awalaze mahala pema peponi. Amen

    ReplyDelete
  8. ebwana eeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee du we mdau unakumbukumbu ile mbaya vipi ile hadithi ya kibanga ampiga mkoloni wadau mnaikumbuka au pazi mtoto shujaa du kweli tumetoka mbali

    ReplyDelete
  9. Lugha ingefundishwa mashuleni kwa kutumia tungo kama hizo, nadhani elimu ingekuwa juu. Wakaja wale wajanja, wenye akili potovu,
    Wakaanza zao tungo, zenye siasa za chuki.
    Wakapandikiza tungo na hadithi za kilimo,
    huku wao hawalimi, bali wezi wa kalamu.

    Wengi wao wadiriki, kusomesha watoto ng'ambo, hali wao wasimama kudanganya wa masikini.

    Twataka karumekenge, na riwaya za abunwasi, tumechoka longo longo na siasa za kichina.

    ReplyDelete
  10. ASANTE KWA KUNIKUMBUSHA MBALI,NAOMBA ANAYELIKUMBUKA SHAIRI LA IDD AMINI JASUSI JOKA HILI NI JOKA KUU,ALIMWAGE HAPA PIA

    ReplyDelete
  11. Ebwaeee!!!! hiyo haitoshi hata watoto wavivu walikua na shairi lao
    SIKIRI MIMI MASIKINI,
    UVIVU WANGU NYUMBANI
    UKIWA HUU NJIANI
    NAKUFA HAPA KWA NINI?

    ReplyDelete
  12. Hapo Mdau umepiga Pentagon...SIZITAKI MBICHI HIZI NI NGANO YA WAZANZIBAR KUUKATAA MUUNGANO HUKU WAKIJUA WAO NDIO WANANUFAIKA NAO SANA TU!!!!
    <<<>>>

    ReplyDelete
  13. Dah umetukumbusha mbaaaali sana mpaka chozi limenitoka! those were he OLD good days that will NEVEr roll back! Aiseee ..kisa cha madenge na mandawa ! HERI MIMI SIJASEMA ! BABU ANAPULIZA CHAI KIJANNJA KWA KUSEMA WATOTO NAWASIFUUUU! HII NYUMBA INA SIAFUUUUU! DAH! those were th days

    ReplyDelete
  14. namshukuru sana mdau aliyetukumbusha hizi tungo, hii ndio iliyokuwa elimu sio sasa hivi. mimi nilisoma kijijini lakini shairi hili niliimba darasa la tatu na la nne, tena wakati huo kitabu kimoja wanafunzi watatu, lakini leo hii kila mtu anatoa kitabu mitahala haieleweki mara masomo ya sayansi kimu yameondolewa matokeo yake watu wanamaliza darasa la saba hawajui kusoma wala kuandika,lakini hata kupika kufua hawajui. Tungo hizi zilitufundisha maisha ukakamavu na mambo mengine sasa hivi sijui hata wanasoma nini maana ukienda sekondari za kata mtu hata jina lake hawezi kuandika, ukimuuliza Kigoma iko wapi anakuambia ipo nchi za njee. Jamani turudie mitaala ya nyuma na jiografia tufundishe watoto waijue hata dunia ikoje.
    Namshukuru sana Mdau kwa Kutukumbusha ila na wadau wa elimu waangalie kwa mtazamo tofauti ili tuboreshe elimu

    ReplyDelete
  15. tuwekeeni na sikukuu ya sabasaba ilianza julai saba, wakoloni kuwakaba, sikukuu ya sabasaba,ooooooo, jamani wanalijua zaidi waendeleze. maana nalo zuri sana

    ReplyDelete
  16. JAMANI EE MBONA MMELISAHAU SHAIRI HILI
    Karudi baba mmjoa toka safari ya mbali
    kavimba yote mapaja na kutetemeka mwili
    Watoto wake wakaja aili kumtaka hali

    wakakata ta shauri liwafae maishani

    ReplyDelete
  17. Asante wadau mlioweza kukumbuka mashairi mengine...Zamani tulikuwa tunafundishwa bwana hadi leo mashairi yako vichwani..kama alivyosema mdau mmoja hapo juu wakaja wajanja wakaanzisha nyimbo za siasa..

    SIKIRI MIMI MASIKINI..Weee nilikuwa naogopa kweli wimbo huo..Watoto wasingeweza kuzamia mijini kama ilivyo sasa

    David V

    ReplyDelete
  18. EE jamani blog ya Michuzi ina mambo,,,EE kweli kiswahili ni lugha ya kujivunia sana,nawashangaa hao wanaopenda kuvuruga kiswahili eti wanajifanya hakuna maneno ya kiswahili kukamilishia sentensi zao,,wanaweka kithungu,,yaani Swanglish,yaani huwo ni ushamba wa hali ya juu,,,hayo mashairi nani aliyatunga jamani,,basi kamilisheni na hizo tungo zingine Idd Amin,Karudi baba mmoja na sikiri mimi masikini(hivi kwani ni sikiri au fikiri mimi masikini?),Azimio la Arusha...Ahlam UK

    ReplyDelete
  19. Wengi wanakumbuka mengi kama vile tumbo niachie nimwachie madenge, ila maisha ya ulimwengu yamewashinda akili ya shule ukiwa nayo huku akili ya maisha huna ni upuuzi tu kwangu.Unapaswa umanage school na elimu dunia.

    ReplyDelete
  20. Ndio kweli kabisaa...Wazanzibar ndio wanaonufaika na Muungano lakini wanaleta ...SITAKI NATAKA ...SIZITAKI MBICHI HIZI...ukiona Mzanzibar analalamikia Muungano ujue ajira tatizo hana pesa ana njaa...mfano Maalim Seif alikuwa mpinzani mkubwa wa Muungano je? sasa anaongelea kuvunja Muungano???... hapana ameona pana Maslahi!!!!!!

    ReplyDelete
  21. Wimbo wa JKT:

    Idd Amiini akifaa, mimi siwezi kulia,
    Nitamtuupa Kageraa, awe chakuuula cha mambaa.....

    Je mnaikumbuka pia ile hadithi:

    Mama kanambia winga Kuku,
    Nami siwezi kuwinga Kuku,
    Nimekalia Kiteletele,
    Mtama wa mama waliwa na ndege....

    ReplyDelete
  22. Idd Amin Jasusi, tena hili joka kuu, limefanya uvamizi kuiteka ardi yetu.
    Hatuna kazi nyingine ni kulifunza adabu ndipo litakapojua Tanzania ni ya watu.
    Kwa kweli hatukutaka kuchezewa na shetani mengi tumevumilia dunia ina habari.
    Katumwa na mabeberu kuja kutuangamiza, Idd amini malaya .. wa kwanza mwafrika........

    ReplyDelete
  23. Wadau hii imenikumbusha mbali sana!

    ReplyDelete
  24. Sikiri mimi maskini, uvivu wangu nyumbani, ukiwa huu njiani nakufa hapa kwa nini,Sadiki sasa ashiba chakula kingi kwa baba,....Nimekosa baba na Mama nisameheni. Enzi za mafunzo tabiti kwa vijana, na hadithi ya sungura ikiwafunza kuwa madhubuti na kutochukulia vitu kama ni haki yao ya msingi badala yake ni kutokana na utendaji kazi...Naamini.AHERI ZAMANI...Mashairi ya saadani, Chonya of chilonwa me!! na mengi mengi yaiwafunza vijana stamina ya maisha... JKT ....Eee mola wetu tubariki tuelewe tuendako, ututoe katika kiza na utuwezeshe kuuthamini utamaduni wetu na mila na desturi zetu...Vinginevyo ndiyo mambo ya bwana Cameron kutuambia bila ya kukubali ushoga hakuna misaada.....INASIKITISHA

    ReplyDelete
  25. Huo wimbo wa Idd Amini umenichekesha sana, inaonyesha jinsi gani serikali ilikuwa inamuogopa hadi wakamtungia wimbo, Jamni siku hizi kuna mchakamchaka mashuleni? T'was very nice in those days we have to go to school 6am because of mchakamchaka. Ndo maana siku hizi watoto wanawaza tu mapenzi maana hakuna mazoezi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mchakamchaka utoke wapi wakati watoto wanakuja kwa school bus wawahi class

      Delete
  26. Mimi sidhani kuwa shairi hili linawagusa wazanzibari musiwapige madongo ni haki yao ya msingi kama ilivyo kwa mimi,nyinyi na wengine kwalolote lile unalohisi unanyongwa. Kwani muungano huu ni wa ridha ya viongozi tu waanzilishi na unaenziwa kwakuwa tu mwalimu yumo na hatajwi kwa makosa yake.

    Muundo wa muungano ndio zimwi likulalolisokwisha. kama zanzibar inafaidika ndio haki yake na kama wanakosewa ni haki yao kupiga kelele na kama hazisikilizwi basi hakuna lisilo na mwisho watafika na kufunguka kutoka katika dema liliundwa na mvuvi mwalimu.

    kwamaoni yangu sungura huyu mjanjambile ni CHADEMA juu ya mchakato wa kutunga sheria ya katiba ambao waliulilia njaa na kupelekwa shambani wakashindwa vuna matunda yake kwa ubole wao wa kujitwisha ujanja pori wa kurukaruka.

    Sikuzote ndege mjanja hunasa kwenye tundu bovu lakini mara hii sungura Mjanja hunasa mtegoni tena aliyeutega mwenyewe.
    Mjomba usinibanie

    ReplyDelete
  27. hahaha na hapa mabata wadogo dogo wanaogolea katika shamba zuri la bostani duuu kweli ilikuwa raha zamani bila ya kusahau maua mazuri yanapendeza ukiyatizama ukayechekela hakuna mmoja asiyependeza zumm zummm ee mama nyukiliaa ee

    ReplyDelete
  28. OLD GOOD DAYS FOR REAL! HIVI NAWEZA KUPATA WATU HIVI VITABU VYA ENZI ZILE, PAMOJA NA CHA JUMA NA ROZA

    ReplyDelete
  29. Anonymous wa Fri Nov 18, 05:50 PM 2011

    UHUSIANO WA WAZANZIBAR NA SHAIRI LA SIZITAKI MBICHI HIZI!

    Umenifurahisha sana kwa vile sasa lengo la mshairi kutupa mistari limetimia!

    Ninakukumbusha kuwa Mashairi,Methali,Nahau na vingine huwa na lugha za mafumbo na wakati mwingine hutoa maana kinyume nyume, au maana kwa misingi ya ulinganishi wa mambo halisi...MFANO WA SIZITAKI MBICHI HIZI ..NA MSIMAMO WA KI SIASA WA WAZANZIBAR...hii ndio sanaa ya ushairi bana!

    ReplyDelete
  30. Asante sana, ila wadau wamalizie tungo hizo za Karudi baba mmoja..
    na Azimio la Arusha pia Ninaye ndege mzuri hadi raha....

    ReplyDelete
  31. Hilo shairi msianze kuhusisha na siasa... Hiyo ni lugha iliyotumika kwa hadhira iliyokuwepo na wala siyo siasa kama wengine wanavyotaka tuamini

    ReplyDelete
  32. BABA ANA NG'OMBE

    Huyu ni Baba,
    Baba ana ng'ombe.
    Ng'ombe wake ni mweusi
    Baba anasema, kimbia ngo'mbe.
    Kimbia upesi, Kimbia nyumbani.
    Baba ananjaa.

    Wiki ijayo tawaletea hadithi ya Juma na Roza ila mniambie kama hii mmeipenda na ijayo mnaihitaji!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...