Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi iliyokutana kwa siku mbili kuanzia tarehe 23-24 Novemba, 2011 mjini Dodoma chini ya Mwenyekiti wa CCM, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na mambo mengine imeazimia yafuatayo:

UNUNUZI WA MAHINDI

     I.         Halmashauri Kuu ya Taifa imeipongeza Serikali kwa kuwa na mkakati wa kutafuta fedha haraka kwa kuamua kuuza mahindi tani 80,000 kwa UNFP na nchini Kenya ili kwanza, kulipa madeni ya wakulima, na pili, kununua mahindi ya wakulima yaliyopo majumbani na kwenye vituo vya ununuzi kabla ya upandaji wa msimu mpya haujaanza.



   II.         Imeipongeza pia Serikali kwa kuruhusu uuzaji wa mahindi nje ya nchi, hali ambayo itasaidia mahindi yaliyobaki kwa wakulima kupata soko. Hata hivyo, imesisitiza kuwepo na tahadhari sasa na siku zijazo, ili chakula chote kisiuzwe nje ya nchi na kusababisha tatizo la njaa nchini.



   III.         Imeitaka Serikali iimarishe Wakala wa Chakula wa Taifa kwa kuuwezesha kwa fedha zaidi na kujenga maghala mengi na makubwa zaidi ili uweze kununua kiasi kikubwa cha mazao.



  IV.         imeiagiza Serikali ihimize kuundwa kwa Vyama vya Ushirika vya Mazao ya Chakula, ambavyo navyo viwezeshwe kujenga maghala ya kuhifadhi nafaka katika maeneo yao pamoja na kuanzisha mfumo wa ununuzi wa mazao wa stakabadhi ghalani.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. repoti hii inasikitisha sana,unajua tunakoelekea TUNAONGOZWA NA VIPOFU NA HAWAJUI DUNIA IMETOKA WAPI NA INAENDA WAPI,leo hii hakuna siri.Mfano wanasema Vyuoni watu wasivae Sare za vyama,wakati Mzumbe Morogoro hadi kadi za CCM zinatolewa ndani ya Chuo na Sherehe za CCM zinafanyikia ndani ya Campus.
    Pia Vurugu za Majiji ni zao la udadhirfu na Rushwa amabvyo ni baba wa CCM.

    ReplyDelete
  2. ASIYESIKIA LA MKUU HUVUNJIKA GUU. WE WAACHE TU SIKU ZAO ZISHAKWISHA, PUNDE SI PUNDE WATASHANGAA, NA WATAKUWA EXPIRED BY THEN!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...