UHAI CUP YAINGIA ROBO FAINALI
Michuano ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 kwa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom imeingia hatua ya robo fainali ambayo itachezwa kesho (Novemba 21 mwaka huu) kwenye viwanja vya Karume na Azam ulioko Chamazi.
 
Oljoro JKT na Simba zitapambana saa 3 kamili asubuhi kwenye Uwanja wa Karume wakati katika muda huo huo kwenye Uwanja wa Azam kutakuwa na mechi kati ya JKT Ruvu Stars na Toto African.
 
Mechi nyingine zitachezwa saa 10 kamili jioni ambapo Serengeti Boyz (timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17) itaumana na Villa Squad kwenye Uwanja wa Karume. Uwanja wa Azam utashuhudia mechi kati ya Moro United na Azam.
 
Nusu fainali ya michuano hiyo itachezwa Novemba 23 mwaka huu Uwanja wa Karume ambapo mechi ya kwanza itakuwa saa 3 kamili asubuhi wakati ya pili itaanza saa 9.30 alasiri. Fainali itachezwa Uwanja wa Karume, Novemba 25 saa 9 kamili alasiri ikitanguliwa na mechi ya kutafuta mshindi wa tatu itakayoanza saa 3 kamili asubuhi.
 
Bingwa wa michuano hiyo inayodhamini na kampuni ya S.S. Bakhresa kupitia maji Uhai atapata sh. milioni 1.5, mshindi wa pili sh. milioni moja wakati wa tatu atapata sh. 500,000. Mbali ya fedha hizo, bingwa atapata medali za dhahabu, makamu bingwa medali za fedha na mshindi wa tatu medali za shaba.
 
Mchezaji bora sh. 400,000, mfungaji bora (sh. 300,000), kipa bora (sh. 300,000) na timu yenye nidhamu sh. 300,000.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...