Naomba kutoa kuufahamisha umma juu ya kifo cha mtanzania mwenzetu, NASSIB JUMA MANYALA (pichani) alifayeriki akiwa nyumbani kwake, East Lansing, Michigan USA siku ya tarehe 22/10/2011. Marehemu ambaye alishafiwa na wazazi wote wawili ameacha watoto watatu, wawili wakiwa USA na mmoja Tanzania.
Wazazi wa marehemu ni wenyeji wa mkoa wa Tabora (baba) na Wilaya ya Muheza, Tanga (mama). Kwa bahati mbaya, familia ya marehemu imeshindwa kupata fedha za kusafirisha mwili kwa ajili ya mazishi nyumbani kwao, gharama ambazo zilikisiwa kufika/kukaribia $15,000. Kutokana na hali hii iliamuliwa marehemu azikwe huko Lansing, MI. Kwa kupitia Blog yako, tunaomba watanzania wote kwa ujumla, jamaa na marafiki wenye uwezo kusaidia kifedha katika kufanikisha mazishi ya merehemu Nassib pamoja na gharama zitakazojitokeza katika kuweka msiba na kukamilisha taratibiu zot ezinazotakiwa.
Michango ya fedha inaweza kupelekwa moja kwa moja kwenye akaunti maalumu iliyofunguliwa na marafiki pamoja na jumuiya ya watanzania waishio Lansing, MI kwa ajili ya kusaidia mazishi ya marehemu kule. Jina la mfuko huo ni:-
NASIBU JUMA MANYALA MEMORIAL ACCOUNT
MSU Federal Credit Union
Acc # 43380705
Routing #272479663
Familia pia imewateua Professor Deogratius Ngonyani wa Michigan State University pamoja na ndugu Mussa Maingu wa East Lansing, MI kusimamia suala zima la mazishi na taraytibu husika.Kwa watanzania ambao wangepend akushiriki katika hili wawasiliane nao moja kwa moja kupitia anuani zifuatazo ili kupata utaratibu mzima na mipango ya mazishi:-
1. Prof. Ngonyani:-- 2538 Glen Cove, Holt, MI 48842, USA Phone +1 517-694-7904.
2. Mussa Maingu:- +1 517 980 4444
Tunatanguliza shukrani wasukuru za dhati
Tunaomba kwa Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi, Amen
RIP, so young.
ReplyDeleteinnallialah wainnaillah rajiuun,
ReplyDeletemdau.
May his soul rest in peace.
ReplyDeleteLoh.Habari ya kusikitisha sana hii..Kama itapatikana hela kidogo huyu mtoto aliyeko Tanzania basi asafirishwe haraka kuhudhuria mazishi ya Baba yake.
ReplyDeleteR.I.P Nassib
David V
Msg kidogo haijatulia.....Marehemu atazikwa USA?...ameshazikwa?...au mwili utaletwa TZ?
ReplyDeleteKWAKE TUMETOKA NA KWAKE TUTAREJEA SIFA ZAKE ZITUKUKE "AMIN" SWALI LA UZUSHI MICHIGANI CHAMA CHA WABONGO IMEKUAJE TENA NANI MSIMAMIZI AMEISHA KULA PESA PALIKUA NA VISHINDO VYA CHAMA NA MADARAKA SASA KIJIJI JIRANI MSIBA UMETUFIKA HATUONI KUJITOKEZA INSHAALLAH KHERI
ReplyDeleteMussa na Deogratius wako pamoja kwenye kamati ya mazishi ya ndugu yao Nassib. Hao ndio watanzania, huo ndio utanzania.
ReplyDeleteRIP brother, but tunaomba hii msg iwe clear je mnataka michango ya kuusafirisha mwili au ya kuupumzisha huko huko? Please wahusika iweni specific
ReplyDeleteTUNATAKA MICHANGO YA KUMZIKA HAPA MAREKANI HATUNA HELA ZA KUMSAFIRISHA MAREHAMU NA HATUWEZI KUZIPATA HARAKA, KWAHIYO TUNAMZIKA JUMAPILI HII TAREHE 20/11/2011
ReplyDeleteEAST LANSING.
MPIGIE PROF. NGONYANI +1 517 614 3543 ATAKUELEWESHA VIZUZI.
poleni na msiba wafiwa
ReplyDeletemkisoma vizuri mtaelewa anasema nini ipo clear kuwa pesa ni za kumzika USA msisome kwakuuka maneno au rudia ukiwa umetulia kuelewa nini mtu anaandika
RIP
INNA LILLAH WA INA ILAYHI RAJIIIUUUN!
ReplyDeleteBwana ametoa na Bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe mwenyezi mungu aipumzishe roho yako mahali pema peponi kaka yetu Nassib tutakukumbuka daima. Amen.
ReplyDeleteRIP Nassib, I remember him as a classmate at Moro Sec. Cool and friendly to everyone. Trendy as well!
ReplyDelete