Mratibu wa Programu ya kuendeleza wajasiriamali wanawake na Usawa wa Kijinsia kutoka ILO, Gloria Kavishe akifafanua jambo kuhusu tamasha la wanawake wajasiriamali (MOWE) lililoandaliwa na Shirika la Kazi Duniani na kufanyika kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam leo.
Mjasiriamali kutoka Rufiji, Chiku Ngoengo akitoa maelezo ya jinsi ya kutengeneza mkaa kwa teknolijia rahisi ya kutumia mabaki ya muogo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Copy Girlz, inayojishughulisha na kilimo cha mbogamboga, Maua Mohamed akionyesha dawa ya kutibu magonjwa mbalimbali yakiwemo ya Presha, Vidonda vya tumbo, kisukari pamoja na kuongeza kinga za mwili kwa wagonjwa walioathirika na ugonjwa wa ukimwi,Wakati wa tamasha la nne la Wanawake Wajasiriamalia (MOWE) lililoandaliwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) linaloendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam na kuwashirikisha wanawake kutoka mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani.
Dawa hiyo imetengenezwa na wanachama wa kikundi hicho kwa kutumia mbegu za mti wa Mlonga, mwenyekiti wa taasisi hiyo nae alisema kuwa wako mbioni kuanzisha Sacos ili kujiongezea mitaji yao kutokana na taasisi yao kuwa na muda wa miezi mitatu tangu kuanzishwa kwake huko Bagamoyo.
"Tunaishukuru ILO kwa kutuwezesha kufika katika tamasha hili kwani tumeweza kukutana na taasisi za kifedha pamoja na zile za kiserikali na kuweza kupata mafunzo yatakayotuwezesha kuendeleza vikundi vyetu, pamoja na hayo pia tumeweza kubadilishana ujuzi na wanawake wenzetu".Picha na Francis Dande.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...