Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Bw. Dioniz Malinzi akifurahia baada ya kukata utepe kuzindua mbio za kumi za Kilimanjaro Marathon zitakazofanyika Februari mwakani. Wengine kwenye picha ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe (kushoto), George Rwehumbiza, Mkuu wa Udhamini wa Vodacom, Mkuu wa Masoko wa GAPCO, Ben Temu na Mkurugenzi wa Michezo, Leonard Thadeo. Hafla hii ilifanyika mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Southern Sun jijini Dar es salaam. (Picha: Hisani ya Executive Solutions)
 Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Bw. Dioniz Malinzi akikata utepe kuzindua mbio za kumi za Kilimanjaro Marathon 2012 zitakazofanyika Februari mwakani. Wengine kwenye picha ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe (kushoto), George Rwehumbiza, Mkuu wa Udhamini wa Vodacom, Mkuu wa Masoko wa GAPCO, Ben Temu na Mkurugenzi wa Michezo, Leonard Thadeo. Hafla hii ilifanyika mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Southern Sun jijini Dar es salaam.  (Picha: Hisani ya Executive Solutions)
 Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe akihutubia waalikwa katika uzinduzi wa mbio za kumi za Kilimanjaro Marathon zitakazofanyika tarehe 26 Februari 2012. Hafla hii ilifanyika mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Southern Sun jijini Dar es salaam. (Picha: Hisani ya Executive Solutions)

  1. Mkurugenzi wa Executive Solutions, waratibu wa mbio za Kilimanjaro Marathon akiwatambulisha washindi wa kwanza wa mbio za Kilimanjaro Marathon 2003 wakati wa hafla ya uzinduzi wa maandalizi ya mbio za kumi za Kilimanjaro Marathon zitakazofanyika Februari 26, 2012. Hafla hii ilifanyika mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Southern Sun jijini Dar es salaam. (Picha: Hisani ya Executive Solutions)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Executive Solutions, mnaweza vipi kuzumzia riadha bila kutambua uwepo wa katibu wa riadha?

    ReplyDelete
  2. katibu hana lolote badala kutafuta wadhamini kazi kulialia tu na serikali

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...