Uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mara (FAM) ulifanyika Novemba 13 mwaka huu wilayani Rorya.
 
Uchaguzi huo uliendeshwa na Kamati ya Uchaguzi ya FAM chini ya Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Viongozi waliochaguliwa kwa kuzingatia Katiba ya FAM na Kanuni za Uchagzui za wanachama wa TFF ni wafuatao;
 
Fabian Samo amefanikiwa kutetea wadhifa wake wa Mwenyekiti huku Deogratius Rwechungura akichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti. Wengine waliochaguliwa ni Mugisha Galibona (Katibu Mkuu), Samwel Silasi (Katibu Msaidizi), Evans Liganga (Mhazini), David Sungura (Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF), William Chibura (Mwakilishi wa Klabu) na Valerian Goroba (Mjumbe).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mbona mmefanya haraka hivyo?? Si mngesubiri kwanza Bw. Michael Richard WAMBURA amalize sula lake na TFF?

    ReplyDelete
  2. Mpira unatafsiriwa kwamba ni sehemu ya mizengwe na fitina ndio maana kwenda mahakamani hakuruhusiwi!!!

    ReplyDelete
  3. Hope there's something kwa ninni hawakutaka kungoja rufani ya mrufani wambura ikamilike je tukisema tff mnamkimbia wambura mtakataa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...