Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Akiba kwa Wafanyakazi Serikali (GEPF), Daudi Msangi akipokea cheti cha ushindi kutoka kwa Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudensia Kabaka wakati wa uzinduzi wa wiki ya Hifadhi ya jamii katika viwanja vya Mnazi mmoja,jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akisoma hotuba wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Hifadhi ya Jamii,katika viwanja vya Mnazi mmoja,jijini Dar es Salaam leo.
 Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akizindua rasmi Wiki ya Wizara kujitangaza na Uzinduzi wa Wiki ya Hifadhi ya Jamii jijini Dar es Salaam leo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Akiba kwa Wafanyakazi Serikali (GEPF), Daudi Msangi akimkaribisha Waziri wa Kazi na Ajira Gaudensia Kabaka alipokuwa akiwasiki kwenye Banda la Mfuko wa Akiba kwa Wafanyakazi Serikali kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam leo.
 Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akisaini kitabu cha Wageni alipotembelea banda la mfuko wa Akiba kwa Wafanyakazi Serikalini.
 Mrisho Mpoto 'Mjomba' akitumbuiza katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Wizara kujitangaza na Uzinduzi wa Wiki ya Hifadhi ya Jamii.
 Meneja Masoko wa Mfuko wa Akiba kwa Wafanyakazi Serikalini (GEPF), Aloyce Ntukamazina akitoa maelezo ya jinsi ya kujiunga na mfuko huo kwa wadau waliotembelea banda lao.
Wanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam wakiangalia mchoro wa daraja la Kigamboni.Picha na Francis Dande wa Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Wekeni njia za kutosha za watembea kwa miguu na waendesha baiskeli (miguu miwili, mitatu, na bajaj). Itakuwa vema kama mtaomba maoni ya watumiaji barabara.

    ReplyDelete
  2. Naungana na mtoa maoni wa kwanza. Pia wekeni parking spaces za dharura, sio gari ikiharibika basi ndio inaziba njia hadi kesho.

    ReplyDelete
  3. Huu mradi bado upo kiganjani tu hadi leo????

    ReplyDelete
  4. wawekeeni sehemu na watu wanaotaka kujiuwa kwa kujitosa

    ReplyDelete
  5. Twende mbele turudi nyuma,hilo vazi alilovaa mjomba mpoto linaonekana ni vazi la kike.
    *michuzi weka hii

    ReplyDelete
  6. ILA MPANGO WA DARAJA LA KIGAMBONI UWE WA UKWELI ....USIWE WA ''MANYAU NYAU''...kama ile DART (Dar Rapid Taransport) ...yaani mabasi yaendayo KASI!.

    ReplyDelete
  7. MPENI TENDA MCHINA. MWISHO WA YOTE. WENGINE MTAKULA HASARA KAMA RELI YA KATI. (TRC)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...