Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Ezekiel Maige (aliyeshika bunduki), akipewa maelezo juu ya aina za bunduki zinazoruhusiwa kutumika katika shughuli za uwindaji wanyamapori na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Uhifadhi wa Wanyamapori Mweka, Prof. Feetham F. Banyikwa, Mweka, Kilimanjaro mwishoni mwa wiki iliyopita. Mhe. Maige alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya 46 ya chuo hicho.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Ezekiel Maige (watatu kulia) akielekezwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Uhifadhi wa Wanyamapori Mweka, Prof. Feetham F. Banyikwa jinsi ya kulenga shabaha na moja ya bunduki zinazotumika na askari wanyamapori kukabiliana na wanyama waharibifu na doria, Mweka, Kilimanjaro mwishoni mwa wiki iliyopita. Mhe. Maige alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya 46 ya chuo hicho.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Ezekiel Maige (kulia) akipanda mti katika viwanya vya Chuo cha Uhifadhi Wanyamapori Mweka, Kilimanjaro mwishoni mwa wiki iliyopita na kushoto ni mwanafunzi wa chuo hicho Grace Lyimo. Mhe. Maige alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya 46 ya chuo hicho.
Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Ibrahim Mussa (kulia) akimsisitizia jambo mwekezaji wa sekta ya utalii, Robert (kushoto) katika Ziwa Chale, Rombo, Kilimanjaro alipofanya ziara wilayani humo kuangalia maeneo yatakayotengwa kwa ajili ya uwekezaji wa Hoteli za Kitalii huku Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Ezekiel Maige (katikati) akisikiliza kwa makini, Rombo, Kilimanjaro mwishoni mwa wiki iliyopita.Picha na Tulizo Kilaga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...