Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya simu ya mikononi ya Airtel, Bw. Sam Elangallor akipokea tuzo na cheti cha heshima kwa kushika nafasi ya mlipa kodi kwa ridhaa kati ya taasisi 10 zilizochaguliwa. Tuzo hiyo imetolewa leo kwenye hotel ya Serena jijini Dar wakati wa hafla fupi ya maadhimisho ya miaka 5 ya siku ya mlipa kodi kwa taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hivi hawa wanalipa kodi vizuri kushinda mie mfanyakazi (wa kuajiriwa na serikali) ambaye nakatwa PAYE kila mwezi bila mgogoro wala kuchelewesha!!!! ifikie hawa TRA watambue mchango wetu na kututunuku na sisi hayo makombe na kutufutia baadhi ya kodi ikiwezekana, say nataka kununua kiwanja basi wawe wanatupa incentive ya kutokulipia kodi wakati wa manunuzi. Maana Mfanyakazi huyo huyo alipia kila bidhaa anayonunua VAT. Ni maoni yangu tu.

    ReplyDelete
  2. Wewe kuwa mpole, maana hautoi kodi kwa hiari. Utake usitake ni lazima ukatwe tuu. Sasa zawadi wanapewa wanaolipa kwa hiari, ambao kama wakiamua kutumia ujanja ujanja wanaweza kukwepa hiyo kodi

    ReplyDelete
  3. teh teh teh teh anon wa wed dec 07,01;00;00 am 2011 jibu zuri sana la ukweee

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...