Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Rukwa Mhe. Hiporatus Matete akionyesha kadi ya CHADEMA aliyokabidhiwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho katika Manispaa ya Sumbawanga Ndugu Geophrey Shayo (kulia) katika ukumbi wa Sabasaba uliopo katika Manispaa ya Sumbawanga. Anayeshuhudia katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ambaye pia ni Mbunge Viti Maalum CCM wa Mkoa wa Songea ambaye ni Mhe. Eng. Stella Martin Manyanya. Mwenyekiti huyo amechukua hatua hiyo kwa madai kuwa amechoshwa na udanganyifu ambao upo ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Mbunge wa jimbo la Sumbawanga Mjini Mhe. Aeshi Hillal (kulia) akimpa mkono wa pongezi Ndugu Shayo mara baada ya hatua yake aliyoichukua ya kukabidhi kadi ya CHADEMA kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa na hatimaye kujiunga na Chama hicho. Ndugu Shayo amempongeza Mhe. Aeshi kwa kazi nzuri aliyokwisha kuifanya katika jimbo lake la Sumbawanga Mjini na kusema kuwa hatua yake hiyo ya kuihama CHADEMA ni kuja kumpa nguvu ili maendeleo yaweze kuja kwa kasi zaidi katika jimbo hilo. Kushoto ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Mhe. Sabas Katepa.
wamekununua sh ngapi.....?
ReplyDeleteChukueni na Hamad Rashid
ReplyDeletekwenye msafara wa mamba na kenge wapo
ReplyDeletewamekuahaidi ubalozi Rwanda nini? kama ni kuhama basi uamuzi wako ni mzuri lakini wakati wake ni mbaya.kama unatafuta cheo CCM haujachelewa kwani kikwete kupanga leo kupangua kesho ni jambo la kawaida.Nchi yetu hakuna kiongozi anayejali kutawanya mali hii ni desturi yetu benki ya dunia ipo,IMF ipo,wafadhili wapo watatusaidia kuganga nja zetu.kama wapo watetezi wa wananchi basi mola awajalie kwa umakini wao wa kuthamini Utu kabla ya mali.
ReplyDeleteCCM PAMBALAMA X2!
ReplyDeletePOTELELI CCM EEE ,POTELELI CCM PAMBALAMA!
CCM PAMBALAMA X2!
POTELELI CCM EEE, POTELELI CCM
PAMBALAMA!
Kifipa hicho Jamaa amefanya uamuzi wa busara na AMEPIGA BAO! kwa kuzitambua alama za nyakati baada ya kuona dira ya CHADEMA inaenda mrama!
Sina tatizo na watu kuhama chama fulani na kuhamia chama kingine, kwasababu ni haki yao na ndio demokrasia yenyewe, lakini nina tatizo na utamaduni uliojengeka wa kuichukua kadi ya chama unachokihama na kuikabidhi katika chama unachohamia. Kadi ni mali ya chama, na kama umeamua kuhama chama, basi kabidhi kadi kwa chama unachotaka kuhama na sio unachohamia. Yaani uende katika chama chako uwaambie kwamba mie nahama na kadi yenu hii hapa nawaachia! Nadhani sio ustaarabu, ni ushabiki wa kijinga kwa anayetoa chama, na hata wanaopokea kadi ya chama ambayo sio yao. Ni ushabiki unaoweka kuchochea hasira na kujenga chuki zisizo za lazima
ReplyDeleteMm sina lawama lkn ukimuangalia huyu jaamaa ktk sura ana aibu ya usaliti. Hii inamaanisha hataka kufanya hili jambo. Mpaka suti yake km ya CHADEMA. Je CCM mtwamwamini vp msaliti au chezo tu?
ReplyDeleteMdau wa 6 hapo juu , kwa mazingira ya Siasa za visasi na jazba zisizo za kistaarabu kama za CHADEMA inakuwa ni vigumu kwenda ktk Ofisi ya Chama kama hicho, na ukawapa kadi yao ukisema unahama inawezekana kabisa huwezi kutoka hapo ukiwa hai!
ReplyDeleteKwa siasa za UHALIFU za chama kama CHADEMA za mapanga mkononi sha!, sha!, huwezi rudisha kadi unapohamia CCM kwa mazingira unayosema Mdau wa sita 6 hapo juu!
ReplyDeleteLabda uitume kadi kwa njia ya Posta kuirudisha CHADEMA!
Geophrey Shayo ,uamuzi wake kuondoka CDM na kuingia CCM ametumia akili sana!
ReplyDelete1.Ameangalia Tanzania ina makabila 126 lakini akaona CDM inatawaliwa na kabila moja tu!
2.Akatazama mfano, kila kabila likiwa na mwakilishi 1 ina maana CDM itakosa kura 125 kati ya 126!
3.Akaangalia kuwa kwa sera za CDM na dalili zao za siri za ndani sio rahisi kuwashawishi makabila mengine yote 125 yaliyobaki yaichague CDM!
Hivyo kwa FIKRA na TATHIMINI ya NAMBA 2 hapo juu ni kuwa, CHADEMA ITASHINDWA NA HAIWEZI KUPATA MAMLAKA NA NDIO MAANA KWA BUSARA NA AKILI ZA HALI YA JUU AKAAMUA KUHAMIA CCM!
Ohooo , aende kwenye ofisi ya Chadema kurudisha kadi?
ReplyDeleteAhh hii ni hatari sana atakufa buree Shayo jamaa kwa uamuzi wa kuhama chama kwenda CCM watamkata kawoshi kuanzia masikio, mikono na miguu kwa mapanga!
Unajua Mdau Chadema wana mwenendo wa uhalifu labda kwenda kurudisha kadi ofisi ya chadema asindikizwe na Polisi!
Mdau mtoa Maoni wa saba 7 kutoka juu, Geophrey Shayo anaonyesha uso wa huzuni sio kwa Usaliti bali ni kwa masikitiko kuwa alifuata itikadi mbaya ya CDM na amehamia CCM na kuwa anajutia alipoteza muda bure kule!
ReplyDelete........... kumbe kuhama chama ni birthday !?
ReplyDeleteBwana sHAYO AME-HIT HEADLINES ! tehee......tehee tihiii !
SHAYO amepiga bao!
ReplyDeleteAmeonyesha kuwa yeye ni Mchagga mjanja, hataki kuchemsha mawe, ameona muda umepotea bure na biashara yake imeyumbishwa na misimamo batili ya itikadi za Chadema!.
Ameona aingie CCM ili biashara yake iimarike upya baada ya kufilisiwa na Chadema kutokea uchaguzi mwaka jana.
Ametambua mbio za Chadema ni za mwendawazimu za kufukuza kuvuli!
Hahahah Geophrey Shayo baada ya kuhamia CCM kwa njia rahisi rahisi hawezi rudisha kadi Chadema akijua kuwa kwa vile yeye ni Mchagga na ktk kabila lao itikadi ya Chadema ni kama dini ni lazima watamfanyia ubaya!
ReplyDeleteGeophrey Shayo,,,uammuzi wake wa kuhama Chadema kwenda CCM kwa itikadi mbaya ya Chadema badala ya kuchukuliwa kama matashi yake binafsi ya kisiasa atachukuliwa kama vile ameasi kabila la Uchagga!
ReplyDeleteKanunuliwa but haisaidii, Chadema bado ndio mkombozi wa watanzania wengi.
ReplyDelete