Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) Sabasaba Moshingi (kushoto) na MKurugenzi wa huduma za Kibenki wa CITI bank Bw.Gasper Njuu wakisaini mikataba itakayowawezesha wateja wa Citi bank kupata huduma za kibenki kupitia kwenye matawi ya Benki ya Posta .Mkataba huu ulisainiwa makao makuu ya Benki ya Posta Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) Sabasaba Moshingi (kushoto) akipeana mikono na MKurugenzi wa huduma za Kibenki wa CITI bank Bw.Gasper Njuu mara baada ya kutiliana saini mkataba ambao utaiwezesha Citi bank kutumia mtamdao wa matawi ya Benki ya Posta katika kutoa huduma zake za kibenki.Mkataba huu ulisainiwa makao makuu ya Benki ya Posta Tanzania.
Na Mwandishi wetu
Benki ya Posta Tanzania na ile ya Citi Bank zimetia saini makubaliano ambayo yatawafanya wateja wa Citibank kuweza kutumia matawi ya Benki ya Posta Tanzania kama wanavyotumia ya benki yao.
Makubaliano hayo yamesainiwa jijini Dar Es Salaam kati ya Afisa mtendaji mkuu wa Benki ya Posta Tanzania Bw.Sabasaba Moshingi na MKurugenzi wa huduma za Kibenki wa CITI bank Bw.Gasper Njuu.
Akizungumza baada ya kutia saini makubaliano hayo Bw.Moshingi amewahakikishia wateja wa Citibank kuwa wataweza kupata huduma kwa karibu zaidi kupitia matawiya Benki ya Posta yaliyopo nchi nzima.
Naye Mkurugenzi wa huduma za Kibenki wa Citibank Bw.Gasper Njuu amesema hatua ya benki yao kuamua kutumia huduma za Benki ya Posta Tanzania zinatokana na wao kuridhishwa na ufanisi wa benki hiyo.Aliahidi kwamba huu ni mwanzo tu kwani uhusiano huu utaendelezwa na kuhusisha nyanja nyingine, nia ikiwa ni kutoa huduma bora na za uhakika kwa wateja wa benki hizo mbili.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...