Wazee wa kitambi noma hufanya bonanza kila siku ya jumapili katika viwanja vya shule ya msingi Slaa manispaa ya Arusha. Lengo la bonanza hilo ni kupunguza vitambi kwa vijana pamoja na wazee wenye vitambi mjini hapa.Bonanza hilo limedhaminiwa na Bar maarufu mjini hapa yaani QX Pub. Katika bonanza hilo michezo mbali mbali hufanyika ikiwa ni pamoja na mpira wa miguu, riadha, kuvuta kamba na kufukuza kuku.Mashindano ya kupiga danadana yakiendelea ndani ya viwanja vya shule ya msingi slaa.
Kikosi kazi cha wazee wa kitambi noma wakiwa kwenye pozi la pamoja mara baada tu ya mazoezi kukamilika katika viwanja vya shule ya msingi Slaa manispaa ya Arusha.
Kikosi kazi cha wazee wa kitambi noma wakiwa kwenye pozi la pamoja mara baada tu ya mazoezi kukamilika katika viwanja vya shule ya msingi Slaa manispaa ya Arusha.
Baada ya mazoezi wazee wa kitambi noma hukusanyika QX Pub ili kupata supu kabla ya kuendelea na shughuli binafsi za weekend kama wanavyoonekana pichani kwenye picha.
dUUH YAANI BAADA YA MAZOEZI HALAFU MWAPIGA SUPU EEEH,NA COCA BARIIIIDIIII,WALLAH KITAMBI NOMA HAKITOKWISHA KWA DIZAINI HIO.
ReplyDeletekwa picha hii ya mwisho wazee wa kitambi noma watendelea kuwa wazee wa vitambi.
ReplyDeleteKumbe inabidi ukitoka mazoezini shurti usile?....wacha na hicho kitambi kishamiri nyie wazee kuleni kwa kwenda mbele kuliko kuacha mazoezi.....
ReplyDeleteNyie wazee bigup kwa saana Hayo ndio mambo. Nami ninge kuwa huko yaani chama Hilo must. Fanyeni promo muongeze washiriki. Bigup guys. Supu kwa mbele mwili haujengwi kwa tofali banaa....
ReplyDelete