HABARI ILIYOTUFIKIA HIVI PUNDE INAELEZA KUWA,ALIYEKUWA MTANGAZAJI WA ITV/RADIO ONE MIAKA YA NYUMA NA BAADAE KUHAMIA KWENYE SHIRIKA LA UTANGAZAJI LA UINGEREZA (BBC),BW. JOHN NGAYOMA AMEFARIKI DUNIA MAPEMA LEO ASUBUHI.
HAYATI NGAHYOMA AMBAYE AMEFIKWA NA MAUTI LEO AKIWA HOSPITALI AMBAKO ALIKUWA AKIPATIWA MATIBABU YA MARADHI YALIYOKUWA YAKIMSUMBUA KWA MUDA MREFU AMBAPO ALIENDA MPAKA NCHINI INDIA KWA MATIBABU YA MARADHI YAKE HAYO BILA MAFANIKIO.
MSIBA UPO NYUMBANI KWA MAREHEMU MAENEO YA TABATA SEGEREA NA TARATIBU ZOTE BADO ZINAENDELEA KUFANYIKA.
HIVYO TUTAENDELEA KUPEANA TAARIFA KADRI TUTAKAVYOKUWA TUNAZIPATA.
GLOBU YA JAMII IMEPOKEA KWA MASIKITIKO MAKUBWA SANA TAARIFA HIZI ZA MSIBA WA MPIGANAJI WA SIKU NYINGI KATIKA TASNIA HII YA HABARI,BW. JOHN NGAHYOMA NA INATOA POLE KWA NDUGU WOTE WA MAREHEMU NA TUKO PAMOJA KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU CHA MAJONJI.
TUNAMUOMBEA KWA MUNGU AIWEKE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI.
AMEIN.
Mjomba kwake ni Tabata Segerea, na sio Mbagala.Ukifika Segerea mwisho unaenda mbele kidogo unaacha mitaa nne kulia kwako wa tano ndio mtaa wake,au ukitokea kinyelezi baada ya njia ya kwenda gerezani mtaa unaofuata kushoto. Au tuseme ni njia amabayo inatumiwa na wakazi wanaoenda kisukulu baada ya njia ya gereza kupigwa marufuku.
ReplyDeleteJamanii... RIP John Ngahyoma, alikuwa bosi mzuri sana alipokuwa newsroom ya ITV... Poleni sana wafiwa pamoja na wapiganaji wote
ReplyDeletePumzika kwa amani John, pole kwa familia wanahabari woote na aliowahi kufanya nao kazi. Nimesikitishwa sana ila tukumbuke kuwa kila nafc itaonja mauti, haikwepeki.
ReplyDeleteEe Mungu tunusuru tufike hiyo Jumapili
ReplyDeletesisi wote niwafiwa ingawa familia inahusika zaidi Mungu ailaze pema roho ya marehemu
ReplyDeleteRIP John,ulikuwa mcheshi pale tulipokuwa tunafanya kazi ITV,nakumbuka sauti yako ilivyokuwa ukisoma jiji letu na habari za biashara saa za news.mungu aieke roho ya marehemu mahali pema peponi amen.
ReplyDeleteJamani mbona mwaka unamalizika vibaya John kweli umekwenda?? so sad
ReplyDeleteR.I.P John ngayoma mchangia mada hapo unayeomba tufike j'pili be serious hapa si mahali pa matani muda wote grow up
ReplyDeletePOLENI WAFIWA..TULIMPENDA LKN MUNGU AMEMPENDA ZAIDI. TULIE KWA IMANI.
ReplyDeletePole Winnie kwa kufiwa na baba yako.
ReplyDeleteNi huzuni sana. John tunakukumbuka sana na tutaku-miss. Mungu akupumzishe kwa amani, na pia aifariji familia yako na kuwalinda daima.
ReplyDeleteIts soo sad, really sad, umetutoka.
Mchango wako mkubwa katika sekta ya habari kamwe hautasahaulika!!!
RIP my brother! So sad!
ReplyDeleteJazba mbaya jamani kumwomba Mungu atufikishe mwaka 2012 kuna utani gani lakini? R.I.P John. ingekuwa ni uchafuzi wa hali ya hewa ankal asingeweka ai kuelewa mambo kazi!!
ReplyDeleteR.I.P John Ngahyoma. Mwenyenzi Mungu amekupenda zaidi.
ReplyDeleteEe MWENYEZI MUNGU WAPOKEE VIUMBE WAKO HALIMA NA NGAHYOMA.
ReplyDeleteR.I.P uncle John, Cc tulikupenda lakini mungu amekupenda zaidi, Pole sana Faith ni kazi ya mungu, Pole sana DrUpendo na Dr Edmond mungu awatie nguvu na awape moyo wa uvumilivu, tunaelewa kuwa inauma sana lakini tunaamini kungu atawapa roho ya ujasiri na uvumilivu, manzishi ni lini na wapi?
ReplyDeleter.i.p Poleni sana wafiwa, poleni sana familia ya akina Ngahyoma
ReplyDelete