Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akikabidhi msaada wa vyakula kwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik , katika ofisi ya mkuu huo jana. Vyakula hivyo vyenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 4, vimetolewa na CCM kwa ajili ya kusaidia waliokumbwa na maafa ya kafuriko yaliyosababishwa na vyua katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.
Nape akimchumu mtoto Fatuma Fadhili aliyekuwa na mama yake Ofisi za mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, leo.
Nape akizungumza na baadhi ya wananchi alipofika kwenye kambi maalum ya Mchikichini walikohifadhiwa waathiorika mwa mafuriko, wilayani Ilala.
"Tunashukuru serikali imetuhudumia vizuri sisi waathirilka.. wanaolalamika ni wale wanaojichomeka ili wapate msaada wakati si wahusika.." akisema mmoja wa wazee (kulia) ambao Nape alizungumza nao kujua serikali ilivyosaidia waathirika wa mafuriko, alipotembelea kambi la Mchikichini walikohifadhiwa kwa muda waathirika hao,leo.
Nape akipata taarifa za matibabu wanayopatiwa waathirika wa mafuriko, katika kituo cha muda cha wathirika hao, shule ya msingi Mchikichini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. KWENU Vyama vya Siasa, CHADEMA, CUF, na CCM:

    Kampeni za uchaguzi jimbo moja tena uchaguzi mdogo matumizi MABILIONI lakini Maafa ya Mafuriko matumizi VI MILIONI kiduuuchu!

    ReplyDelete
  2. Hivi ninyi vyama vyote vya Siasa mngetoa 10% ya gharama za uchaguzi mlizotumia Igunga, si ingewezekana hata waathirika wa mafuriko wakajengewa nyumba Mbagala?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...