Wengi tumemsikia ama kumuona ndege Tausi lakini sio kwa karibu namna hii. Mtazame ndege huyu mwenye urembo na madaha upate kumjua zaidi japo kidogo. ajabu ni kwamba huyu ni dume...Inasemekana urembo wake na mabobish ni wa kuvutia majike waingie kwenye 18 zake....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Wanyama wengi wazuri ni Madume Tizama Tausi huyo Tizama Njiwa Tizama Simba dume ndio wanaovutia.

    ReplyDelete
  2. Anavyoringa hadi anafurahisha moyoni!

    Hongera kwa aliyepata nafasi hii.

    ReplyDelete
  3. Nadhani pia huchanua kwa ajili ya kujilinda na adui.

    ReplyDelete
  4. Dume la Tausi hilo kweli limejua kusasambua na kuuza sura kwa tija!

    ReplyDelete
  5. Mdau wa Kwanza hapo juu, naungana na wewe kabisa!, zaidi ya Uzuri wa Madume Wanyama pia tukienda ndani zaidi hata kwa Binaadam Mzuri ni Mwanaume!, hapa najua watu watabisha.

    Hebu twende kwa hoja,
    Jaribu kuangalia wawili wawepo ktk maisha Mwanamke na Mwanaume baada ya muda Mwanaume anazidi kuonekana kijana wakati Mwanamke anaonekana mzee kwa kasi zaidi!

    Kwa kawaida Wanaume ni Wazuri kwa vile hawazeeki haraka kama wanawake, angalia mfano wewe ni mwanaume wanawake uliosoma nao baada ya miaka 10 manaume atabaki kijana mzuri wakati wanawake wataonekana wazee na wabaya!, baada ya miaka 20 mwanaume ataonekana bado bado wakati wanawake duhh Vikongwe!!!

    Zaidi zaidi Mwanaume ni Mzuri hata akiwa babu wa Miaka 65 na kuendelea ili mradi ana fedha ni kimbilio la mademu anakuwa handsome tu!

    ReplyDelete
  6. Nyie mnaosema wanaume ni wazuri hamjawahi kuona wanawake wazuri. Mwanamke mwili wake jamani acheni.

    ReplyDelete
  7. Tausi ana njaa huyu hamna lolote.

    ReplyDelete
  8. Hv ni kwann tausi wamekuwa ni nadra sn kuonekana kwenye maeneo ya kawaida (hasa uswazi) tatizo ni nn au bajeti yake ni ndefu? na hv wanapatikana wapi kwa tz na kwa pesa ngapi ?

    ReplyDelete
  9. Mdau wa Sita unayempinga Mdau wa tano 5 kwa hoja ya uzuri wa Mwanaume dhidi ya Mwanamke kwa misingi ya umri na kuzeeka!

    Kwa kweli Mwanaume hata akiwa na zaidi ya umri wa miaka 75 bado anahesabika kuwa Handsome man endapo atajisikia kuwa hivyo,,, acheni ubishi!

    Nataka twende kwa Experiment na kwa mifano hai hapa chini kwa kuwa mimi mara nyingi ni Mtu wa experinemt naamini zaidi Sayansi kuliko ulinganishi usio na hoja!

    ___________________________________
    EXPERIMENT
    ___________________________________
    Kwa asili Mwanamke akisha kuwa na wajukuu anakuwa tayari ameanguka kisaikolojia na hajiamini kuwa miongoni mwa wazuri na vijana! labda awe mwanamke jasiri kama Bibi Kidude wa Muhogo wa Jangómbe!,wakati Mwanaume inakuwa ndio kwanza badooo!
    ___________________________________
    CLASSIC EXAMPLES
    ___________________________________
    -Waziri Mkuu wa Italia aliyepita SILVIO BERLUSCONI,
    -Raisi wa sasa Afrika Kusini,JACOB ZUMA,
    -Raisi wa Benki ya Dunia aliyepita
    PAUL WOLFOWITZ,
    -Kiongozi aliyepita wa Libya ,ambaye ni Marehemu,
    -Mkurugenzi wa IMF aliyepita DOMINIQUE STRAUSS KAHN,

    Hao wote ni mifano ya Mababu waliojisikia bado ni Vijana Wazuri!
    ___________________________________
    RESULTS:
    ___________________________________
    Haya sasa Wadau milinganishe baina ya EXPERIMENT NA CLASSIC EXAMPLES ili kupata results na msimamo mbivu na mbichi juu ya Uzee na Uzuri kati wa Mwanamke na Mwanaume, sio mimi tena hapo!!!!!!

    ReplyDelete
  10. Mdau wa sita Wanawake uzuri wao ni wa muda mfupi ni vile wanazeeka haraka kuliko wanaume!

    ReplyDelete
  11. Jogoo vipi jamani?

    ReplyDelete
  12. we anonymous unasifia wanaume hapo juu unajua wanawake wanapata kasheshe gani katika kuongeza watu duniani or you are just saying? umeniboa. Kwa taarifa yako ni hela tu wanawake wasomi na wenye hela wanaoishi mjini wana mvuto wa nguvu compaired na wanaume walioachwa vijijini au wenye hali mbaya kifedha. kwa hiyo maisha ni hela tu, kila mtu ni mzuri kwa kadiri Muungu alivyomuumba

    ReplyDelete
  13. Wewe unayesema wanaume wazuri kuliko wanawake sababu, eti wanawake wanazeeka haraka. Je umesahau kuwa miili ya wanawake inabeba mimba, inanyonyesha na kulea watoto? Ukosefu wa usingizi peke yake unanyangisha kuzeeka.

    Hata hivyo uzee si ubaya hapa kilichoongelewa ni uzuri siyo jinsia gani anazeeka kuliko nyingine.

    ReplyDelete
  14. Mdau uliyenijibu Ni Kweli na ushahidi tizama Mwanaume Hajipambi sana, wanawake wataanza kujipamba mara nyusi mara vipodozi mambo kibao japo kuna vijana wa siku hizi nao wanaiga mambo ya wanawake kuonesha dunia ilivyoharibika ila Mwanaume hana usumbufu wa majipambo sababu tayari mzuri.

    ReplyDelete
  15. Mwanamme anavutiwa na mwili wa mwanamke na mwanamke anavutiwa na mwili wa mwanamme, sasa haya mashindano ya nani mzuri kati ya mwanamke na mwanamme inategemea tuu wewe ni jinsia gani. Na kama wewe ni mwanamme unaangalia wanaume wengine na kuanza kutamani maumbile yao basi ukae ukijua kwamba kuna mushkel sehemu fulani za mwili au akili yako.

    Kuhusu huyo Tausi hapo juu, hivyo ndivyo tausi dume anavyofanya katika harakati za kumvutia tausi jike. hapo karibu lazima kulikuwa na tausi jike lakini mchukuaji picha hakuwa na muda na Tausi jike.

    ReplyDelete
  16. Mwanamke ataacha kuzeeka mapema? mtoto anamnyonya, baba anamnyonya. Pia wanaume wengine magomvi kila kukicha yaani wanaume msitamani maana hamtaweza

    ReplyDelete
  17. Mwanaume mmoja alikuwa anafanya kazi jumatatu-jumamosi. Mke wake alikuwa mama wa nyumbani. Cku moja yule mwanaume akaanza kumgombeza mkewe "mimi kila siku naenda kazini wewe umenyoosha miguu, kula na kwenda chooni" "akamalizia kwa kusema Ee Mungu naomba namimi nipumzike sasa niwe mwanamke na mke wangu awe mwanaume. Akalala kwa kuwa alikuwa amechoka. Usiku huu Mungu akambadilisha akawa mwanake akawa anapika,kufua, kulisha mifugo,kupeleka watoto shule n kuwachukua. Baada ya cku 2 akaomba Mungu arudie hali yake ya kuwa Mwanaume kwani hata hiyo nafasi ya kunyoosha miguu alikuwa hana kwani watoto wakirudi shule hata kuwapikia ilikuwa bado, Mungu akamwambia "SAMAHANI MWANANGU JANA ULIPATA UJAUZITO HIVYO OMBI LAKO LAKURUDI KUWA MWANAUME HADI BAADA YA MIEZI 9. Akalia kili kikuu. Wataalamu wa mambo wanasema mwanaume mwenyewe alikuwa Mtanzania kwani hata kuwasha jiko hawajui huwezi kumlinganisha na mzungu ambaye yote wanafanya kwa pamoja, chekeni x mas inakuja

    ReplyDelete
  18. Kuna tofauti kubwa kati ya uzee na uzuri. Au ni vitu viwili tafauti kabisa, uzuri na uzee. Au itakuwa sio kumtendea haki mmoja wa watu hawa- kumlinganisha mama wa miaka 70 na msichana wa miaka 22. Kama unataka kutenda haki chukuwa picha ya mama wa miaka 70 wakati alipokuwa na miaka 22 na uilinganishe na msichana wa miaka 22. Au subili huyo msichana wa miaka 22 atakapofikisha miaka 70 chukuwa picha yake na uilinganishe na ya mama mwenye miaka 70. Hata hivyo ulinganishi huo unaweza kuleta uatata kwa kuwa wahenga walisema HUJAFA HUJAUMBIKA!Ninakubaliana na mdau aliyesema kuwa kila binadamu ni mzuri kulingana an jinsi Mwenyezi Mungu alivyomuumba.
    Mdau
    W. Mwisho

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...