Ankali habari ya kazi,naomba niwakumbushe wadau wa Blog yetu jinsi Tanzania ilivyofikisha miaka hamsini ya Uhuru huku ikiwa na kumbukumbu adimu ambazo watu hawazijui, picha hii ilipigwa Siku ya Ijumaa Tarehe 19 October 2001 na hili ni Daraja la Mto Malagarasi kule Kigoma,nasikia Daraja hili lilijengwa long time lakini bado liko Imara kama limejengwa juzi tu,Ukitoka Kibondo lazima uvuke hapa kabla hujafika Kasulu.
Home
Unlabelled
Daraja la Mto Malagarasi - Kigoma
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



Reminds me of Bulumbora JKT :)
ReplyDeleteSidhani kama magari yanaweza kupishana hapo. Inabidi yasubiriane. Sasa sijui nani anayeamua gari lipi lianze kupita kabla ya lingine
ReplyDeleteAnonymous wa Wed Dec 28, 12:44:00 AM, nadhani sheria zetu za nchi huwa zinazuia magari kuoishana kwenye daraja (sijui kwanini lakini fuatilia) pia unapokaribia madaraja ya mito mikubwa huwa kuna sign za kuonyesha kwamba mbele kuna daraja pia kuna vituta vidogovidogo. Hivyo basi mara nyingi yule anaekaribia ndio huwa anaruhusiwa pamoja na msafara wa magari yaliyo nyuma mpaka yaishe ndio na mwingine anafuatia pamoja na magari mengine.
ReplyDeleteAah ah, usishangae: TULITHUBUTU, TULIWEZA, TUNASHINDWA NA TUNAENDELEA KUSONGA MBELE"
ReplyDeleteYa siku hizi hayadumu kwa ajili ya slogani hiyo hapo juu. Kuchakachua kwingi.
Juzi juzi Mh. Magufuni alikuwa anatoa tahadhari kwani anajua.....
Asante kwa picha mdau.
ahsante kwa picha ya kwetu!!!! Hilo daraja means a lot kwangu!!!
ReplyDeleteHivi unadhani common sense ndiyo itamuongoza dereva mmoja amsubirie mwenzake?
ReplyDeleteSiku moja tulikuwa darajani pale Ruvu (lile daraja la zamani). Mwenye basi letu alianza kuingia kwenye daraja na alishavuka karibu robo tatu ya daraja. Tulitegemea dereva aliyekuwepo upande wa pili asubiri kwa muda mfupi tu ili tumalizie na yeye aendelee. Cha mshangao aliingia na kutuzibia njia kabisa na akakataa kurudi. Tulikaa hapo mpaka tukamsihi yule dereva wetu awe muungwana arudi nyuma ampishe.
Bahati nzuri yule dereva wetu alisikia na kurudi nyuma pole pole, tukampisha yule mbishi avuke.
Kwa hivyo siyo wote wenye akili hizo unazofikiria wewe.