HELLO MZEE WA LIBENEKE, NAFAHAMU KAMA KAWAIDA YAKO WE SI MTU WA KUWEKA HABARI YA MTU KAPUNI MANA UNA MSEMO WAKO UNAOSEMA KUWA ATAEKUZIKA HUMJUI;

MI DUKUDUKU LANGU NA USHAURI KWA SERIKALI YA WATANZANIA WAISHIO UK WAWE WAWAZI KATIKA SHUGHULI HIZI HASA ZINAZOHUSU SHEREHE ZA KITAIFA MFANO HIVI KARIBUNI KUPITIA BLOG YAKO WAMETANGAZA KWA JUHUDI ZOTE KUWA KUTAKUWA NA SHEREHE ZA KUADHIMISHA MIAKA 50 YA UHURU WETU KATIKA UKUMBI WA LA ROYAL BANQUETTING SUITE (819-821 HIGH STREET N17 8ER TOTTENHAM, LONDON).

 LAKINI CHA KUSHANGAZA WATU TULIBAKI KINYWA WAZI WALIPOFIKA PALE NA WALINZI WAKITUAMBIA HAKUNA SHEHERE ZOZOTE MANA MPAKA SASA HATA PESA YA UKUMBI BADO KULIPWA. 

MI KAMA MDAU WA LIBENEKE NILIKUJA NA WAGENI WANGU TOKA SCOTLAND TUBURUDIKE NA WATANZANIA WENZETU LAKINI CHA KUSHANGAZA TULIBAKI HATUNA LA KUFANYA MBALI NA KWENDA KATIKA PARTY INGINE SOUTHBANK AMBAPO AKINA PROF.JAY WALIKUWA WANAKAMUA IPASAVYO.

 JE SI BORA WANGESEMA SHEREHE NI SOUTHBANK KULIKO KUTUUZA WATANZANIA TULIOKUJA NA NIA YA KUSHEREHEKERE HII MIAKA 50 YA UHURU KWA DHATI

ANGALIZO KAKA MICHUZI KAMA INAWEZEKANA NAOMBA UCHUJE BAADHI YA TAARIFA HASA HIZI ZINAZOHUSU KUTAARIFU WATU KUHUSU PARTY MANA ZINASABABISHA USUMBUFU MKUBWA KWA WATU NA KUDHARIRISHA BLOG YAKO; IMAGINE USWAHILI UNALETWA HADI LONDON REAL I CAN’T IMAGINE AND IS REAL SHAME TO ORGANIZERS

NI HAYO TU KWA WADAU

GODWIN (LONDON)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. NILISHAACHAGA KWENDA KWENYE SHEREHE ZA WATANZANIA LONG TIME KWA SABABU YA UJINGA WAO.

    ReplyDelete
  2. Mdau ni kweli tulifika Tottenham, Royal Banquetting Suite tukapewa taarifa na walinzi kuwa ubalozi umeshindwa kulipia ukumbi,hivyo baadhi ya watu tukaamua kwenda sehemu nyingine southbank ambako kulikuwa na sherehe nyingine ya Diamond, Ally Kiba na prof.Jay, cha kushangaza hapo tulimkuta na balozi yupo hapo na pia tumetoa kiingilio kikubwa na shughuli yenyewe hwaw jamaa wote watatu wamekuja saa saba na kumaliza saa tisa na muandaaji wa shughuli hii Ayub Mzee anasema hata yeye anashangaa nakusababisha vurugu kwa baadhi ya watu kwani watu wametoka miji mbali na London. Sasa kama walijua hayo maandalizi bado kwa nini wasingetufamisha mapema ili kusiwe na usumbufu.

    ReplyDelete
  3. MJOMBA HUJUI WABONGO. WANAITWA WA-BO-NGO!
    MIAKA 50 YA UHURU WA GHANA NA DR CONGO SHEREHE ZAO HAPA UK ZILIFANA SANA. ZILIPANGWA NA WATU WA NGAZI ZA JUU SERIKALINI WALIALIKWA.

    MIAKA 50 YA WABONGO NI NDOMO, UDAKU NA USHUZI TU. WASUBIRI WACHAT KWENYE F BOOK, BBM, LYCA, GT MOBILE, LEBARA NA USHUZI MWINGINE.

    WANAITWA WA BO NG O! EH

    ReplyDelete
  4. Wee Godwin ukome kusema ujinga uliofanywa na hao walioleta hilo tangazo ni uswahili. Kama hujui huo ni ushamba wa wabara, uswahili maana yake ni ustaarabu. Sasa kama hicho walichokifanya unaona ni ustaarabu nitakushangaa sana. MMEZOEA SANA KUTUKANA WASWAHILI, kwanza huku uswahilini tunasema kutotimiza ahadi ni unafiki na kukosa ustaarabu au hujawahi kusikia kuwa ahadi ni deni?

    ReplyDelete
  5. Karungula, Deo. L. Esq.December 11, 2011

    We have gone through whole issue ! What the so called Ruta made it off over the whole issue of being welcomed at a certain place remains personal ! So you educate him/her more importantly before this shame is publicly and vividly and made to us (Tanzanian Comunnity back in DSM) open !

    ReplyDelete
  6. TATIZO LA WABONGO KUDANDIA MISSION JAMAA WALIPO SIKIA TWANGA WANAKUJA KAMA KAWAIDA WAKADANDIA WAWAPE KITU KIDOGO WAFANYE SHOW PALE,TATIZO UBALOZI WETU NAO UMEKUWA KAMA KIJIWE WATU WATUMIA SIKU KUBWA KAMA HIYO KUPITIA UBALOZI BILA UBALOZI KUHUSIKA KIPLOTOKALI NI MAMBO YA KIUSHIKAJI ZAIDI,HAWAKUZINGATIA RATIBA YA TWANGA NA PESA YA KUWAONGEZEA MUDA WA TIKETI HAWANA WAMESUMBUA SANA WATU NI AIBU KWA TAIFA KWA UJUMLA.

    ReplyDelete
  7. Makubwa, madogo yana nafuu. Kumbe mnamtumia michuzi kwa matangazo ya kusafisha jia; Lol.

    ReplyDelete
  8. Bila shaka si wabongo wote huko Ulaya wapo hivyo, jana niliona short coverage hapa TBC na ITV zilikuwa sinaonyesha jinsi sherehe hizi za Uhuru zilivyopendeza Germany na Helsinki. Labda waandaji hapo wajifunze kutoka kwa wenzao, walifanikiwa vipi wao washindwe?

    ReplyDelete
  9. mIMI NINAVYOJUA UBALOZI NDIO ULIOSHIRIKI KUANDAA HIYO SHEREHE YA SOUTH BANK, NA KIINGILIO KILIKUWA KIKUBWA SANA.
    KWA UZOOEFU WANGU WENZETU WA NCHI NYINGINE HAPA UK ZA KIAFRIKA HUWA HAWATOZI RAIA WAO KUSHEREHEKEA TUKIO KUBWA NA MUHIMU KAMA HILI, HUWA NI SHEREHE YA WOTE NA BALOZI HUPEWA FUNGU MAALUM KWA AJILI YA SHUGHULI HIYO.
    NASHANGAA JE KWANI UBALOZI WETU KWELI HAUKUPEWA FUNGU LOLOTE KUANDAA SHUGHULI MUHIMU KAMA HII? AU NDIO......?
    NI SAWA KAMA KUNA WATU BINAFSI WALIAMUA KUANDAA PARTY MBALIMBALI HAPO NI SAHIHI KUWEKA KIINGILIO,
    LAKINI LICHA ZA PARTY HIZO TULITARAJIA SHEREHE YA BURE KWA WOTE INGETAKIWA IANDALIWE NA KUGHARAMIWA NA UBALOZI, SAWA KAMA AMBAYO HUFANYWA KWA MIKUTANO YA DIASPORA,
    HIVI KWELI UBALOZI WETU UMESHINDWA KUANDAA , MAIAKA HII MUHIMU 50?

    ReplyDelete
  10. Unaona unaona sasa Michuzi? huyo Annon hapo juu keshaanza kuleta Udini. hatuja dharau dini yoyote...tumesema Uswahili....

    ReplyDelete
  11. Wewe anonymous wa Sun Dec 11 06:31:PP nani amezungumzia udini hapa?

    Jee uswahili na udini ni sawa? Kwani pwani hakuna wakristo vile vile?

    Hebu jifunze lugha ujue kutafautisha baina ya vitu hivi viwili.

    ReplyDelete
  12. Hi ni yenu UK siyo Bongo , mbona US everything was very well organized, a few bad apples not all
    Tanzanians, shauri yenu siyo bongo

    mdau US

    ReplyDelete
  13. Bora hata hao walioshindwa kulipia ukumbi wamethubutu, hivi kweli ubalozi mmeshindwa hata kuandaa chai na maandazi kusherehekea hiyo miaka 50? Balozi mzima na msafara wako hamuoni tabu kudandia shughuli za watu na hotuba ndefuuuuuu?

    ReplyDelete
  14. Bora hata nyie mmefanya hiyp shehere japo chini ya daraja,hapa Swiss sidhani kama hata kuna ubalozi wa Bongo,yaani hapa kila siku nasoma wabongo uk,usa,germany,italy na kwengineko ukiona picha za Swiss na wakubwa wamekuja tena hata taharifa hatupati na kuangalia picha kwa michu then imetoka..Jamani wabongo Swiss tupendane

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...