Na Ripota wa Globu ya Jamii.
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetoa tahadhari ya kuendelea kunyesha mvua kubwa zaidi katika siku 10 zijazo, huku ikizitaja Alhamisi hadi Jumamosi kuwa ni siku za mafuriko mengine makubwa zaidi katika jiji la Dar es Salaam.Wakati TMA ikitoa tahadhari hiyo, Shirika la Reli Tanzania (TRL), limesitisha safari za treni ya abiria kwa muda usiojulikana kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma, kutokana na mvua
zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali ya nchi.
Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Agnes Kijazi aliyasema hayo jana katika taarifa yake kuwa kutokana na mvua hizo, ni vyema tahadhari zote zikachukuliwa mapema ili kuepuka maafa zaidi.“Wale wananchi ambao wanaishi mabondeni na waliokumbwa na mafuriko, wahame kutokana na mvua zinazoanza kunyesha Desemba 27 (jana), hadi Desemba 31 mwaka huu, kwani zitaleta madhara makubwa kwa wanaoishi mabondeni na sehemu nyingine mbalimbali,” alisema Dk Kijazi.
Alisema kwamba ukanda wa mvua unatarajia kuimarika maeneo mengi nchini na mvua zinatarajiwa kuanza kwenye ukanda wa pwani,ikiwemo Mkoa wa Dar es Salaam na kuongezeka kuelekea mwaka mpya wa 2012.
Dk Kijazi alisema mifumo ya hali ya hewa inaonyesha kuimarika kwa hali ya joto katika Bahari ya Hindi na kuongezeka kwa msukumo wa hewa yenye unyevunyevu kutoka misitu ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC).
Alisema hali hiyo imesababisha makutano ya upepo katika eneo la Mashariki na Kusini Magharibi mwa nchi,kuanzia leo kuelekea mwaka mpya... “Hali hii inatarajia kusababisha kuanza kwa vipindi vya mvua kubwa katika maeneo mengi hapa nchini.”Alisema maeneo ya mikoa ya ukanda wa Pwani (Dar es Salaam, Pwani, Mtwara, Lindi na Unguja), yanatarajiwa kuwa na vipindi vya mvua kubwa.
Dk Kijazi aliyataja maeneo mengine kuwa ni ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi ambayo ni Mikoa ya Mbeya, Iringa na Rukwa na Kanda ya Kati katika Mikoa ya Dodoma na Singida.“Kwa upande wa Magharibi mwa nchi, Mikoa ya Kigoma na Tabora na maeneo machache ya Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki katika Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara, yanatarajiwa kuwa na vipindi vya mvua kubwa,” alisema.
Alisema kutokana na viwango vikubwa vya mvua vilivyonyesha, ongezeko kidogo la mvua linatarajia kusababisha mafuriko na uharibifu wa miundombinu, hivyo ni muhimu tahadhari stahili ziendelee kuzingatiwa.Msimbazi wagomaLicha ya tahadhari hiyo ya TMA,baadhi ya wakazi waishio katika Bonde la Mto Msimbazi wamedai kuwa hawataondoka katika nyumba zao zilizokumbwa na mafuriko hadi watakapoona maji yamejaa katika mto huo.
Wakizungumza jana kwa nyakati tofauti wakazi hao walisema hawana pa kwenda licha ya kuisikia tahadhari hiyo ya TMA.“Ningekuwa mpangaji sawa, sasa mimi nimejenga nitakwenda wapi na kwetu ni mikoani huko,” alisema Ramadhani Kimbuyu wakati akifanya ukarabati wa nyumba yake huku akisisitiza kuwa kipimo chao kitakuwa Mto Msimbazi.Alisema kosa walilofanya awali ni kupuuza licha ya kuona mto huo umejaa jambo ambalo alidai hawatalirudia...
“Tukiona yamejaa tu tunahamia juu relini,yakipungua tunarudi.”Kauli ya RCMkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiki amesema Serikali utawachukulia hatua kali watakaokaidi amri ilivyotangazwa na Rais Jakaya Kikwete ya kutorejea katika maeneo hatarishi ya mabondeni.
“Tangu mwaka 1979 Serikali ilitoa amri ya watu kuondoka mabondeni lakini wamekuwa wakikaidi na kuendelea kuishi, kitendo hicho kimechangiwa na uzembe kwa baadhi ya viongozi katika kutekeleza agizo hilo,” alisema.
Sadiki alisema baadhi ya watu wameanza kurejea kwenye mabonde yaliyoathirika na kuwaonya wasirudi na badala yake watafute maeneo mengine kuendesha makazi yao.
Alisema Serikali itawapatia waliojenga mabondeni viwanja na siyo wapangaji. Wakazi hao wametengewa viwanja katika eneo la Mabwe Pande lililoko mpakani na Bagamoyo, Pwani na kwamba mpaka sasa
viwanja 700 vimeshapimwa.“Baada ya kugawa viwanja hivi tutaanza zoezi la kuzibomoa nyumba walizokuwa wanaishi maeneo ya mabondeni ili kutoruhusu watu kurudi tena huko kwani bila kufanya hivyo,hatutafanikisha lengo hilo,” alisema Sadiki.Treni zatishwaKutokana na mvua kubwa zinazonyesha maeneo mbalimbali nchini wa TRL, jana ulitangaza kusitishwa kwa safari za treni ya abiria kutoka Dar es Salaam hadi Kigoma...
“Safari hizo zimesitishwa hadi itakapotangwa vinginevyo baadaye,” alisema Meneja Uhusiano wa TRL,Midladjy Maez.Alisema abiria wote waliokuwa wamepanga kusafiri jana na katika treni zijazo,wanatakiwa kufika na tiketi zao katika ofisi za Stesheni Masta wa kituo husika ili warejeshewe fedha zao.
Walia na huduma mbovu Waathirika wa mafuriko waliopo katika Kituo cha Hananasifu, Kinondoni Dar es
Salaam, wamelalamikia uongozi wa kituo hicho kutoa huduma za chakula na malazi usiku bila umeme.Wakizungumza kambini hapo jana waathirika hao walisema, uongozi unatoa huduma hizo waathirika kuanzia saa 4:00 hadi saa 6:00 usiku kitendo ambacho kinafanya baadhi yao wapoteze vifaa vyao.
Kambi ya Hananasif imeshapoteza magodoro 50, ambayo inaelezwa na wananchi hao kuwa waliohusika ni baadhi ya viongozi waliopewa dhamana ya kuhudumia eneo hilo.
“Hapa kituoni hatuna umeme, lakini utaona viongozi wanakaa kimya mpaka ifike saa nne ndipo wanaanza kugawa magodoro, wengine wakishirikiana na vibaka usiku kuhamisha baadhi ya magodoro kupeleka mahali kusikojulikana,” alisema Hamed Shaban.Habari hii imeandikwa na Boniface Meena, Keneth Goliama na Aidan Mhando, Pamela Chilongola, Joseph Zablon, Ibrahim Yamola.


hivyo viwanja na wapewe kweli wahanga na sio mafisadi.
ReplyDeleteMIMI NITAILAUMU SEREKALI MAPAKA NAKUFA.WANAPOTAKA KUFANYA JAMBO lao hawashindwi. kwanini washindwe kutafuta njia za wananchi kutokuishi mabondeni...waliwezaje kuwahamisha wananchi kwa nguvu uwanja wa ndege washindwe kwengine???? Usanii waweke pembeni. Nachakushangaa tuna wasomi sasa sijui umeishia kwenye kalamu na makaratasi...veti??? RUSHWA MBAYAAA
ReplyDeletemi kwa mawazo yangu nafikiri ungetaja tarehe siku uliyofika airport kujua ni akina nani walikuwa zamu ili waweze kuambiwa, kingine hiyo bank ungeitaja na niwapi ili waweze kujua na pia huko ulikoenda mbugani ungetaja ni hoteli gani ili wajijue unajua si binadamu ni wasahaullifu tusameheane mpe pole sana mpenzi ndio bongo customer care mbovu halafu hatuachi kulalamika wakenya kwa kweli wako juu sana pole!
ReplyDeleteMimi nina ushauri:
ReplyDeleteMafuriko yanayotokea maeneo ya magomeni, k'ndoni mkwajuni, Mwannyamala yanatokana na eneo la barabara ya Kawawa kuanzia Kndoni Mkwajuni kufikia Magomeni Kanisani kufuata bonde, eneo hili lilipaswa kuwa na usawa wa juu na kuwa na madaraja madogomadogo kama saba hivi.
Barabara ya jangwani pia imejengwa ndani ya usawa wa maji, lilipaswa kuwa juu kidogo usawa wake ulipaswa kutafutiwa eneo la magomeni mapipa na Faya, barabara yake iko bondeni, ushauri wangu ni kuwa tukubali kwamba kuna tatizo la ujenzi wa miundombinu kutokufuata taratibu za sheria.
Uamuzi wa kuwahamisha wakazi wa mabondeni ufanyike sambamba na kufanya marekebisho ya msingi katika maeneo haya.
Tunaweza kurejea historia, miaka ya tisini, yalitokea mafuriko makubwa sana Bukoba Mjini, kuna baadhi ya watu walipoteza maisha, tatizo ilikuwa ni daraja la chini la Kanoni lilikuwa na eneo dogo la kutolea maji kwenda ziwani, baada ya matengenezo hayo ya kuongeza urefu na upana wa daraja tatizo hilo sasa limesahaulika.
Tutafakari na tuchukue hatua!!!
katerero73@gmail.com