Hii ni Barabara ya Old Bagamoyo inavyoonekana leo baada ya kujaa maji yaliyotokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha jijini Dar Es Salaam ambayo ilianza usiku wa kuamkia jana.
 Maji yamejaa kina kona na hakuna hata kwa kupita.na haya ni baadhi ya maeneo yaliyopata madhara hayo ya maji kwani maeneo mengine hadi madaraja yamevunjika na kusababisha kwa wakazi wengi wa jijini Dar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. TUMEDHUBUTU NA TUMEWEZA CCM OYEEEEEEEEEEEE MIUNDOMBINU

    ReplyDelete
  2. MBONA UMECHELEWA KUTUPA HABARI UNALETA PRECIAIN NDO NINI WATU WANKUFA HUKO

    ReplyDelete
  3. Kwakweli ni balaa,poleni sana mlioathirika

    ReplyDelete
  4. Haya ni maendeleo? Maneno mengi Bongo lakini harudi mtu kutoka hapa ughaibuni. Kama mkipata maafa ya Ufilipino Je? si mtakufa wote?

    ReplyDelete
  5. Ndiyo bongo yetu hiyo tambarare. Picha hizi ni za eneo la Mikocheni kabla hujafika kwa mwalimu. Ni nini hasa kimetokea hadi haya maji kuanza kutuama hivi? Nalikumbuka hili eneo vizuri na miaka ya nyuma, mvua ilikuwa ikinyesha hakukuwa na matatizo kama haya. Sijui tunaelekea wapi?

    ReplyDelete
  6. Bongo Tambarare Mnalalamika nini sasa Mpo Dar-es-salaam Mnapiga Ma Box si mrudi vijijini kwenu? ndio maneno yenu hayo au tunasema maneno ya wakosaji sindio tehtehteh.

    ReplyDelete
  7. bongo tambarare! Baada ya miaka 50 ya uhuru! Sina mengi picha zinaongea zaidi!

    ReplyDelete
  8. Kwa kweli sisi wa bongo ni blah blah tupu. Tunasingizia serekali wakati tumeichagua wenywewe na nani wakusema enough is enough kama siyo sisi wananchi. Lakini iliyobaki ni kutoa kashfa kuhusu nchi yetu na blah blah tupu. Najilaumu mwenywe pia kwa passiveness. Nina uzalendo lakini I'm controlled by the inability to take a step. Something is going down soon. Ndiyo kuna mafuriko so whats the plan?

    ReplyDelete
  9. poleni wenzetu kutoka dar hiyo ni mipango ya mungu na sio ccm.

    ReplyDelete
  10. Mnaonyesha huku na kuacha maeneo yaliyoathirika vibaya zaidi. Mnaficha nini?

    Dar es salaam

    ReplyDelete
  11. Turudi kufanya nini?we endelea kuogelea kwenye hayo maji machafu,unafikiri hatupendi kurudi kwetu?lkn mambo km haya ni km hatuna serikali,hapo na maradhi yataanza mana kuna maji ya choo humohumo.Yani kwakweli mi sirudi ng'o.

    ReplyDelete
  12. MAJI BWANA HAYANA MCHEZO, HILO NI BONDE LA MPUNGA MSASANI SASA SISI NA PESA ZETU ZA UFISADI TUMEWAHONGA WIZARA NA CITY COUNCIL BAADA YA NYERERE KUFARIKI NA TUKAKATIWA VIWANJA, TUKAFIKIRI PESA INAKOMESHA MAJI, LA HASHA, MAJI YANA SEHEMU ZAKE ZA HASILI MILELE NA MILELE - SIKU YATARUDI SEHEMU YAKE, KAMA HIVI SASA - BONDE LA MPUNGA. SASA KAMA WEWE ULINUNUA NYUMBA AU KIWANJA SEHEMU HIZI WAKATI WA KIANGAZI SASA KADAI URUDISHIWE PESA YAKO. NA PIA KAMA UMEKODI APPARTMENT ZA $ 3,000 hapo MIKOCHENI - KALAGABAO

    KWA MAONI YANGU MIMI - HAO WALIOJENGA BONDE LA MPUNGA MSASANI/MIKOCHENI HATA KAMA HIZO NYUMBA ZENU NI MA BUNGALOWS HAMNA TOFAUTI NA WALALA HOI WALIOJENGA JANGWANI MKWAJUNI, MBURAHATI NA USWAHILINI.

    ReplyDelete
  13. ACHENI KULAUMU MAAFA NI MAAFA TUU.HAYO NI MAAFA NA SI PKULUMIWA MTU.JAPANI NCHI BORA KWA TECHNOLOGY NA MAFA YANATOKEA SEMBUSE SISI TZ

    ReplyDelete
  14. Our infrastructure are still in a sorry state, roads are still pot hole infested, coruption is still high, our hospitals are colapsing due to lack of funds, our MPs spend the entire 5 years fighting each other and worse of all, the gap between the rich and the poor is getting wider every day. Look at the slums people live in. We are not yet where you seem to think we are, we are years away from being anything than poor, thats if you are not that dreamer called unlucky guy.

    ReplyDelete
  15. watu tunaojidai tupo nje na tusiotaka kurudi nyumbani kwa kuwa hatuwezi fanya cha maana ama hatuna qualifications tumepata cha kuongea na ku-provr kuwa tupo sahihi...marekani yenyewe ilikumbwa na miundombinu bora..this is natural disaster na haina bongo tamarale ama uk au marekani tambarare..

    ReplyDelete
  16. Nasikitika kuona tunalalamikia serikali wakati ni mother nature nimeishi Europe na U S A ni vitu vya kawaida uwezi shindana na mother nature

    ReplyDelete
  17. JAmani jamani watanzania hayo ni mambo ya global warming mnajua kwa nini kulikuwa na mkutanio wa mabadiliko ya hali ya hewa hiyo ni dunia nzima angalieni ninikimetokea juzi pHilIpinE, wat 1800 wamefariki dunia kwa mkasa huo huo. hilo ni tukio lazima lipime mara moja mpaka tatu kwa kila miaka 50-

    tumuombe yarabi atunusuru!

    ReplyDelete
  18. Hahahah Mdau mtoa Maoni wa 16 uliyeishi Europe na USA kwa Tanzania hapo analaumiwa Raisi wa nchi Miundo mbinu na Serikali kwa mvua kubwa na mafuriko yanayofikia juu ya mapaa ya nyumba!

    ReplyDelete
  19. acheni lawama za kinafki fikirieni ndugu zetuwanavyopta shida hizi ni mvua zilizopita piata kiwango. nchi ngapi zenye miuondo mbinu zinakumbwa na matatizo acheni ashabiki jamani hakuna mtu anaye weza zuia gharika.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...