JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
TAARIFA KWA UMMA
WANAHABARI WAPANDA MLIMA KILIMANJARO
Kama sehemu ya Maadhimisho ya mika 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara, wanahabari 10 wanapanda Mlima Kilimanjaro kwa mwaliko wa Hifadhi za Taifa (TANAPA).
Jana (Jumanne) wanahabari hao ambao wako chini ya uongozi wa Pascal Shelutete ambaye ni Meneja Uhusiano wa TANAPA, walifanikiwa kufika katika kituo cha pili cha kupanda Mlima huo kiitwacho Horombo.
Wanahabari hao wanategemea kufika kileleni mapema tarehe 9/12/2011 kama ilivyopangwa. Wanahabari hao wanapanda mlima huo wakiwa pamoja na kikundi cha wanajeshi ambacho kinaupandisha Mwenge wa Uhuru Mlimani Kilimanjaro.
Wanahabari hao ni Asraji Mvungi wa ITV, Daniel Mjema wa Citizen, Musa Juma wa Mwananchi, Emmanuel Amasi wa TBC na James Range wa Star TV. Wengine ni Irene Mark wa Tanzania Daima, Lilian Joel wa Uhuru, Salome Kitomari wa Kilimanjaro Press Club, Juma Kapipi wa Channel Ten, Nicholaus Mbaga wa TBC na Sheiba Bulu wa Wizara ya Maliasili na Utalii.
George Matiko
MSEMAJI WA WIZARA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...