JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UCHUKUZI
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI
Taarifa hii inatoa mwelekeo wa mabadiliko ya mifumo ya hali ya hewa na mvua kuanzia mwezi Desemba 27, 2011 kuelekea mwaka mpya 2012.
Ukanda wa mvua unatarajiwa kuimarika maeneo mengi nchini na mvua zinatarajiwa kuanza kwenye ukanda wa pwani kesho ukiwemo mkoa wa Dar es salaam na kuongezeka kuelekea mwaka mpya 2012.
Mifumo ya hali ya hewa inaonyesha kuimarika kwa hali ya joto la Bahari ya Hindi, sambamba na kuongezeka kwa msukumo wa hewa yenye unyevunyevu kutoka misitu ya Kongo na kusababisha makutano ya upepo katika eneo la mashariki na kusini magharibi mwa nchi kuanzia Disemba 28,2011 kuelekea mwaka mpya 2012.
Hali hii inatarajiwa kusababisha kuanza kwa vipindi vya mvua kubwa katika maeneo mengi hapa nchini.
Maeneo ya mikoa ya ukanda wa pwani( mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Mtwara, Lindi na Kisiwa cha Unguja,), Nyanda za juu kusini magharibi(Mikoa ya Mbeya, Iringa na Rukwa), kanda ya kati(Mikoa ya Dodoma na Singida) na magharibi mwa nchi(Mikoa ya Kigoma na Tabora) na maeneo machache ya Nyanda za juu kaskazini Mashariki(mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara) yanatarajiwa kuwa na vipindi vya mvua kubwa.
Kufuatia viwango vikubwa vya mvua vilivyonyesha, ongezeko kidogo la mvua linatarajiwa kusababisha mafuriko na uharibifu wa miundombinu. Mamlaka inashauri tahadhari stahiki ziendelee kuzingatiwa.
Meaeno mengine ya nchi yanatarajiwa kupata mvua za kawaida katika kipindi hicho.
Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia mwenendo wa mifumo ya Hali ya hewa na athari zake na itaendelea kutoa taarifa na tahadhari kila inapobidi.
Dkt. Agnes L. KIjazi
MKURUGENZI MKUU
Mafuriko yametokea ndo utabili unafuata.Dada Agnes bado haujatushawishi wataalam wa mambo labda wakulima wa kule vijijini na ambao hawana mitandao.Jipangeni upya ndani ya mamlaka yenu hapo.
ReplyDeletehebu toeni upuuzi wenu hapa hadi matatizo yashatokea ndio mnajidai mnatabiri?
ReplyDeleteMwenendo wa mabadiliko ya hali ya hewa, Mamlaka ikitoa taarifa zake kama hizi mara nyingi tumekuwa hatuzingatii.
ReplyDeleteNi vizuri kufuatilia mwenendo wa mabadilko ya hali ya hewa unapotolewa na Mamlaka kama hivi hapa na ktk vyombo vingine vya habari bila kupuuza ingawa wakati mwingine watu watasema hauakisi kama hali halisi inavyotokea!.
Mbona wiki moja kabla ya mafuriko hatukuona maelezo ya dizaini hii. Mpaka yatokee ndo wanaamka sasa!
ReplyDeleteMatangazo huwa yanatolewa kila siku. Mara baada ya taarifa za habari kuna kipindi cha utabiri wa hali ya hewa, lakini watu hatufuatilii. Ikiisha tu taarifa ya habari kinapofuata kipindi cha utabiri wa hali ya hewa watu wanaondoka.
ReplyDeleteBinafsi nilishawahi kumsikia mtu akisema, hawa watu wa hali ya hewa hakuna chochote, wanampangia Mungu juu hali ya kesho? Wanakufuru sana. Je, kwa mtu kama huyu utamshawishi vipi kufuatilia mambo ya hali ya hewa?
Sasa nauliza, mnataka watu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa waseme kwa jinsi gani hata mfuatilie. Ndivyo tulivyo, hasa sisi watu wa bara la Afrika, mambo mengi tunayadharau lakini wepesi wa kulaumu pale matatizo yanapotokea.
Tuweni wakweli; JE, NI MARA NGAPI SERIKALI IMEKUWA IKITUASA KUONDOKA MABONDENI? SIYO HIVYO TU, JANA TU VYOMBO VYA HABARI VIMETANGAZA KUWA WATU WAMEANZA KUREJEA TENA KATIKA MAENEO YALE YALIYOTOKEA MAFURIKO. SASA TUNATAKA TUELEZWE KWA JINSI GANI??? MSIWATUKANE BURE WATU WA TMA, WAKATI MWINGINE NI MAKOSA YETU SISI WENYEWE. TUMWOGOPE MUNGU TUWE WAKWELI. HAKUNA WA KULAUMIWA KWA JANGA HILI, NI KUPEANA POLE NA KUMSIHI MUNGU ATUEPUSHE NA JANGA KAMA HILI LISITOKEE TENA.
POLE MAMA AGNES KIJAZI KWA LAWAMA HIZI UNAZOBEBESHWA, FAHAU MKUBWA NI JAA.
Nafikiri mchangiaji wa kwanza huwa hasikilizi vyombo vya habari, nakumbuka kwa masikio yangu mwenyewe,hali hii ya mvua,mafuriko na uharibifu mbalimbali ilitangazwa kuanzia sep mwishoni au oktoba mwanzoni,kuwa kutakuwa na mvua nyingi,na mvua za mwakam huu zitaleta maafa,mafuriko n.k hivyo watu wachukue tahadhari, na kwa waliopo mabondeni wachukue precautions. Kwa yeyote ambaye alisikia atanisaidia kwa hili, i remain to be corrected though!
ReplyDeleteMdau wa Tatu (3) na wa tano (5) ni kweli sisi hasa wa Tanzania hatuzingatii matangazo ya hali ya hewa ktk vyombo vya habari,,,TV itatoa matangazo yote ikifika ktk hali ya hewa kila mtu anaondoka ,au wanabadili Stesheni kwa kutafuta Michezo ya Runinga na Mechi za Mipira!
ReplyDeleteJAmani acheni kuwaonea watu wa hali ya hewa! matangazo yalitolewa mwenzi wa tisa na kila siku matangazo yalitolewa! na mara kadhaa watu wa bondni wametahadharishwa mntaka wafanye nini? wawashike mikono watu wa mabondeni? juzi yametokea mafuriko! nendeni mkaone pale bondeni msimbaziwatu wamekaidi na wamesema hawatoki! mmoja amesema ameishi hapo miaka 20 na hakikutokea kitu na kwamba ile bahati mbaya! nyie mnachekesha kweli! semeni na ndugu zenu wa mabondeni!
ReplyDeleteNinyo mnaokataa kuamini taarifa ya MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA kwa vyombo vya Habari kama ilivyo rusha humu ktk Blogu ya Jamii jana Jumatatu tarehe 26 Desemba, 2011.
ReplyDeleteJE KAMA HAMKUBALI TAARIFA HIYO,HAMUONI ANGA LILIVYO LEO TAREHE 27 DISEMBA, 2011?
JUA LINAONEKANA?...HAKUNA MAWINGU?
Duhhh Wa Tanzania wagumu sana kweli kazi ipo!
Mimi nadhani Mamlaka hii haiwezi kuepuka lawama, kwa sababu kuweka magazetini na katik Tv si watu wote hawa maskini wa bondeni hawawezi kuwa na Tv na magazeti... hivyo walipaswa kuwa na mfumo wa kutumia public addressing systems kuwatangazia watu katika mitaa, hasa wanapoona kuwa mabadiliko ya hali ya hewa yatasababisha majanga.. hiyo inakuwa ni tahadhari ya dharura.. wenzetu nchi nyingine wanafanya hivyo
ReplyDeleteWale wanaosema kuwa matangazo yanatolewa kila siku wafuatilie waone. hakuna umakini kila option ipo katika matangazo yale.
ReplyDeleteUtasikia kutakuwa na mvua, jua, baridi joto kila kitu hivyo watu wamechoka kabisa.
Yaani utabiri ni kama vile kusema kuwa mama huyu mjamzito atajifungua mtoto wa kike ama wa kiume
mi naona hapo zimetabiriwa hali ya hewa zote.
ReplyDeleteKutakuwa na mawimbi madogo, makubwa na hadi ya kati. Utabiri gani huo wa hali ya hewa. Hawajui chochote. Europe utabiri wao ni mwingine kabisa. SABABu wenzetu wana vifaa na sisi hatuna vifaa. Naya vitu vinginesi vya kulaumu nimshiko tu. EUROPE NA USA oyee! Niko tayari kubeba box ughaibuni.
Hakuna sababu ya kuilaumu Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania!.
ReplyDeleteHizo taarifa za matangazo ya Vipaza sauti Mtaa hadi Mtaa kwa watu wabishi kama Wa Tanzania zitasaidia?
Hebu angalia Mafuriko yemetokea juzi tu , waathirika wamepewa makazi ya muda, angalia sasa tayari wameanza kurudi kule kule makwao kuliko furika eti kwa kigezo maji yamepungua!,,,huku Mamlaka ikiwa imetoa taarifa ya mvua nyingine jana tu!
Mfano kukiwa hakuna hata dalili ya mvua wala mawingu jana 26 Disemba, 2011 Taarifa Hii ilirushwa na Mamlaka kuwa kutakuwa na mvua tena!
Leo hii 27 Disemba, 2011 kumekucha mawingu yanaokena sehemu ya Dar Es Salaam, halafu mnaleta ubishi Mamlaka haiwajibiki haitoi matangazo!
Hayo yanayowachosha kila siku ndiyo ya msingi. Unapoacha kufuatilia kwa kuwa jana walisema hivi hivi na leo hivi hivi basi unaacha kufuatilia au kusikiliza. Hujui siku unayoacha kuvaa nguo ndiyo siku unakutana na mkweo hiyo.
ReplyDeleteWabongo wabishi tu. Yaani unawatetea kuwa watu hawana Tv au Redio. Kweli wote waishio mabondeni walikuwa hawana TV au redio? Usiwadhalilishe.
Jamani tusilaumiane kwa yaliyotokea. Tujipange kwa tahadhari zaidi. Kama si wabishi, mbona tunarudi tena kule kule?