Na Mwandishi wa Jeshi la Polisi Zanzibar
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar, limejipanga kikamilifu kuhakikisha kuwa sherehe za siku kuu za Krismas na Mwaka Mpya zilizopo mbeleyetu, zinashehehekewa kwa amani na utulivu.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar, limejipanga kikamilifu kuhakikisha kuwa sherehe za siku kuu za Krismas na Mwaka Mpya zilizopo mbeleyetu, zinashehehekewa kwa amani na utulivu.
Afisa Habari wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, amesema kuwa tayari Viongozi Waandamizi wa Polisi mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar wameanza kutembelea maeneo tofauti yatakayokua na mikusanyiko mikubwa ya watu wakati wa ibada za mikesha ya sherehe hizo.
Inspekta Mhina amesema kuwa Viongozi hao wa Jeshi la Polisi pia wamefanya mazungumzo na viongozi wa Makanisa mbalimbali na kuweka mikakati ya pamoja ya kudhibiti usalama.
Amesema tofauti na utaratibu wa mawasiliano ya barua na sim uliozoeleka miongoni mwa taasisi mbalimbali za Serikali, Viongozi wa Jeshi la Polisi wameama kufika wenyewe kwa Viongozi hao wa madhehebu ya dini na kfanya mazungumzop ya ana kwa ana na kuweka mikakati ya pamoja itakayosaidia kudhibiti ulinzi na usalama wakati wa sherehe hizo.
Akizungumza na baadhi ya Viongozi wa Makanisa ya Anglikana na Romani Kathoriki kwa nyakati tofati mjini Zanzibar, Mkuu wa utawala wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar SP. Bukini Ali Mohammed aliwahakikishi viongozi hao kuwa Jeshi la Polisi litaweka ulinzi wa kutosha kwenye makanisa yatakayokuwa na mkesha wa ibada siuk hiyo ili kwafanya wamini kfanya ibada yao bila ya hofu
Amesema pamoja na kuweka ulinzi katika maeneo ya nyuumba za ibada, pia Jeshi la Polisi litaimarisha doria za askari wa miguu na magari katika maeneo mengine yatakayoukwa na mikusanyiko ya watu ikiwa ni pamoja na maeneo ya viwanja vya burudani kwa watoto.
Kwa upende wao Bw. John Mwakanjuki Mkuu wa utalii katika Kanisa la Anglikana Mkunazini na Padri Evaristus Mushi, wa Kanisa la Roman Kathoriki mjini Zanzibar, wamelishukuru Jeshi la Polisi na kupongeza utaratibu wake wa kila mwaka wa kuimarisha ulizi kwa waumini wa dini mbalimbali hasa kwa nyakati za sherehe kubwa kwa imani ya dini zao kama ilivyo kwa makanisa.
Naye Kamanda wa Polisi mkoa wa Mjini magharibi ACP Aziz Juma Mohammed, amewatahadharisha wazazi na walezi kutowaacha watoto wao wakiranda barabarani na kuogelea kwenye fukwe za bahari pasipo na uwangalizi wa watu wazima ili kuepka ajali za magari na kuzama majini ama kupotea.
Amewaonya madereva kua makini wanapoendesha magari na pikipiki ili barabarani ili wasiwe chanzo cha ajali kwa watmiaji wengine wa barabara na kwamba kwa yeyote atakayekaidi agizo hilo atapambana na mkono wa dola.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...