Katibu wa Bunge la Tanzania, Dr. Thomas Kashililah (kushoto) ambae pia ni Katibu wa Afrika wa Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola akimfafanulia jambo Katibu Mkuu wa chama hicho duniani, Dr. William Shija wakati walipokutana jijini London jana, Dr. Kashililah na ujumbe wake wako London kuhudhuria Mkutano wa Kamati ya Utendaji ya Dunia ya Chama hicho. Kulia ni Katibu Msaidizi wa Afrika wa chama hicho, Nd. Demetrius Mgalami ambae pia ni Mkuu wa Itifaki wa Ofisi ya Bunge.
Mwenyekiti wa CPA barani Afrika ambae pia ni Spika wa Bunge la Majimbo nchini Afrika Kusini,Mheshimiwa Mninwa Mahlangu (wa kwanza kushoto) akizungumza na Sekretarieti ya chama hicho barani Afrika inayoongozwa na Dr. Thomas Kashililah walipokutana jijini London. Wengine pichani ni wajumbe wa Sekretarieti hiyo, Nd. Demetrius Mgalami(wa kwanza kulia) na Nd. Emmanuel Mpanda (wa pili kushoto) ambae pia ni Mkurugenzi Msaidizi katika Ofisi ya Katibu wa Bunge
Katibu wa CPA Barani Afrika na Katibu wa Bunge la Tanzania, Dr. Thomas Kashililah akizungumza na wajumbe kutoka Afrika wanaohudhuria Mkutano wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola unaofanyika London, kutoka kushoto ni Mhe. Mary Boya kutoka Cameroon na Mhe. Elijah Okupa kutoka Uganda. Tanzania ndio makao makuu ya Chama cha Wabunge wa Madola ambapo Katibu wa Bunge la nchi yenye makao makuu ndio kikatiba huwa Katibu wa Bara husika. Picha zote na Saidi Yakubu wa Ofisi ya Bunge

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Hivi tufike mahali tujiulize, safari hizi za viongozi wa serikali, bunge na mashirika ya umma vina tija gani? Gharama ya kila safari fedha yake ingeelekezwa kwenye madeski na dispensary na hawa jamaa wakabaki nyumbani situngekuwa na tofauti ya maendeleo ya elimu na kupunguza vifo vya watu wetu?

    ReplyDelete
  2. CPA Africa mkutano London!!!!!

    ReplyDelete
  3. jamani Said Yakub mbona hayupo kwenye picha naye ni cordinator wa CPA.

    ReplyDelete
  4. Sasa wewe Annony hapo juu umeshaambiwa kwamba ni Katibu wa Bara la Afrika unategemea abaki dodoma kuendesha chama hicho?ama kweli akili ni nywele!

    ReplyDelete
  5. kila siku wanaota wapate safari na marupurupu yake utaalamu wasasas un videoconference itasaidia kuokoa gharama kama hizi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...