Baada ya kumaliza kutumbuiza Athens,Amsterdam na Napoli, bi Kopa alirejea tena Athens 26/12 na kukutana na watanzania pamoja na watoto wao katika ofisi ya jumuiya.
Alipomaliza kusaini kitabu cha wageni bi Kopa alielezea furaha yake jinsi tulivyompokea na alipendezeshwa mno na umoja wetu "Ukweli furaha yangu haielezeki kwa maneno na nimeridhishwa mno na jinsi mnavyoishi na hasa kuwa na jumuiya iliyopangika kama hii”Aliyasema hayo baada ya kutembezwa katika eneo la Serengeti sehemu yenye michezo ya pool na kantini ya jumuiya.
Kabla hajaondoka alikabidhiwa zawadi ya jumuiya toka kwa Katibu bw.Kayu Ligopora ambaye alimshukuru bi Kopa kwa jinsi alivyowafurahisha watanzania wa Ugiriki ambao wengi wao walihitaji aje tena mwakani.
Atarudi Tanzania 28/12.
KAYU LIGOPORA
KATIBU WA JUMUIYA YA WATANZANIA UGIRIKI


AAH WAZEE WA UMANGANI MUMEZIDI SASA HATA KAMA NCHI IMEFILISIKA,GUEST BOOK SIO ZAWADI YA KUMPA MAMA KOPA.
ReplyDeleteNOTE:MAMA KOPA SOMA KITABU CHOTE KABLA HUJAONDOKA,WAZEE WA BEACH HAWAAMINIKI..TEHE TEHE
we anony hapo juu uwe unasoma habari kabla ya kutoa maoni kwani umeambiwa amepewa zawadi ya guest book? Hicho kitabu amesaini tu! Ujuaji ukizidi bwana...
ReplyDeletewee chizi nini au inaonekana uwelewaji wako mdogo,kapewa guest book kwa ajili ya kusaini na sio zawadi au haujui maana yake? ni kitabu cha wageni na kila anaetembea usaini na ukiaacha,babu wewe upo dunia gani inaonekana mchanga wa macho haujakutoka.
ReplyDeletewe limbukeni aliyekwambia mtu anapewa Guest Book nani?
ReplyDeletefikiri kabla ya kuropoka au umechanganyikiwa baada ya kuku wako kwenda maji?
SAMAHANI NILIKUWA SIKUSOMA VIZURI MSINISHAMBULIE HAMNA DOGO NYIE?
ReplyDeleteNILIDHANI KWA KUWA NCHI INA WAYA NDIYO JUMUIYA IMETOA ZAWADI YA GUEST BOOK KUMBE SIYO.SORRY WADAU WENZANGU
we tambua matatizo ya kiuchumi yameikumba serikali ya ugiriki, watu tunapeta kama kawa kwasababu hakuna Mbongo anayefanya kazi ktk serikali ya ugiriki watu tunafanya kazi katika sekta za watu binafsi, na ndio mana tunaruka nyanga kila kukicha coz maisha hatuyaogopi kama wewe, na new year Matonya in ATHENS,ukijinyonga shauri yako sisi maisha yanaendelea.
ReplyDelete