Usiku wa jana 23/12 hadi leo asubuhi,Malkia wa mipasho bi Khadija Kopa aliwatumbuiza watanzania katika ukumbi wa Axum Athens.Ukumbi ulifunguliwa kwa show ya Mike Jackson na  .Sandra walioshangiliwa  na umati uliofurika ukumbini humo kwa nyimbo zao mwanana.Bi Kopa alialikwa na jumuiya ya watanzania ugiriki,ambayo imeanza mikakati ya kuwaalika waimbaji tofauti wa kitanzania.Bi Kopa atatumbuiza Holland leo 24/12 na kesho  J'pili atafanya vitu vyake Italy.Atarejea Ugiriki 26/12 siku ambayo atajumuika na  watoto  wetu ofisini katika sherehe maalum iliyoandaliwa kwa ajili  yao. Baadae atarejea Tanzania.
Kwa picha zaidi tembelea fb WATANZANIA UGIRIKI
  
KAYU LIGOPORA
KATIBU MKUU
JUMUIYA YA WATANZANIA UGIRIKI




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. KWA SISI TULIO ULAYA SIKU HIZI UKITAJA "GREECE" MOYO UNASHTUKA KIDOGO!

    ReplyDelete
  2. pamoja na hali ngumu ya kiuchumi inayoikumba ugiriki,maisha bado yanaendelea. Ugumu wa uchumi daima siyo sababu kuu ya kuzuwia starehe zisiendelee.Hata wakati wa vita vya pili vya ulimwengu, starehe zilikuwepo.Hivi ndivyo maisha yalivyo.
    Mdau wa Ugiriki.

    ReplyDelete
  3. Mtupe basi ratiba kamili huyu bibiye atakapokuwa Italia. Tujue ni mji gani na ukumbi gani na saa ngapi!!

    ReplyDelete
  4. hongereni sana,waache wapige kelele Umangani hivi umangani vile maisha hivi maisha vile,watu wanakula kiulaini bila wasi wasi,usawa ni usawa tu,Mdau uk

    ReplyDelete
  5. uk wanatakujitoa kwenye umoja wa ulaya kwa ajili ya shida zenu wamechoka kuendelea kuwasaidia kila siku nyie tu utafikiri mpo afrika?aibu

    ReplyDelete
  6. hadija kopa kafanana na aretha franklin.

    ReplyDelete
  7. ETI NI KWELI ARETHA FRANKLIN ANA UNDUGU NA HADIJA KOPA?

    KUNA MENGI YANASEMWA KUWA NI NDUGU WA DAMU KAMA VILE BARAKA OBAMA NA NDUGU ZAKE WA KENYA

    ReplyDelete
  8. Dah hiyo greece imechoka mpaka aibuu sasa cjui ndugu zangu mnakuwa na moyo gani wa kufanya starehe hizo.Mana cc wa nchi zingine za ULAYA tunaona hiyo greece afadhali ya Bongo yani chooka mbaya.Wewe Kopa cjui kama umeingiza kwenye sherehe iyo watu wenyewe wamepigika rudini TZ jamani mkajenge nchi yetu

    ReplyDelete
  9. Ma-haters, eat your hearts in envy. Bw na Bi Furaha.

    ReplyDelete
  10. hili bibi badala kurudi kwa mungu bado tu anaendeleza maasi,na we unosema uk wanataka kujitoa kwa shida za umangani we mwenyewe unaosha vibibi hapa uk unanawisha mavi kama huna shida rudi kwenu tanzania sio ukae hapa ujiripue,mdau uk

    ReplyDelete
  11. wabongo mna matatizo maisha yanaendelea uwe bongo uwe ulaya shika lako sio kuangalia mwenzio kavaa nini anakula nini anaishi maisha ya aina gani ndiyo maana hamna maendeleo

    ReplyDelete
  12. Mdau wa kwanza (KUSIKIA 'GREECE' MOYO UNASHITUKA KIDOGO) na wa nane (Dah hiyo greece imechoka mpaka aibu)!

    Wandugu mnajua sisi binaadamu tuna ile kitu mazoea na mtu hakubali kuitwa ameshindwa!

    Maneno yenu ni kweli kwa sababu dunia nzima sasa mambo ni magumu na kama hilo linajukana ,ni busara kukubali matokeo, mficha maradhi mauti humuumbua!!,,,itafaa wandugu huko Greece wageuze mwelekeo warudi nyumbani tena ikiwezekana kwa kuficha soo na maneno ya watu moja kwa moja waende TABORA KUCHANA MBAO AMA KUPAKUA ASALI MWITU na wengine WAREJEE NYUMBANI DODOMA NA SINGIDA WAKAVUNJE KOKOTO na wengine,kwa vile UGIRIKI NI HODARI KWA UVUVI WATAKUWA WAMEPATA UZOEFU HUKO, wafikapo huku nyumbani WACHUKUE NYAVU WAENDE RUFIJI NA MAFIA WAKAVUE SAMAKI NA KAMBA zote hizi ni sekta zetu za KUJENGA NCHI NA UCHUMI TANZANIA!

    ReplyDelete
  13. GREECE na nchi zingine za Ulaya baada ya kufilisika Kifedha na Kiuchumi, imebidi baadhi za sehemu watu wahamie vijijini huko kwa kazi za mashambani kuvuna matunda na kilimo cha mboga!

    Labda angalau walio mijini kama GREECE SPAIN NA ITALY ,wenye nafuu ya maisha ni wale wenye biashara ya kisasa ya mavumbi!

    Wanaotia huruma zaidi ,ni wale waliopo TANZANIA wakipanga kwenda Ulaya kupata Ukimbizi na wale waliopo huko Ulaya wanaoota kupata UKIMBIZI!

    KITU AMBACHO NI NDOTO ZA MCHANA KUMWOMBA MKEKA MTU ALIYE NA MSIBA NYUMBANI KWAKE!

    WANDUGU TUTAFUTENI NJIA MNYINGINE YA KUKABILIANA NA MAISHA, HIVI SASA NI VIGUMU NCHI ZA ULAYA NA MAREKANI KUBEBA WAKIMBIZI KWA VILE WAO WENYEWE WAMEFILISIKA KIFEDHA NA KIUCHUMI!

    ReplyDelete
  14. Rudini kutoka Ulaya hasa Greece na Marekani mfike nyumbani mje kufanya UMACHINGA na KULIMA,,,,Raisi ameanzisha Diaspora na pia kuna mpango wa kilimo kwanza!!!.

    ReplyDelete
  15. Mambo yakikataa Greece msilazimishe,!

    Mpange kurudi, sawa RE PATRIATION MTU ANAFIKIA GEREZANI lakini sio ishu unaweza lipa faini au kifungo cha miezi 6 tu unatoka!

    Mtoe taarifa Ubalozini mrudishwe nyumbani Bongo!

    ReplyDelete
  16. mnachonga sana hivi unafikiri ulaya inaweza kufirisika kikweli? hizo ni politiki tu kuweni na akili ndio maana mtabakia kuwa wa mwisho duniani

    nchi za ulaya ndio washika mpini sasa njaa itatokea wapi?

    alafu wanaowasema hao ndugu zetu wa ugiriki eti uingereza itajitoa kutokana na kuchoka kuwasaidia ugirikia hayo ni mambo ya serikali na wala sio mambo ya wewe mkimbizi wa uingereza na wenzio wa ugiriki kupigana madongo

    shida itaikumba serikali na wala sio wewe mkimbizi wa uwongo unaepiga boxi mpaka mkeo anakushinda kumtimizia haki yake mpaka unasaidiwa kazi

    waacheni watu na maisha yao na wewe angalia maisha yako sio wakati wa kuangaliana tujaribu kubadilika watanzania maisha hatutofanikiwa

    eti ulaya imefirisika hivi unacheza na washika mpini?
    misaada kila siku inaendelea kuja huko afrika kutoka kwa hawa wazungu mamilioni ya misaada hivi kweli wana njaa hawa?

    shame on u unaesema kuwa ulaya wameishiwa acheni wenzenu na politiki zao msiwaingilie hawana njaa hawa wanaongoza dunia shauri zenu.

    ReplyDelete
  17. Mdau wa 16 .....mnachonga sana hivi mnafikiri ulaya inaweza kufilisika?......Anonymous wa Mon Dec 26,02:35:00 PM 2011

    Hiyo rasilimali ya Ulaya na Marekani ambayo unasema haifilisiki imetafutwa kwa ajili ya vizazi vyao na sio wewe muomba Uraia au mpata Uraia kwa njia ya (Urajisi) au Usajili.

    Kwanza wenyewe mnalalamika nchi hizo zina sera za Ubaguzi mnaona wenyewe hata hao Mastaa wanaocheza mpira wa kulipwa huko ktk Klabu za Ulaya na kulipwa EURO kibao wanadharauliwa na kubaguliwa!

    Itakuja kuwa wewe Maganga au Mbonde uliyepata URAIA kwa usajili kama wa namba za magari TZ?

    Wewe huna ufahamu kabisa, Hakuna jamii walioishi uhamishoni Duniani kwa Karne nyingi kama Waisrael, lakini kutokana na Madhila waliyoyapata ugenini kwa kutumiwa na kudharauliwa wamejikuta hata hii leo ukimkuta mtu ana Uraia Marekani, Ulaya au popote duniani lakini ana damu ya Israel bado anajitambua ktk Taifa la Israel!

    KALAGA BAHO, WEWE UTAKE USITAKE CHAKO KIPO HUKU RUDI NYUMBANI TANZANIA UJENGE NCHI, ONDOKA UTUMWANI ULAYA NA MAREKANI NJOO ULIME!

    ReplyDelete
  18. Mdau wa 16 juu Uraia wenyewe wa Ulaya ni kwa kupitia tiketi ya Kujilipua ya Ukimbizi?

    Hahahaha, mmekalia kuti kavu siku yeyote yakitokea mabadiliko ya serikali ikaja serikali ya siasa kali woooote mtanyangánywa pasipoti na mtarudishwa kwenu!

    Sasa kazi kwao wale Watanzania waliojilipua:
    -(kupata Ukimbizi kwa njia ya Usomali)breki ya kwanza ni Mogadishu Somalia mnapokelewa na al shaabab!.
    -(kupata Ukimbizi kwa njia ya Urundi) breki ya kwanza Bujumbura mnapokelewa na Banyamulenge!.
    -(kupata Ukimbizi kwa njia ya Ukongo) breki ya kwanza Kinshasa mnapokelewa na Etienne Tshisekedi aliyejiapisha mwenyewe Uraisi!

    Sasa wandugu hapo mtaweza vipi hadi kuchomoka gerezani mdai ninyi ni Watanzania mrudishwe kwenu?

    ReplyDelete
  19. Wandugu biashara ya Utumwa ya Ukimbizi imepitwa na wakati rudini nyumbani mnatutia aibu huko!!!!!

    ReplyDelete
  20. Dunia imefilisika, Markani na Ulaya hasa Ugiriki,,,,huku watu wengi huko wanaishi kwa msaada wa Serikali, sasa hapo je?...jamani rudini nyumbani Tanzania mje kulima!

    ReplyDelete
  21. ha ha ha ha! teh teh teh! mshikaji wa 1 kuna mtu kakuchukulia mke wako nini ugiriki? kwani hapa issue nikopa yupo gr kawafurahisha watu na sio mambo ya uchumi.ww hutakuwa unachuki binafsi kwani kila mtu ana malengo yke ya maisha so uwezi kumfundisha cha kufanya. jivunie utanzania sio unatamba na nchi za watu. tukutane bongo tuone ww umevuna nini huko unapojivunia a mimi wa wa gr nina nini?nb hata ukiwa unaishi somali kama una malengo yako utashinda tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...