Mamia ya Watanzania kutoka katika pande tofauti nchini Ujerumani, walikusanyika jijini Berlin, kwa lengo la kufurahi pamoja kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika ambayo sasa ni Tanzania Bara.
Hafla hiyo iliyofanyika kwa namna tatu tofauti, ilianza kwa uzinduzi wa Umoja wa Watanzania Ijumaa, ikiwa siku ya kilele, siku hiyo ilibatizwa jina la usiku wa kidiplomasia ambapo mabalozi wa Afrika nchini Ujerumani walijivinjari katika sherehe ya jioni iliyoandaliwa na ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani.
Hafla hiyo ya kidemokrasi ilivunja hata protokali ya aina hiyo ya watu pale ambapo walijikuta katika kizimba cha burudani wakisakata rhumba lililokuwa likiporomoshwa na Ngoma Afrika Bend AKA F.F.U chini ya usimamizi wa kamanda Ras Makunja.
Jumamosi mchana ikiwa siku za mdahalo ambapo washiriki walijadili kwa kina namna ya kusaidia wenzao huko nyumbani, si kisiasa bali kwa vitendo katika nyanja mbalimbali za maendelea zikiwemo za kielimu na kiafya.
Kama vile haitoshi, usiku wa kuamkia jumapili watoto wa mitaa ya Berlin,Augsburg, Bonn, Munich, Cologne, Essen, Frankfurt na kwengineko walisema watajiachia siku za jumamosi, pale ambapo pamoja na Ngoma Afrika kurusha walimwengu hao Taarab, Bongo, Flava na muziki mwingine ulipata nafasi.
Pia alikuwepo mwanamuziki mkongwe Afrika mashariki ambaye makazi yake kwa sasa ni hapa ujerumani Tabia Mwanjelwa alikonga nyoyo za mashabiki kwa muziki wa dansi.
Hakika Ulaya wacha iitwe ulaya watu walipendeza, ni usiku wa baridi lakini viguo vilivaliwa kina kaka na kina dada, kina mama na watoto ili mradi tu kila mtu alikonga moyo wake.
Wadau Mbali Mbali walijumuika katika hafla hiyo
Ras Makunja nae ndani na bendi yake.
Burudani mtindo mmoja.
Kila mtu alikuwa ni mwenye furaha siku hiyo wakati burudani za hapa na pale zikiendelea.


Kuadhimisha Uhuru wa Tanganyika ni kwa kucheza muziki? Mbona tuna mambo mengi ya kufanya bado.
ReplyDeleteSASA WEWE ULITAKA IWEJE TULIE?
ReplyDeletemDAU dENMARK
Hata sijui mnachosherekea
ReplyDeletehuwezi jua maana huna uzalendo na nchi yako
ReplyDeleteUhuru Tanzania sherehe Berlin, kaa wabongo noma
ReplyDeleteKinacho sherekewa kipo ni miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bara,kwani kuna nchi nyingi za kiafrika kabla ya miaka 50 ya uhuru wao wamejikuta hawana amani,vita na mauaji na kumwagika kwa damu ndiko kulikotawala ,lakini watanzania tuna amani kubwa na demokrasia,lazima tusherekee miaka 50 ya uhuru
ReplyDelete