Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA,Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na wahitimu wa Mahafali ya Saba ya Chuo hicho (hawapo pichani) kabla ya kuwatunuku shahada zao katika mahafali hayo yaliyofanyika leo Viwanja vya Chuoni hapo Vuga Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,pia Mkuu wa Chuo kikuu cha Taifa SUZA Dk Ali Mohamed Shein,akimtunuku Shahada ya heshima ya chuo kikuu cha Taifa cha SUZA Rais Mstaafu wa Zanzibar Dr Amani Abeid Karume,wakati wa mahafali ya 7 yaliyofanyika katika viwanja vya chuo Mnazi mmoja Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,pia Mkuu wa Chuo kikuu cha Taifa SUZA Dk Ali Mohamed Shein,akimkabidhi zawadi Said Salim Bakhresa,kwa mchango wakemkubwa kukisaidia Chuo,wakati wa mahafali ya 7 yaliyofanyika katika viwanja vya chuo Mnazi mmoja Mjini Zanzibar.
Wajumbe wa Bodi ya Chuo cha SUZA,Simai Mohamed (kushoto)na Mfanya biashara maarufu Said Bakhresa na Dr Nariman Jidawi,walipompongeza kwa kupata zawadi kutokana na mchango wake mkubwa kwa SUZA,wakati wa mahafali ya 7 chuoni hapo.
Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA wakisubiri kutunukiwa Shahada zao na Mkuu wa Chuo hicho ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza La Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika Mahafali ya Saba ya Chuo hicho yaliyofanyika leo Viwanja vya Chuoni hapo Vuga Mjini Zanzibar.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza La Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wa katikati waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa SUZA pamoja na wahitimu wa Chuo ngazi ya Stashahada baada ya kuwatunuku Stashahada zao katika Mahafali ya Saba ya Chuo hicho yaliyofanyika leo Viwanja vya Chuoni hapo Vuga Mjini Zanzibar.picha na Ramadhan Othman IKULU ZANZIBAR.
Na Hamad Hija,
Maelezo zanzibar
Mkuu wa chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar Suza Dk Ali Mohd Sheni leo amewatunuku Marais wastaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wa awamu ya tano na ya sita Shahada ya heshima ya udakitari kutokana na mchango wao mkubwa walioutowa kwa masuala mbali mbali ya maendeleo hapa Zanzibar
Waliotunukiwa shahada hizo ni Rais mstaafu wa awamu ya tano Dk Salmin Amuor Juma Rais mstaafu wa awamu ya sita Dk Aman Abeid Karume ambapo shughuli hiyo ilifanyika katika viwanja vya kampasi ya chuo kikuu cha Vuga mjini Zanzibar shugghuli hiyo ya kutunuku shahada hizo ilienda na mafahali ya saba ya chuo hichosamba mba
DkSalmin Amuor Juma ambaye alitukukiwa shahada hiyo ya udakitari wa heshima bila kuwepo katika tukio hilo ambalo lilifanyika leo samba mba na utowaji mwengine wav yeti na shahada mbali mbali kwa wahitimu mbali mbali wa fani mbali katika mahafali ya saba ya chuo hicho
Mbali na kazi hiyo ya kutunuku shahada hizo kwa viongozi wastaafu walioitumikia nchi yetu kwa mafanikio makubwa pia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi DkAli Mohd Sheni alikabidhi vyeti ,Stashahada na shahada kwa wanafunzi 327 wa fani mbali mbali ambao wamehitimu chuoni hapo
Kwa upande wa wa hitimu hao waliotunukiwa shahada ya kwanza ya sayansi na elimu walikuwa wahitimu 63 ambapo kwa upande wa wahitimu katika fani ya Diploma ya sanaa na elimu walikuwa wahitimu wapatao82
Aidha Mkuu wa chuo hicho cha Suza na Rais wa Zanzibar katika mahafali hayo ya saba ya chuo hicho Rais aliwatunuku shahada ya kwanza ya sayansi na computer wahitimu 11 wakati wahitimu 14 wa fani ya komputer walItunukiwa cheti kwa kuhitimu masomo hayo.
Katika shughuli hiyo ambayo ilihudhuriwa na wananchi mbali mbali na baadhi ya mawaziri wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi ambaye pia ni mkuu wa chuo hicho cha Suza aliwatunuku shahada ya kwanza wahitimu 139 fani ya Elimu na sanaa ambao nao wamemaliza masomo yao
Baada ya kumaliza kazi ya kutunuku vyeti na shahada na stashahda Mkuu wa chuo hicho Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein alisema kuwa kuongezeka kwa vyuo vikuu hapa Zanzibar hiyo ndio dalili moja ya maendeleo ya nchi hii
Aidha alisema halitakuwa jambo la ajabu kwa siku za baadaye kuongeza na chuo chengine alisema tuna fanya hivyo kwa kuwa mahitaji ya kuwa na chuo chengine yapo
Akizungumzia suala la kukikuza Kiswahili alisema zanzibar ni moja ya sehemu ambayo inasema Kiswahili sanifu lakini ameseshangazwa na tabia iliyojengekaya kuwa katika mikutano yenyewatu kidogo wasiozungumza lugha ya Kiswahili tunalazimika kungumza kingereza amesema kuwa katika hali kama hiyo ni vyema tukazungumza lugha yetuwenyewe na wale ambao hawajuwi tukafikishia ujumbe tu





yaani chai jaba nae apata honorus
ReplyDelete