Mkuu wa Mkoa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu (katikati) akifungua kikao cha kamati ua ushauri ya mkoa huo mjini Songea hivi karibuni.Kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa huo,Dkt. Anslem Tarimo na Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Songea,Mh.Thomas Sabaya
Katibu Tawala wa wilaya ya Namtumbo,Bw. Ndaki Stephano (kushoto),akipokea moja ya mipira 100 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mantra Tanzania Ltd,Asa Mwaipopo mjini Namtumbo ilioyotolewa na kampuni hiyo kwa lengo la kukuza vibaji mashuleni.
Afisa ardhi,maliasili na mazingira wa halmashauri ya wilaya ya namtumbo,Kiyungi Kiyungi akikosoa mpango wa wizara ya maliasili na utalii kuzuia ujenzi wa barabara ya kutoka kijiji cha Likuyuseko wilayani humo kwenda katika mto mkuju ambako kuna hazina kubwa ya madini ya urani
Wajumbe wa Kamati ya ushauri ya Mkoa wa Ruvuma,kutoka wilaya ya Namtumbo wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo,Mh. Said Mwambungu (hayupo pichani) wakati wa kikao hicho ambapo pamoja na mambo mengine walijadiliana namna ya kupata fedha kwa ajili ya kuwalipa wakulima wa mahindi ambao wanaidai serikali zaidi ya tshs 10 bl baada ya kuuza tani ya 24 000 za mahindi kwa serikali kupitia wakala wa hifadhi ya chakula taifa kituo cha songea.
Mfanyabiashara maarufu mjini Songea,Jotam Mbilinyi (kulia) akicheza muziki na mfanyabiashara mwenzie Zakaria Sanga, wakati wa hafla fupi ya watumishi wa kampuni ya sigara mkoani Ruvuma na mawakala wao katika ukumbi wa Hertage cortage manispaa ya Songea
akina dada ambao hawakufahamika majina yao mara moja wakicheza muziki katika ukumbi wa polisi jamii,maarufu kama PJ Manispaa ya songea hivi karibuni,ukumbi huo ni maarufu sana mkoani Ruvuma baada ya kufanyiwa matengenezo makubwa na unauwezo wa kuchukua watu zaidi ya 800 kwa wakati mmoja.
Wakala wa kampuni ya sigara mkoani Ruvuma Bw Emanuel Kondoe kulia akicheza muziki sambamba na mtumishi wa kampuni hiyo ambaye hakufahamika jina lake mara moja wakati wa chakula cha jioni kati wa watumishi wa kampuni ya sigara na mawakala wao.
Jengo jipya la halmashauri ya wilaya ya namtumbo mkoani Ruvuma ambalo linaendelea kujengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya kiofisi,ndilo linaloongoza kwa ubora kuliko majengo yote ya serikali mkoani humo,na kuwavutia wageni wengi wanaofika kufanya shughuli mbalimbali.Picha na Muhidini Amri wa Globu ya Jamii,Ruvuma.










Naomba mlitembelee jengo hili baada ya mia miwili tangu kufunguliwa!
ReplyDeleteTunashukuru kaka Michuzi kwa kutuwekea picha za Songea kwa ni muda mrefu hatujui kinachoendelea mkoani kwetu.Naomba tuwekee mara kwa mara matukio ya Ruvuma.Thanx
ReplyDeleteNa hilo dongo jekundu, si tuone baada tu ya miezi 7
ReplyDeleteWeka la la Kilolo ambako ndiko ramani hii ilichukuliwa
ReplyDeleteJengo zuri sana lakini vipi hapo nje parking lot?hayo mavumbi na madongo mekundu wangeyafunika basi hata na kokoto na bustani ya majani kama hawana uwezo wa kuweka lami au concrete,wasipofanya hivyo hilo jengo litakuwa chafu kama manzese,na vipi hao wanaume wawili wanacheza pamoja..hakuna ubaya lakini kwa wenzetu wanaweza fikiri ni couple hao.
ReplyDeleteHuo udongo mwekundu na rangi nyeupe haviendani kabisa. Wangechagua rangi nyingine la sivyo jengo lote litabadilika rangi baada ya miezi michache.
ReplyDeleteHalafu jengo lenyewe limekopa baadhi ya fedha za kilimo kwanza kinyemela, sijui zimesharudishwa?
ReplyDeleteWadau, imekuwa ni utamaduni wetu kutokuhudumia vitu baada ya kukamilika, unakuta nyumba inajengwa kwa mabilioni ya shilingi halafu halifanyiwi usimamizi makini wala kuhudumiwa kwa usafi.
ReplyDeleteSasa basi hata kama ujenzi umeshafanyika kulihudumia jengo ni muhimu na sio kuwa kama Jumba la makumbuhso ya Historia!