Na Dixon Busagaga
CHAMA Cha waandishi wa habari mkoa wa Kilimanjaro (MECKI) leo kinakutana na marafiki wa habari pamoja na wadau mbalimbali katika mkutano utakao fanyika ukumbi wa Umoja Hostel kujadili changamoto mbalimbali zinazohusu pande zote mbili.
Akizungumza na wandishi wa habari ,kaimu katibu mkuu wa MECKI,Nakajumo James alisema mkutano huo unafanyika kwa mara ya kwanza tokea uongozi mpya uingie madarakani mapema mwaka huu na mgeni rasmi ni mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama ,
“Mkutano huu wa kwanza kwa MECKI inaratibiwa na chama chetu ,una lenga kuwakutanisha wadau na marafiki wote wa habari mkoani Kilimanjaro kwa lengo la kubadilishana mawazo na kupeana changamoto mbalimbali”alisema James..
Alisema pia mkutano huo unalenga kuboresha mahusiano ya kikazi hususani tunapoelekea kwenda kuanza mwaka mpya wa 2012 pamoja na kutafuta njia bora zaidi ya kujenga misingi imara ya kufanya kazi kati ya wadau na waandishi wa habari.
“Kupitia mkutano huu tutaweza kutambua mchango wa wadau katika tasnia ya habari na jinsi gani tutaweza kukabiliana na changamoto zinazowakabili waandishi na wadau wa habari katika tasnia yetu hii”alisema James.
Mkutano huo utakao anza majira ya saa 4:00 asubuhi utaenda sanjari na zoezi la utolewaji wa vyeti kwa wadau mbalimbali na waandishi wa habari walioshiriki kutoa taarifa za klabu wakati wa kongamano la wadau wa Kahawa lililofanyika mwanzi mwa mwaka huu.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...