Mbunge wa jimbo la Namtumbo Ruvuma Mh. Vita Kawawa akiongea mjini Namtumbo wakati wa mkutano wake na wananchi wa kata ya Namtumbo mjini wenye lengo la kutafuta suluhisho la kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa kata hiyo. Kulia ni diwani wa kata hiyo Bw. Alpius Mchucha,na kushoto ni mwenyekiti wa serikali ya mtaa Bw. Bakari Kayuni
Mkazi wa kata ya namtumbo mjini Bw Athuman Kombo akihoji juu ya kitendo cha mamlaka ya maji wilayani Namtumbo kuongeza gharama za huduma ya maji licha ya wananchi wa kata hiyo kukabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya ccm wilayani humo,ambao ulihudhuriwa pia na mbunge wa jimbo ilo Mh. Vita Kawawa
Diwani wa kata ya Namtumbo mjini Bw. Alpius Mchucha,akifafanua mambo mbalimbali jana kwa wananchi wa kata hiyo katika mkutano wa hadhara kati ya mbunge wa jimbo hilo Mh. Vita Kawawa aliyekaa katikati na wananchi wa kata hiyo
Diwani wa kata ya namtumbo mjini Alpius Mchucha kushoto na katibu wa afya wa wilaya ya Namtumbo Bw. Lucas Nela (katikati) wakijadiliana jambo na mbunge wa jimbo la Namtumbo Vita Mh. Kawawa baada ya kumaliza mkutano wa hadhara uliofanyika juzi wilayani humo.
Picha na Muhidin Amri wa Globu ya Jamii, Songea
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...