Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini ( TANROADS )Mhandisi Patrick Mfugale (kushoto) pamoja na Meneja Mkazi wa Kampuni ya Mkandarasi M/S STRABAG INTERNATIONAL GmbH ya Ujerumani Heribert Schippers (kulia) wakitiliana saini mkataba wa Ujenzi wa Miundombinu ya Mfumo wa Usafiri Haraka wa Mabasi jijini Dar es Salaam Awamu ya kwanza, Kandarasi wa Kwanza (Barabara) Nov.22.2011 katika makao Makuu ya Wizara ya Ujenzi,. Mradi huo wa Ujenzi unafadhiliwa kwa mkopo wa Benki ya Dunia ambapo mradi mzima wa kazi utagaharimu shilingi 240.9 Bilioni. Ujenzi wa awamu ya kwanza unahusisha ujenzi wa barabara unaofikia kilometa20.9 katika barabara ya Morogoro(kutoka Kimara hadi Kivukoni (Feri), barabara ya Kawawa (kutoka) Magomeni hadi Morocco ) na barabara ya Msimbazi (kutoka Fire hadi makutano ya Nyerere -KAMATA). Hafla hiyo imehudhuriwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli , Viongozi wa TAMISEMI, Wizara ya Fedha na wadau mbalimbali wa sekta ya Ujenzi
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini ( TANROADS )Mhandisi Patrick Mfugale (kushoto) pamoja na Meneja Mkazi wa Kampuni ya Mkandarasi M/S STRABAG INTERNATIONAL GmbH ya Ujerumani Heribert Schippers (kulia) wakibadilishana hati za mkataba wa Ujenzi wa Miundombinu ya Mfumo wa Usafiri Haraka wa Mabasi jijini Dar es Salaam Awamu ya kwanza, Kandarasi wa Kwanza (Barabara) Nov.22.2011 katika makao Makuu ya Wizara ya Ujenzi,. Mradi huo wa Ujenzi unafadhiliwa kwa mkopo wa Benki ya Dunia ambapo mradi mzima wa kazi utagaharimu shilingi 240.9 Bilioni. Ujenzi wa awamu ya kwanza unahusisha ujenzi wa barabara unaofikia kilometa20.9 katika barabara ya Morogoro(kutoka Kimara hadi Kivukoni (Feri), barabara ya Kawawa (kutoka) Magomeni hadi Morocco ) na barabara ya Msimbazi (kutoka Fire hadi makutano ya Nyerere -KAMATA). Hafla hiyo imehudhuriwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli , Viongozi wa TAMISEMI, Wizara ya Fedha na wadau mbalimbali wa sekta ya Ujenzi.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akionyesha baadhi ya ramani yenye michoro ya barabara za juu (Flying- Over) zitakazojengwa jijini Dar es Salaam. mbele ya waandishi wa habari na Wadau wa sekta ua Ujenzi leo, wakati ya hafla ya uwekaji wa sahihi ya Mradi wa ujenzi wa miundombini ya mfumo wa Usafiri haraka wa mabasi jijini Dre salaam-awa. mu ya kwanza, Kandarasi ya kwanza (barabara), utakapo kamilika ujenzi wa barabara hizo itasaidia kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es Salam, ambapo ndio lengo kubwa la serikali. (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
DART ,,,,huu muujiza wa Nabii Mussa (Mradi usiotekelezeka wa KINADHARIA )bado ndio unasainiwa na upo ktk makabrasha tu?.
ReplyDeleteAh aisee ndio kwanza mifereji ya barabara ,viwanja vya wazi na madaraja yamejaa mafuriko!
Kwa maana ingine Mradi wa Mabasi Yaendayo kasi Dar ,Kwa miundo mbinu tuliyonayo ambayo ndiyo kwanza imeathiriwa vibaya na mvua kubwa na mafuriko, ni kama experiment ya Wahandisi wanafunzi Elimu ya Juu ambapo uwezekano wake ni sawasawa na inzi (mdudu) kuruka, kupenya ktk ndimi za moto na kutokea upande wa pili BILA KUFA!
ReplyDeleteMradi huu kwa kusua sua kwake kuanza, ni dalili tosha kuwa hautekelezeki ng'o!
ReplyDeleteDaktari, Profesa, Mhandisi au mwanaharakati yeyote mwenye akili iliyotulia atakae uwezesha mradi huu kwa hali tuliyo nayo ,atapata nishani ya Nobel mwaka ujao 2012!
ReplyDeleteHuyo atakae utoa mpango kiganjani hadi ardhini , du itabidi angalau tumpe Ubunge nae akale zake kidogo au apewe heko zake babake!
ReplyDeleteSasa Traffic lazima wawe wakali maana walevi wa bongo watapaa kwenye hizi fly-over na kutua upande mwininge. Jameni serikali lazima iweke sheria kali za bararani na kufata sheria na matraffic walipwe mishahara mizuri ili waache kuchukua hongo. Huku Majuu hata akiwa mtoto wa raisi kama kafanya kosa anapata ticket (fine) na analipa hapo bongo ukionyesha drivers licence na una yale majina ya viongozi wa bongo basi wewe umepona wala fine hupati na afande unampa chau chau. Mark what i said today kama sheria za barabarani hazitakazwa watanzania watazidi kufa barabarani kama kuku! You see what always happened ajali za kipuuzi mtu anaovertake kwenye kona au mlima. Mungu wabariki hawa investors.
ReplyDeletemsukamano wa magari mjini dar lazima utafutiwe utatatuzi wa kudumu,majengo yote mapya mjini yalazimishwe kuwa na parking area.Kama nyumba ya ghorofa kumi lazima iwe kuwa ghorofa mbili za mwanzo ziwe parking
ReplyDeleteRapid Bus Transit inaweza kuwa mkombozi wa msongamano barabarani. Kitu muhimu ni kuakikisha wanaanzisha congestion pricing kupunguza watu kuendesha magari binafsi. Uanzishaji wa Park and Rides katika maeneo tofauti jijini utasaidia kupunguza magari barabarani.
ReplyDeleteNjia nyingine ni kushirikisha makampuni kutoa incentives kwa wafanyakazi wanaotumia usafiri wa umma.
Development of tier cities around Dar-es-salaam with job creating industries will reduce number of people commuting between suburbs and city center.
Kuna msemo hapa Marekani unaosema "You can't build your way out of congestion." Construction za fly overs mara nyingi unaongeza magari barabarani.
Wizara ya ujenzi haiwezi kufanya kazi kama independent entity bila kushirikisha City planners.City planners wanaweza kuallocate maeneo ya park & ride,kutoa projection ya mji unavyokua kusudi kupanga ujenzi au upanuzi wa barabara katika maeneo yote jijini.Cha kushangaza ukienda kwenye office za jiji uwezi kuona future throughfare plan ya jiji.
Pongezi kwa wizara ya ujenzi/Magufuli kujaribu kutatua msongamano.
Mdau-USA
zijengwe treni za chini ya ardhi(subway).mji umejaa mno.magari,machinga daladala .nk.
ReplyDeleteHizo plans za fly-overs na mabasi yaendayo kasi zimezingatiwa kutumika kiufanisi na kwa kutosheleza kwa idadi gani ya watu Tanzania na kwa miaka mingapi ijayo?
ReplyDeleteserikali inadaiwa na Tanesco bilioni 300,halafu serikali hiyo hiyo inakopa zingine bilioni 240 kwa ajili ya msongamano,kwa haraka haraka serikali yetu haina fedha hata za kununua kuku wa kienyeji kwa ajili ya wageni wetu.Hapo hapo inawapandishia posho wabunge kwa asilimia 150 ili wazidi kuinyonga TZ.Tanzania tunaelekea kubaya kama siyo nchi kununuliwa na wachache.Mimi binafsi namlaumu Mwenyezi Mungu kwa kumchukua Kipenzi cha Watanzania Mwl.Nyerere.Angalau angekemea upuuzi unaofanywa na viongozi wetu.
ReplyDeleteTumewasikia,,,tumewaelewa! Acheni tuanze then mengine yatafuata. Kila jambo kuna mahali huanzia, nasi tunaanzia hapa. Hizo mnazoziona huko mliko nazo zilianzia mahali,,,hii ni hatua ya maendeleo tu wasomi wenzangu...utazaliwa, utatambaa, utatembea, utakimbia...Go...Magufuli...go! Mdau, Canada!
ReplyDeleteinatakiwa kutumia pesa kuongeza quality za barabara za mikoani kwani barabara zenye lane moja na ni kunatokea ajari nyingi sana huko
ReplyDeleteKwanini wizara zote ziko Daslam?hata wizara ya Kilimo ,Dar wanalima nini ??------kuna ulazima wa kufanya decentralization kama tunataka kupunguza foleni Dar,angalau Magufuli anajitahidi kuja na practical solutions ,hongera kwa hili,ila hii ni sio jawabu kamili kama tunaona mbele miaka 50 ijayo............!
ReplyDeleteMradi wa DART dhana yake ni ya kufikirika tu!, kama ilivyokuwa Mnyama MBWA au CHUI MWENYE MIGUU NANE (8)aliyekuwa na NDIMI ZA MIALE YA MOTO na AKITEMA CHECHE MDOMONI ambaye alitumika kuiwakilisha kampuni ya mafuta ya zamani AGIP...!
ReplyDeleteatakae iwezesha DART kwa ufanisi wetu ulio chini ya kiwango kutokana na ufisadi,,,walahi Asalama leko zake kweli!
ReplyDeleteMdau wa 14 hapo juu naungana nawe...Kwanini wizara zote ziko Daslam?hata wizara ya kilimo,Dar wanalima nini??------kuna ulazima wakufanya decentralization
ReplyDeleteKuna Idara moja katika Wizara ya Kilimo hua inaniacha hoi sana!
Ukienda pale Pamba House Mtaa wa Azikiwe na Garden kwenye kona utaona bango limeandikwa WIZARA YA KILIMO/ IDARA YA KILIMO CHA KISASA!
Hivi jamani Kilimo cha kisasa ndani ya Daslamu wapi na wapi?
Ndio kilimo cha Kimjini mjini cha mambo ya Usanii au nini?, maana wazee wetu wa mijini Wasanii wanajiita Wakulima wa Mujini!
Kwa nini angalau Idara hiyo isiwepo huko Dakawa, Mbarali, Kilombero, Rukwa ,Mabuki Geita na Sengerema ambako kilimo cha kisasa kinafanyika?
Subirini tu barabara iishe, mtaona jinsi wabongo walivyokuwa hawana akili nzuri. Hapa taa zitang'olewa, watu watakunya hovyo hovyo ili mradi tu kuwanyea wanaopita kwa miguu chini ama magari yapitayo chini. Kina mama ntilie watakuwa wanaosha vyombo hapo wakitoka feri/kivukoni, yaani hii itakuwa haibu tupu kama vile uwanja mpya wa taifa. Si mnakumbuka jinsi uwanja wa taifa ulivyokuwa unan'golewa vyoo na watu kukojoa kila sehemu kwa makusudi, hii itarudi subirini tu.
ReplyDelete