Home
Unlabelled
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam akihojiwa na TBC1 juu ya Mafuriko usiku huu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
haya kufuata sheria huko unaenda Ardhi ndiyo huko huko wanakuba kibali feki au watu zaidi ya mmoja kibali kimoja.serikali inabidi ijisafishe yenyewe na watumishi wake, wananchi wanategemea sana serikali na ofisi zake kupata taarifa za kweli,kwa nchi yetu ni tofauti.taarifa ofisi nyingi ni siri ili watu wapate rushwa.Cha Muhimu ni kwa serikali kuwa na utaratibu wa kutangaza au kubandika taarifa kwenye ofisi zao ili watu wasome.
ReplyDeleteMichuzi umepooza sana kwenye salamu zako za xmas na mwaka mpya alafu kwikwi nyingi. Tuma nyingine Uncle please mi sijaipenda hii.Tena jitahidi kabla waosha vinywa hawajarudi kutoka nightshift.
ReplyDeleteJamani Jamani Jamani!!
ReplyDeleteHivi, Hizi Mvua Hazijaharibu Ikulu?? (State House)
Jamani Tunaomba Mapicha ya State House Kama Kuna Mafuriko!!
Pole sana Watu Wetu! Mungu Ibariki Tanzania.
Hivi Mkuu wa Mkoa anashindwa kufahamu kuwa serikali inaundwa vile vile na wanasiasa? Sasa anaposema wanasiasa wanabidi kuzungumza na serikali anamaanisha nini?
ReplyDeleteMafuriko ni ''Natural Disaster'' janga la asili, pasipatikane wa kulaumiwa isipokuwa suala la tahadhari kabla ya tukio ndio suala la mjadala (mfano walivyoshauriwa wakazi wa mabondeni kabla juu ya kuhama) na nini,uharakishaji na jinsi hatua ya dharura kuchukuliwa baada ya janga.
ReplyDeleteMoyo wangu unawaendea wale wote walioathirika na haya mafuriko. Lakini kusema ukweli pamoja na kwamba sipendi siasa nakubaliana na mkuu wa mkoa kwamba watu ni wabishi pale wanaposhauriwa kuwa wahame mabondeni pale walipojenga kiharamu... kama alivyosema "jeuri isiyo na tija" sasa wewe unaona hatari alafu unaingia kichwa kichwa?.. all in all tumuombe mungu awanusuru ndugu zetu, na serikari ifanye kazi na wananchi wake kuwawasaidia katika kipindi hiki
ReplyDeleteYaani huyu mkuu wa mkoa haja panda Helokopta kuangalia maafa anasimuliwa na jeshi la polisi
ReplyDeleteTumethubutu, Tumeweza tunasonga mbele na Mafuriko yetu. Tanzania Oyeeeeeeeeeeeeeeee
ReplyDeleteZile hela za maonyesho zingetumika kuliweka jiji katika hali nzuri haya yote yasingetokea
ndugu zangu watanzania ifikie wakati sasa tuwe wakweli swala la mabondeni mnataka nani awasaidie kuliko nyie wenyewe?hao wanasiasa wanao watetea hata wenyewe wakiingia madarakani hawatakuwa na msaada kwenu hilo lazima mulielewe nduguzangu kwanini tudanganywe?ifikie wakati na vichwa vyetu fipewe fikra na mungu jamani tusiyumbishwe mbona mambo yapo wazi?
ReplyDeletewatu sio wabishi hawana alternative. bibi aliyeachiwa wajukuu wa kutosha na marehemu watoto wake au hata kijana mwenye watoto zaidi ya watano, hana kazi anategemea vibarua, atahamia wapi? nyumba aliyoridhi ndio iko bondeni atahamaje? Watu wengi wanaoishi kule ni masikini kwelikweli
ReplyDeleteHuu ukweli wa mkuu wa mkoa hautasaidia lolote. kuna wanaoamini kuwa nchi itajengwa kwa lawama tu!
ReplyDeleteMkuu nimekufahamu sana tu japokuwa sijafahamu kwanini serikali haijachukua hatua ya kusimamisha pale watu wanapoanza ujenzi wao.Ina maana hakuna watu maalum wenyekuangalia sehemu zinazotakiwa kuwa wazi.Mvua hizi ni mvua zinazokuja na maafa ambazo hakuna mtu anaeweza kuzuia ila kwa ushauri wangu nawaomba muwape viwanja sehemu ambazo zinafaa kujenga nyumba za kuishi na muwape onyo mtu asirudi huko maana hawa watu sio kama hawajui sehemu ni hatari ila ni kukimbilia kuishi mjini ndio tatizo..Najua serikali haitokuwa na uwezo wa kuwajengea nyumba japo za bei ya chini lakini angalau wapewe viwanja vya kujijengea makazi yao.
ReplyDelete