Ankali taswira hii ilichukuliwa tarehe 24 October 2001 inaonyesha ile kona kali pale Mlima Sekenke Mkoani Singida, hapa ni mahali ambapo wote waliobahatika kupita enzi hizo nadhani wanalikumbuka sekeseke lake, Wakati wa masika ni tope Magari yanakwama kupanda na kushuka, Wakati wa kiangazi ni Dimbwi la vumbi magari kupanda ni kasheshe.Lakini sasa hivi ni Lami na nasikia njia imechepushwa haikupita hapo, hebu wapeperushie wadau wakumbuke enzi hizo.
Mdau Ughaibuni



hhaha nimefurahi sana nAkumbuka enzi zile zangu za safari.SENKEKE ILIKUWA INASHINDANA NA CHIWETA.WE ACHA TU MADEREVA WA MAGARI MAKUBWA WALIKUWA WAKISHINDANA HUYU AKISEMA SENKENKE NI NOMA MWINGINE AKANUSHA ASEMA HAKUNA WEE KITU CHIWETA.CHIWETA IPO NJIA MALAWI KWA WALE MADEREVA WA MAGARI MAKUBWA NADHANI WANAIFAHAMU VILIVYO HII SEHEMU.
ReplyDeleteUko wapi?
ReplyDelete