Brother Michuzi

Naomba unitolee tangazo langu kwa wanawake (wa umri wo wote) ambao wanahitaji kuwa kwenye ndoa, lakini wanasita, au wanashindwa eti kwa kudhania kuwa wapo kwenye disadvantage kwa ajili ya kutokuwa na hisia za kufanyia mapenzi (lack of sex drive) au waliokuwa na hisia zilizo chache.

Mimi nina miaka 51, dini yangu ni muislam na naishi Dar Salaam pia na Uk. Sivuti sigara wala sinywi na pia sina mali, ila ni mchapakazi tu. Mimi ni mpole, mkarimu mpenda jokes na la muhimu napenda sana kusikiliza dini.

Kama kuna yoyote ambae yupo serious awasiliane nami kwa Email yangu abdjay51@yahoo.co.uk.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 41 mpaka sasa

  1. WEKA PICHA BASI

    ReplyDelete
  2. Mimi nina miaka 45 ni mwanamke wa kiislamu, nimetulia, ninaifuata mafundisho ya dini vizuri na ninapenda pia kujifunza dini na nimeshamali kuzaa pia sina hali wala mali je utanikubali?

    Swali la pili je ukaazi wako ni wapi Bpngo au huko UK? Na kama ni huko UK je una makaratasi? Maana isijekuwa baada ya ndoa unanijia na story kuwa inabidi uoe mwanamke mwingine kwa ajili ya makaratasi halafu mimi nakuwa sina status iliyoeleweka!

    ReplyDelete
  3. WEWE KAKA MTAFUTA WACHUMBA NAONA UNA KASORO! WEWE UNAWEZA KUWA UNAKAA UK UKAKOSA MWANAMKE WA KUOA BONGO? WAKO LUKUKI LWA WANAWAKE NAONA KIDOGOMMUSHKERI?

    SEMA TATIZO LAKO ILI LITATULIWE

    mDAU LONDON

    big JAY

    ReplyDelete
  4. ningejitosa sex drive yangu ndogo,ila huo umri hapana mwenzangu usije ukanifia kifuani buree....lol

    ReplyDelete
  5. Jibu la kwanza nasema kuwa kwa sasa nipo Uk. Makaratasi ninayo, picha utaiona na hata mimi mwenyewe utaniona. Wewe niandikie Email kwa anuani yangu (abdjay51@yahoo.co.uk) tutaongea zaidi.
    -------------------------------
    Mdau wa London, Big Jay, nakujibu hivi, 'Kweli mushkeri upo. Na mushkeri wangu mkubwa hasa ni kwenu nyie wanawake wa Uk. Imekuwa kama mmetiwa upupu tumboni. Sijui ni vyakula vya 'Value' vya Tesco mnavyokula? Nyie uzungu wenu mliojifunza ni kusema 'Yes' tu, 'no' hamjajifunza. Mimi sitafuti waruka njia natafuta mke. If you think you don't approve my way you can always shut your gob, thank you.

    ReplyDelete
  6. ngoja upate pesa za kutosha. wanawake wanataka mtu mwenye pesa

    ReplyDelete
  7. ACHA LONGO LONGO, WE SEMA UNA SHILINGI NGAPI.

    Miss Madinda

    ReplyDelete
  8. mie ni mwanamke mwenye miaka 39 sina kazi na ninawatoto ila sitaki kuolewa na masharobalo wanaojiuza humu kwa issa michuzi, nikitaka mme niampata msikitini na si kwenye ma blog. upo hapo sharobalo??

    ReplyDelete
  9. mie ni mwanamke mwenye miaka 39 sina kazi na ninawatoto ila sitaki kuolewa na masharobalo wanaojiuza humu kwa issa michuzi, nikitaka mme niampata msikitini na si kwenye ma blog. upo hapo sharobalo??

    ReplyDelete
  10. mie ni mwanamke mwenye miaka 39 sina kazi na ninawatoto ila sitaki kuolewa na masharobalo wanaojiuza humu kwa issa michuzi, nikitaka mme niampata msikitini na si kwenye ma blog. upo hapo sharobalo??

    ReplyDelete
  11. mie ni mwanamke mwenye miaka 39 sina kazi na ninawatoto ila sitaki kuolewa na masharobalo wanaojiuza humu kwa issa michuzi, nikitaka mme niampata msikitini na si kwenye ma blog. upo hapo sharobalo??

    ReplyDelete
  12. Assalam Alaykum!

    Mtoa maoni wa 2 ,Bibie Hajjat Awlaa mwenye umri wa Miaka 45 nafikiri wewe utakuwa chaguo sahihi la Ustaadh huyo mwenye umri wa miaka 51 anayeishi TZ na UK pia.

    Mtoa maoni wa 3 mDAU LONDON
    big JAY

    Tafadhali wacha tabia ya kujenga dhana pasipo na uhakika, ndio hata kama na wewe upo huko London UK alipo pia Mdau wa miaka 51 anayetafuta Mwanamke usishangae kwa nini anakosa mwanamke wa kuoa hadi sasa!

    ZINGATIA MAMBO HAYA MUHIMU:

    1.Kwa Dunia ya sasa wengi wa waolewaji na waoaji wapo ktk mtihani mzito kwa vile waoaji wengi ni Makachala na waolewaji ni Micharuko!,,,sasa kumpata mtu sahihi inakuwa ni suala lisilokuwa rahisi kama unavyofikiri.

    Mfano ndoa nyingi na mahusiano mengi ni ya kimaslahi saana zaidi ya azma sahihi ya ndoa!, na ndio maana watu wanatafutana kwa hali na hali, wakati huo huo mahusiano ya kawaida na ndoa zinakuwa hazidumu kwa msingi huo huo.

    2.Elewa kuwa ndoa au kumpata mwenza wa kweli inapangwa na Mwenyezi mungu, na sio kwa uratibu wa binaadamu wachache lichaya kuwa jitihada zako na nia binafsi ndio vinakupa mwenza wako!

    Sasa unakuta ktk jamii zetu watu hawazingatii hayo mawili MUHUMU HAPO JUU ,badala yeke watu wakiona mtu anachelewa kuoa au kumpata mwenza wanajenga dhana potofu na mtazamo wa kibinaadam kama mDAU LONDON big JAY hapo juu kiasi cha kumwita Mdau wa miaka 51 ana kasoro!

    Hii ni hatari sana mtu kuwa na dhana kwa mtindo huu!

    Yeye Mdau wa miaka 51 ni mtu kamili wala hana matatizo yoyote na kwa dalili ya kumfuta mwenza ndio anathibitisha hilo!

    ReplyDelete
  13. Haya maendeleo yenu ya mitandao siku hizi! Mnatafuta wachumba kwenye mitandao!! Angalia msijepata wake majini kupitia mitandaoni. Yaani umekosa kabisa nafasi ya kumpata mchumba kwa macho yako mwenyewe? Au kama wasemavyo wengine, kuna kasoro unaficha? Kama ndivyo, ni bora utambulike mapema kuliko baadaye maana hakuna pendo la namna hiyo.

    Kuoa, mtu unaona, unapenda halafu unaamua kuchukua jumla. Siyo kuagizia kwenye mitandao kama bei ya kahawa.

    ReplyDelete
  14. My dear 51 yrz huna ndoa? Au ulshatalak? Mi ni mkiristo km utahiari tufunge ndoa ya kiserikali,nina miaka 37 nitafte kwa namba hii 0753014177 nina watoto watatu.

    ReplyDelete
  15. elezea historia yako vizuri maana miaka 51 ni mingi umewahi kuoa una watoto, nk.Toa profile yako yote

    ReplyDelete
  16. miaka 51 bado huna uzoefu wala fikra za kutafuta anayematch, pamoja na kufika kwako UK?

    Nakushauri uendelee kuwa single ila usizini. Maana ukiowa, talaka naona iko njiani. Kwani tangu umri wa 18 ulikuwa unasubiri nini?

    ReplyDelete
  17. kama unataka kizazi pia inabidi ukubali walio chini ya miaka 40, la sivyo, ukaribio wa menapozi unaweza kuleta mitoto mazezeta.

    kwa hiyo kwa wanawake wa umri huo, kaa tayari kuwatunza na kuwapa zawadi watulie.

    usisahau una 51 kwa hiyo hela za viagra ziwe karibu. La sivyo anza kuangalia vyakula vyenye afya hasa mboga na matunda, punguza dona , wali, na mikate.

    kama hutaki kizazi, utapata wazee wenzako wengi tu.

    ReplyDelete
  18. mimi ni mwanamke mweupe mrefu, mzuri sana mithili ya malkia nina miaka 32 ila dini yangu mkristo, kama unaniahidi kunipeleka UK niko tayari kubadilisha dini niwe muislam, kama tutaishi hapa Bongo sibadilishi dini. Niambie kama utaweza kunikubali kwa hali hiyo.

    Jibu kama unakubali.

    ReplyDelete
  19. Kweli hata mimi nahisi kuna shida fulani hadi mtu amefikisha miaka 51!!!! Au yaelekea mtu huyo alikuwa LIFST SAAAAAAAAAAAAN YAAANI MATANUZI KWA KWENDA MBELE!!!! Sasa ndo anakumbuka shuka asubuhi!!!

    ReplyDelete
  20. Sema matatizo yako usaidiwe wewe au gubu jingi nini?

    ReplyDelete
  21. Tehehehehe Kumbe Ukikaa UK ni sifa ya kupatia wanawake Bongo?! Nilikuwa sijui.

    Mdau HK

    ReplyDelete
  22. Hana lolote huyo, anatafuta kujua watu wana mitizamo gani kuhu ndoa.

    Mtu wa miaka 51 hajui kutafuta mchumba?? Au alikuwa hoi, na sasa baada ya kwenda Loliondo amepata uwezo!!

    Unajua, miaka hiyo ni mingi kulinganisha na ufahamu wa jinsi ya kupata mchumba. Rudi basi Bongo uje utafute mwenyewe mwenye kukufaa. Si unasikia wengine ni weupe, malaika haoni ndani! Sasa unaweza ukavutiwa na sifa au jinsi mtu anavyojieleza ukaingia mkenge.

    ReplyDelete
  23. na mimi niko dubai natafuta pia

    ReplyDelete
  24. umri huo si rahisi kuwa hujapita pita. kuna kaka yangu ana 52 ana watoto karibu 10 lakini hajawahi kuoa zaidi ya kuishi na wanawake tofauti. ni difficult person ingawa kama hujamzoea utasema mwanamume ndo huyo lakini ingia katika anga zake - kipigo nje nje na uongo mwingi kwa wasio mfahamu na kujipalilia tabia nzuri. Akiwa nazo kuhonga nje nje! watu type hii wanafaa part time tu!!! tatizo hamna binadamu anayeweza kuanika weakness zake mwenyewe!!!

    ReplyDelete
  25. HAKUNA USHAHIDI WA KISAYANSI UNAOTHIBITISHA YA KUWA KWA WATU WOTE UMRI MKUBWA KWA MWANAUME NI KIGEZO CHA KUKOSA NGUVU ZA KIUME!

    INATEGEMEA NA MAUMBILE, WAPO MABABU WANA ZAIDI YA MIKA 65 LAKINI WAPO FITI NA HAWATUMII VISAIDIZI VYOVYOTE KAMA VIAGRA.

    WAPO HUMU VIJIJINI MWETU AMBAPO HATA HIYO VIAGRA YENYEWE ,ACHA UWEZO WA KUIPATA WALA HAWAIFAHAMU KABISA!

    UWEZO WA NGUVU ZA KUME UNA MAZINGIRA MENGI SANA, ILA MAKUBWA NI MAWILI TU, NA KAMA WAPO WAGANGA WA NGUVU ZA KIUME HAO NI WATAFUTAJI TU:
    -----------------------------------
    VIGEZO VIKUU MUHIMU VYA KISAYANSI VYA NGUVU ZA KIUME
    -----------------------------------
    1.SAIKOLOJIA: UKIWA NA MSONGO WA MAWAZO AU HUPO MUSTAREHE HUWEZI KUWA NA HISIA ZA KUJAMIIANA.

    2.CHAKULA: ZIPO AINA ZA CHAKULA AMBAZO ZINATOA UWEZEKANO WA MTU KUWA NA NGUVU NA UWEZO WA KUTOSHA KWA KULIENDEA TENDO LA JAMII
    -----------------------------------
    MIFANO YA MABABU AMBAO WAMEKUWA WAMO INGAWA WAMEPITA UMRI WA MIAKA 65.

    1.Paul Wolfowitz-RAISI WA ZAMANI WA BENKI YA DUNIA.
    2.Dominique Strauss Kahn-MKUU WA ZAMANI WA (IMF)-SHIRIKA LA FEDHA LA KIMATAIFA
    3.Jacob Zuma-RAISI WA AFRIKA KUSINI
    4.Silvio Berlusconi-WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA ITALIA.

    Pia kipo kisa cha hapahapa Tanzania, jamaa mmoja alimwita Babu yake Umri miaka 78 kutoka Kijijini kuja Mjini kutembea, siku moja ktk hali asiyoamini jamaa alipata dharura akarudi ghafla nyumbani saa 4 asubuhi kutoka kazini akamkuta Babu yake juu ya kifua cha mkewe...EBO!

    SASA HAO MIAMBA NI KTK MABABU AMBAO SHUGHULI YAO IMEITWA BADO NI PEVU, NA KWA MSINGI WA SAIKOLOJIA ZAO KUWA JUU NA HURU WAMEDIRIKI KUBAKIA KUWA NA NGUVU ZA KUTOSHA KTK MASUALA YA KUJAMIINA ,SASA ITAKUWA MDAU WA UK MWENYE UMRI WA MIAKA 51 TU?

    ReplyDelete
  26. haya basi wengine ambao tuko serious tumekutumia email, tujibu basii

    ReplyDelete
  27. Mimi namtetea huku mtafuta mchumba. Watu wengi ambao waliofika UK kwa kutafuta maisha hiyo miaka yake ni sawa na hatakuwa na tattizo lolote. Hii inatokana na ugumu wa kupata makaratasi hapa UK kwa wazamiaji. Ili upate makaratasi UK inabidi uishi muda mrefu sana sio chini ya miaka 10. Sasa kama uliingia una miaka 30 mpaka ukapata makaratasi ndio 51 sahihi kabisa. Achana na watu waliojiingiza kwa usomali au highly skilled ambao wamepata makaratasi kirahisi. Sasa UK wameondoa hizo njia rahisi za makaratasi.

    ReplyDelete
  28. Huyu Bwanadetails zake ziko shallow, hatuwezi kumhukumu, huenda ana nia njema tu. lakini maelezo yake, ya profile, yangeweza kutoa mtazamo kidogo. kuona kuwa anahitaji kweli msaada (yaani yeye ahurumiwe, au mtu atakayemuoa ahurumiwe) huwezi jua Dunia hii.

    Ukweli kidogo!! kuna maswali mengi mtu atajiuliza. ni kweli hupendi wahuni, au ulikuwa umestaafu? sio vibaya ya umestaafu, ukimpata na aliyestaafu. nina imani mtaishi vizuri tu. nakushauri, usipate mtu ambaye anahitaji maisha. pata mtu aliyekata tamaa na maisha. kwani ukipata anayetamani maisha nawe umestaafu. utamtesa.Ningekushauri oa mtu wa umri wa miaka 50 na kuendelea.

    Nakutakia utafutaji mzuri.

    ReplyDelete
  29. Mwanaume hazeeki kihivyo!,,,kuwa na umri wa miaka 51 tu sio kigezo wapo mababu ambao bado wamo kama huyo wa miaka 78 hapo juu!

    ReplyDelete
  30. Hahaha Duh mababu wengine kauzu kweli,,, sasa huyo babu wa miaka 78 ukimkuta anakupigia mashine wewe mjukuu wake wa miaka 51 tu? Loh itabidi ucheke na umwache maana yeye ni kama mshikaji wako tu Msela mwenzio au sio?

    ReplyDelete
  31. Kaka yangu naomba nikupe tahadhari kumi (10, zisome kwa makini na ziprint, maana mimi kwa sasa nakaribia kutimiza miaka 40 nina ndoa ya na watoto wawili, pamoja na hayo nimewapitia waswahili wawili watatu na nimegundua haya yafuatayo:

    kama kuna mtu alikudanganya kwamba bongo utapata mwanamke wa kuoa inabidi umuulize mara mbili mbili, maana kama uliondoka hapa miaka ya tisini au elfu mbili mwanzoni, kwa sasa hali ya mabinti na kinamama wa hapa imebadilika sana, kitu wanachojali ni pesa zaidi kuliko mapenzi yenyewe, na hata kuliko ubinadamu, nafikiri wewe ni mtu mzima unaelewa athari za kuolewa na mtu asiyekuwa na upendo wa dhati.

    pili, wanawake wengi wa kibongo wana kiburi sana na hasa wakishaolewa, wanakuwa hawaaambiliki, anaweza kujibu lolote analoweza kuona linafaa kukuambia, watakuletea stress sana.

    tatu, uhuni umekithiri sana kiasi kwamba unaweza kukuta mtu ana ndoa lakini nje ana mabwana zaidi ya wanne nje ya ndoa.

    nne, ni kuongeza mzigo wa kimaisha maana usipokuwa mkali pesa ya wanawake wa kibongo haionekani nyumbani, wanachopenda kukukamua wewe pesa yako, yao kazi yake ni kuitumia kwenye vipodozi, nguo, kujenga kwao n.k., kuleta ndugu zao wakae kwako (japokuwa si kosa), nk.

    tano, kunyimwa tendo la ndoa, hasa mkishakaa pamoja, kwa visingizio vya 'kuchoka' na utashangaa mtu hafanyi kazi yoyote ndani anamwachia housegirl, yeye kazi yake ya zaidi ni kuangalia tv.

    sita,usahahu kuambiwa 'samahani' hata kama amekosea, au kuambiwa 'pole', labda kama utakuwa ni mtu wa kumpa zawadi saaaanaaa;

    saba, kikawaida mwanaume ndiye anyeoa kwa tamaduni zetu, si mwanamke!!. mwaaanamke anakufuata kwako, hivyo anapaswa kuwa mtii, huu si mfumo dume bali ni hali halisia, lakini utii na unyenyekevu kwa kinamama wa kibongo wakishaolewa unateremka hadi 0%, kama ipo.

    nane, ni uongo, wabongo wa kike wana matatizo mengi ya kudanganya, ni kama sehemu ya maisha yao, unaweza kuambiwa mtu kaenda kupima malaria kumbe anaenda gesti, au kukwambia yuko kariakoo kumbe kaelekea bagamoyo.

    tisa, call a spade spade; huku bwana wabongo wa kike wanapenda kulipiza kisasi, akisikia (si kuwa na uhakika) kuwa umefanya lolote mfano una nyumba ndogo ni lazima na yeye atafute ya kwake kimyakimya.

    Mwisho, ni onyo, wanawake wengi wa kibongo wanafikiri ulaya maisha ni muswano, unakula na kulalal tu, hawajui ugumu wa huko na wanafikiri kuja huko umeuchinja, kwa tangazo hili mtu anaweza kuwa ana ndoa na akakudanganya kuwa hana mtu na baadae ikakuingiza katika matatizo, unahitaji uwe makini sana.

    USHAURI:
    usitafute mwanamke kwenye blogu, utapata shida sana na utanikumbuka. Mwanamke mzuri ni yule unayejua historia yake mfano kama ni jirani yako au mmekua wote au mmesoma pamoja.

    DISCLAIMER: kuna waosha vinywa wataponda kuhusu niliyoyataja, simaanishi kuwa kinamama wa kibongo wote wako hivi, ila asilimia kama 80% wana tabia hizi, wachache sana wanaojua kuishi na mme. Naomba waliooa bongo msaidieni huyu bwana.

    kama ukipenda tunaweza kuwacliana kimazungumzo kama uko bongo mimi barua pepe yangu ni: katerero73@gmail.com

    ReplyDelete
  32. HALLO BRO SIKIA ! ACHANA NA MANENO YOTE HAPO. MIMI VILEVILE MSELA NIMEKUJA UK NINA MIAKA 30,BAADA YA KUZUNGUKA SANA MABEACH HUKO UGIRIKI ,SPAIN, ITALY MPAKA MAKARATASI KUWA NAYO YA UHAKIKA NI MIAKA 13ILIOFATIA. SASA UBEBAJI WA BOX MPAKA KUJIWEKA FIT. NI HII TU MIAKA 3 ILIOPITA, NINA 50 (UMRI) LEO BADO NINANGUVU NZURI TU KISEX KWANI NILIKUWA SIKUTULIA HIVYO NDIO MAANA NGUVU ZANGU BADO NI NZURI TU HAZINA WALAKINI. NIMEOA MWAKA JUZI NA TAYARI NINA MTOTO WA KIUME KUTOKA KWA MTANZANIA MWENZANGU AMBAYE UMRI WAKE NI MDOGO KWANGU, YEYE BADO ANA MIAKA 34 SASA. SEX LIFE YETU NI NZURI TU WALA HAINA VIKWEZO NAKWENDA GOLI MOJA MPAKA MBILI KARIBIA KILA SIKU WALA HALALAMIKI KUWA ANATAKA APIGWE 5 AU SITA KWA SIKU KWANZA HUKU ULAYA HAKUNA MUDA HUO. SEX NI UTULIVU TU WA AKILI.

    LAKINI NENDA KACHUMBIE KIKAWAIDA KINYUME CHA KUTANGAZA MITANDIONI, JAPOKUWA NDIO DUNIA NIAKWENDA HIVYO.

    JITAHIDI KUFUATIA UTAMADUNI WETU ITAKUWA NI RAHISI ZAIDI KWAKO KINYUME CHA KUTAFUTA MTANDAONI.OLE WAKO USIJE OA MBONGO WA HAPA UK, WOTE HAKUNA PENZI ZAIDI YA KUKUFANYA WEWE BUZI TENA LA KIZAMANI KAMA UNAVYOJUA WOTE NI WATAFUTAJI KAMA SISI NA SIWAKWELI!


    ENDELEA USIKATE TAMAA

    MDAU UK

    ReplyDelete
  33. Mdau, mwenye kutafuta wakuoa. Soma maoni yote lakini kikubwa kulikovyote ni kuwa Mke mwema anatoa mungu. Muombe sana mola wako akupe mke mwema na pia busara ya kumtafuta na kumtambua mke mwema ni yuko.

    ReplyDelete
  34. we mtoa mada unenifurahisha kwenye hizo ishu za "value" za tesco!!

    ReplyDelete
  35. Naomba niulize kwanini kaka yetu anatafuta mdada mwenye kujifikiria kuwa na low sex drive .?Ina maana NA yeye huyu kaka yuko hivyo hivyo kwa hiyo wataendana? Mimi sioni cha a Ajabu kutafuta mwenza mtandaoni kwa sababu ni kitu cha kawaida ulaya kutokana Na ukosefu WA muda kukutana NA watu kwenye starehe au mikusanyiko nk. Inabidi a toe. Aelekezo zaidi je ni mtaliki, ana watoto? Wangapi? Anakaa nao? Anajali huyo mdada akiwa NA watoto? Ana elimu kiasi gani? Wapo akina Dada waliotulia uk wife material lakini wanahitaji more info. Hawa ni watu waliosoma NA kazi nzuri tu

    ReplyDelete
  36. Mzee kijana hivi Huko Uk hakuna dini?mbona uamzi wa kumtafuta mchumba makanisani au miskitini mbona do kitedo cha busala,nakama kweli uwa unaenda kuswali.Kuliko kutumia (Globu ya jamii) Ni Mimi G.G.U S A

    ReplyDelete
  37. Ndugu zangu akina dada nimewasikiliza sasa naona niwashauri kidogo, huyu bwana mimi simfahamu lakini mimi nasema hivi huyu ni mwooaji siyo utani ni kweli yaweza kuwa amewahi kuoa akaacha lakini kusema ati anakasoro siyo kweli, na pia niwaambie dada zangu miaka ni namba tu utashangaa siku unamwona utadhani unaonana na kijana wa miaka 35, wanaume hatuzeeki sawasawa na miaka yetu, tofauti na ninnyi wenzetu na kwahiyo mke au dada anayefaa kuwa na huyu bwana naamini hata akiwa na miaka 30 si mbaya mtamechi tu,halafu pia napenda kuwaonya kwamba,kuwa kwake UK kisiwe kivutio bali yeye mwenyewe ndo kiwe kivutio kwa maneno mengine ni kwamba ni vizuri kama mkionana naye na muone kama anamvuto yaani wazungu wanasema kama chemistry ipo yaani kama unasisimuka kimapendi naye na siyo vinginevyo, sawa jamani, nadhini mumenielewa.
    Asante mimi naitwa Lucian komba, mshauri mzuri wa mapenzi hasa ya kuoana.

    ReplyDelete
  38. KAZI IPO, MAJIBU HAYA TUTAFIKA

    ReplyDelete
  39. Mdau KATERERO e-mail:katerero73@gmail.com ambaye ni Anonymous Tue Dec 27, 04:00:00 PM 2011 na mwenzie Mdau wa UK Anymous Tue 05:33:00 PM 2011

    MAELEKEZO AU MAONI YENU YATAMSAIDIA SANA NDUGU YETU MTAFUTA MKE WA KUOA!

    Mdau wa Dar Es Salaam.

    ReplyDelete
  40. Msaidieni kupata mchumba.... waswahili mnamaneno sana

    ReplyDelete
  41. Anachotafuta chengine watu wamejigeuza Pilato na kuanza kumhukumu. Wabongo kwa ramli kazi kweli kweli

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...