Mheshimiwa,

Naomba msaada wa kibinadamu haraka iwezekanavyo kwa mtu yeyote anayezungumza lugha ya Kikerewe kwa ufasaha aliyeko nchini Uingereza. 

Tafadhali kama unamjua rafiki au ndugu au wewe mwenyewe unaishi Uingereza na unakiongea Kikerewe vizuri basi wasiliana na ndugu Eli kupitia email: 

etambala@yahoo.co.uk au simu 07950413788 (kwa walioko Uingereza tu) kwa maelezo zaidi.
Asante sana kwa msaada wako.
Eli

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Mkalimani wa mambo ya kujilipua aka asylum, kila la kheri kaka.

    ReplyDelete
  2. jamani ukerewe kule salama?tupeana basi habari kama kunavurugu ya aina yoyote kwa wale ambao tupo london tuwahi nyumba kubwa kujilipua.

    ReplyDelete
  3. Sijamuelewa, kwani waingereza hicho kingereza ndio lugha yao au anataka mtu wa aina gani?

    ReplyDelete
  4. 1.kwanza kama unatatizo si uende ubalozi wa tanzania hapo london.
    2. ungekuwa vizuri uandike angalau tatizo lenyewe si kiundani, angalau kudokeza tu

    ReplyDelete
  5. SASA KAMA BWIKO NI GOGORO,UMEFUATA NINI NCHI ZA WATU HUKO?
    ANYWAY JUST A TIP,UKIFIKA MSALANI MEN NI UPANDE WA WANAUME,NA WOMEN NI KWA WANAWAKE,WASIJE WAKAKUFUNGULIA KESI YA KUBAKA.

    ReplyDelete
  6. Sina hakika na hilo la kujilipua lakini kama ni kweli ipo haja ya watanzania kuasha mawazo finyu ya aina hii. Miaka michache iliyopita nilisikia jamaa moja tuliosoma nao O' level na akapata one ya point 8, 1994 na kupata one ya point 4 kama sikosei A level na kusoma kompyuta Sayansi na kufaulu huko Asia Ulaya na baada ya kumaliza na kufaulu akajilipua UK kama msomali. Nilisikitishwa kwa mtu mwenye uwezo kama huu bado umebaki kuwa na wa darasani lakini akili si yake! Hakuwa huru kiakili tena nasikia alisoma tena degree hiyohiyo ya kwanza Uingereza! HUU NI UPUUZI NA ULIMBUKENI WA HOVYO.

    ReplyDelete
  7. Mbona kaeleweka vizuri. Hawezi kuanika hapa kila kitu. Wewe kama wakijua kikerewe, ametoa njia za mawasiliano. Wasiliana naye, utajua anachotaka. Ebooo!

    ReplyDelete
  8. Wasiliana na wana CCM UK watakupa njia sahihi bila longo longo wako karibu miji yote ya UK. wana huduma hata kama unataka contacts za kibiashara, utalii, michezo, elimu na kisheria tena bureeeeeeeee

    Kimamba

    ReplyDelete
  9. Wewe Upo ukwerewe = UK unatafuta mtu anayejua kikerewe =English?? hujasomeka vizuri.

    ReplyDelete
  10. huyu anatafuta mtu anaeongea kikerewe cha ukerewe tanzania na si anaeongea kiingereza!!

    ReplyDelete
  11. Huko UK watu wanafanya kazi nyingi miongozi mwake ni ubebaji wa maboksi madukani!.

    Mtu akiwa anafanya kazi ya Ukuli yani ubebaji Maboski anakuwa akili zake sio timamu!

    Sasa hebu angalieni tangazo hilo la mzungumzaji kikerewe na mazingira yenyewe si ndio walewale?

    Hebu angalia wazee wetu hapa Bandarini Dar Es Salaam Tanzania, unakuta mtu mzee alikini matusi na mambo ya ovyo ovyo kwenda mbele!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...