Tukiwa tunakaribia kumaliza mwaka, Mbunifu wa kiafrika kutoka Tanzania, Mustafa Hassanali atasheherekea msimu huu kwa kufanya mauzo ya ubunifu wake kuanzia tarehe 20th-22nd Desemba 2011.
Kwa mara ya kwanza kabisa tangu alipoanza kazi yake ya ubunifu ,Mustafa Hassanali atafanya pungozo kubwa la nguo zake za kutokea usiku kwa asilimia70. Dhumuni la mauzo haya makubwa ni kufanya watanzania walio wengi kupata Sanaa ya Mustafa kwa bei ya unafuu.
“Kukuza Dhana ya vitengenezavyo Tanzania, Tunaelewa umuhimu wa uzalendo, na wakati wa msimu huu wa skuku, hakuna kililcho bora kama bora kuvaa vazi la Mustafa Hassanali . Ili kuweza kuongeza motisha, Tutatoa marekebisho ya kila nguo itakayonunuliwa” alisema meneja masoko Hamis K Omary.
Mauzo hayo Makubwa ya Mustafa Hassanali yatafanyika, Kilimani Road mkabala Patricia Mezger clinic kuanzia saa 4 asubuhi hadi 12:00 jioni!
“Hii ni nafasi ya mara moja katika maisha ya kujipatia ubunifu wa Mustafa Hassanali kama zawadi kwa hii sikuku ya Krismasi kwa wapendwa wako alihitimisha msemaji wa Kampuni ya Amisa Juma.
KUHUSU MUSTAFA HASSANALI
Mustafa Hassanali ni mbunifu mjasiriamali anaeamini katika ‘daima sitashindwa’ huku akitumia kipaji chake na ubunifu wake wa mavazi katika kuleta maisha bora ya sasa na ya baadae.
Mustafa Hassanali hivi karibuni alibainishwa kuwa kama mmoja wa wabunifu wa mitindo kumi wa kiafrika Mwanaume katika Magazini ya New African Woman inayochapichwa nchini Uingereza
Kazi za mbunifu Mustafa zimekuwa zikithaminika na kuonyeshwa kimataifa, ambapo Mustafa alifanikiwa kuonyesha ubunifu wake katika nchi kama Angola ‘Angola Fashion Business’, FAFA (Festival of African Fashion and Arts in Kenya), Kameruni, Wiki ya Mitindo India 2009, Naomi Campbell’s fashion for relief 2009, Arise Africa Fashion Week 2009, Wiki ya mavazi Durban & Cape town, Vukani Fashion Awards Pretoria, Miss Ethiopia Beauty Pageant, Mediterranean Fashion Festival, Sicily, Italia, M’net Face of Africa, Msumbiji, Uganda, na Wiki ya Mitindo Kenya, ambayo kwa pamoja yamemletea heshima kubwa, ndani na nje ya nchi.
Ukikutana na Mustafa Hassanali ndipo utajua uwezo wake utokanao na kazi zake,yeye kama yeye anajiamini katika kila anachokitengeneza na anatumia karama na ubunifu wake kutengeneza kilicho bora leo na hata kesho,hasa katika swala zima la mavazi, kwasababu kila akifanyacho hutoka moyoni. Mustafa ni Fashionista wa kweli ndani na nnje
Kwa habari zaidi tembelea tovuti www.mustafahassanali.net
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...