Uncle Michuzi,
Pole saana na kazi ya kila siku katika kulihabarisha hili taifa. Uncle Michuzi niwie radhi japo upo busy saaana na habari za mafuriko ili kuokoa maisha ya watu lakini nami mpwao nina tatizo naomba uliweke kwenye globu ya jamii. Nauza camera yangu ili niweze japo kujikimu na hii hasara ya mafuriko iliyo ikumba familia yangu.
Tafadhari niwekee tangazo langu Uncle. Uncle ila naomba email yangu usiiweke simu niliyo wawekea inatosha. Tafadhari Uncle niwekee tangazo langu wajukuu zako wamenichachamalia saana baaba yao, Nina uhakika Camera ikiuzwa watatulia.
Ni camera aina ya SONY ina mda wa miezi sita tu tangu inunuliwe dukani, Bei ni maelewano. Iko kwenye hali nzuri na ubora wake juu ya utoaji picha zenye kiwango cha hali ya juu kama SONY ilivyo. Ina vifaa vyake vyoote pia vikiwa baado vipya.
Zifuatazo ni taarifa zaidi na picha za hii camera:
Aina: SONY (DIGITAL CAMERA)
Mega pixels: 8.1
Optical Zoom: 4X
Model: DC - W130 SONY SUPER STEADY SHOT.
Serial No. : 7634033.
Colour: SILVER.
Kwa yeyote mwenye kuhitaji wasiliana nami kupitia 0757 885 079.
Camera ipo hapa hapa Dar Es Salaam.
Asante.
Mdau wa Bonde la Msimbazi



Mdau wa Bonde la Msimbazi pole sana na maafa,
ReplyDeleteTaarifa tumeipata na tunaifanyia kazi ili tukuwezeshe na wewe ndugu yetu ktk kipindi hiki cha majonzi kwetu!
Isipokuwa huku tukisubiri mnunuzi wa kifaa chetu, hao Wajukuu tafadhali wapeleke kwanza Shule ya Msingi Mchikichini kama hawapo huko kwa vile jamii tumeelekeza nguvu zetu huko pamoja kwa ajili yenu, ili angalau wapate msaada wa dharura!
bei?
ReplyDeleteJamaa anatuyeyusha. Hawa ndio wanataka kutumia haya mafuriko kujinufaisha.
ReplyDeleteWe anony wa Sat Dec 24 08:35:00....hivi una akili kweli? Sasa huyo jamaa anajinufaisha vipi? Yeye ni muuzaji hakuomba pesa hapa!
ReplyDeleteduh nilikuwa natafuta camera,sasa nimeipata, mkubwa please niandikie chapu chapu email yangu ni jacobmayillah@hotmail.ca, niko kidogo mbali siwezi kupiga simu,ila njolo njolo zako zipo tayari
ReplyDeleteCamera ni mpya , naiuza shilling laki mbili kamili, maelewano yapo.
ReplyDeleteAsante.ca