Najitokeza kwa mara ya Kwanza katika GLOB YETU YA JAMII,ili nitoe angalau pongezi kwa chombo chatu cha SUMATRA,kwa kazi nzuri waliyofanya hususani katika kipindi hiki cha Sikukuu za Krismass na Mwaka Mpya.

Nathubutu kusema SUMATRA,ni Idara pekee hapa nchini yenye mafanikio makubwa katika shughuli zake,ikiwa ni pamoja na usimamizi wa Usafirishaji Abiria kwa vyombo vya MOTO.

Nilikuwa hapo Dar,tarehe 22.12.11,nilishuhudia Vijana wa Kazi toka SUMATRA wakiwajibika ipasavyo hapo UBUNGO Terminal,nilipanda Basi mojawapo la kutoka hapo Dar kuelekea Arusha,ambapo basi hilo lilitakiwa kutoza Nauli ya Shs 20,000/=wao walitoza kuanzia shs 25,000/=hadi 30,000/=,lakini Vijana wa kazi yaani SUMATRA,Waliingia katika basi hilo,na kuuliza,JE KUNA ALIYELIPA ZAIDI YA SHS 20,000/=?Mimi nilikuwa wa kwanza,NDIYO,NIMELIPA 25,000/=Mara moja AMRI ilitolewa,na nikarudishiwa 5,000/=na wengine waliolipa zaidi walirejeshewa.

Kwa hilo nawapa pongezi SUMATRA,Na nawaomba wafanye hivyo katika maeneo mengi ya Nchi,wanakopenda kufanya ulanguzi wa NAULI,kama wafanyavyo kanda ya Kaskazini,pia waangalie sasa nauli za kutoka Arusha/Dar,ambako sasa Wengi wameanza kurejea DAR.

Kaka Michuzi,haya ndiyo machache nilikusanya toka Kanda ya Kaskazini,naitakia maisha marefu GLOBU YETU YA JAMII,Kwani inatuelimisha,inatujuza mambo mbalimbali ya muda huo huo,kwa kweli hii ni GLOBU YETU.

AHSANTE SANA
ZABRON LUKELO MLIMBILA-MOSHI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. SUMATRA HAKUNA KITU MZEEE KWANZA NI ILE TU BAS LAKINI KAMA ARUSHA KILA IFIKAPO SAA KUMI NA MOJA JIONI ARUSHA NAULI INAPANDA KWAHIYO YANI ME SIONI KAMA SUMATRA WAPO ARUSHA NA KAMA WAPO BASI NI HEWA YANI POTEZA MUDA TU ULIZA WATU WATU WANOKAA TENGERU,USA RIVER AFU MICHUZI HABARI ZA KIAINA KAMA HIZO SOMETIME USIZIPOST AMANI SANA PAMOJA MDAU KUTOKA ARUSHA

    ReplyDelete
  2. Hongera SUMATRA muendelee hivyo hivyo bado EWURA nao wajipange upya

    ReplyDelete
  3. Ni muhimu kuanzisha sheria ya uwekaji nauli halali kwa kuzibandika vituo vya kuuuzia tiket na katika mabasi husika ili abira angalau awe na taarifa halali ya nauli na pia itasaidia utendaji mzuri kwa SUMATRA.

    ReplyDelete
  4. Sumatra ilikwisha tangaza nauli halali kwa kufuatia kiwango cha ubora wa basi na gharama za uendeshaji, hivyo kazi yao ilikwisha. Hiyo wanayofanya ni kazi ya ziada, ambayo inapaswa kufanywa na raia wenyewe wakisaidiana na polisi. Tukiendelea kuwa tegemezi eti serikali au taasisi zitufanyie kila kitu, hatutafika!

    ReplyDelete
  5. Je hatua gani zilichukuliwa kwa vyombo hivyo kupandisha nauli? au tutaendelea kurudishiwa walicho ongeza tuuuuu!!!!!!!!! kama kuku na mahindi.

    ReplyDelete
  6. Lt.Mayagila AntonyDecember 30, 2011

    Binafsi nilisafiri tarehe 24.11.2011 cha ajabu kuna makarani walikuwa wanatuuzia tiketi kwa shilingi 30,000/= kisha waanatumbia eti Sumatra wakija tuseme ni shs 20,000/= na gafla alitokea jamaa mmoja mrefu wa sumatra na kuuliza kama abiria tumelipa shs 20,000 ikabidi mie na abiria wachache tuseme ukweli na tukarudishiwa kisha nakaona wnaitwa chini wakaandikiwa faini.

    Cha ajabu baadae walitaka kuturudishia nauli zetu tushuke ikabidi nishuke nikawafuata maafisa wa sumatra, ile kufika tu waling'oa leseni yao na kuandika nafikiri faini ingine.waliomba sana msamaha nasi tukaenda kuwaomba maafisa wale wawasamehe ili tuondke na kweli walirudisha ile leseni tukaondoka.

    Nilichokiona pale ubungo wale maafisa ni wachache sana lakini wanafanya kazi kubwa sana sana na sio ya kubez.

    Kingine kwa mujibu wa makarani wale ni kuwa hawa jamaa wa sumatra neno rushwa hawataki kulisikia na ndio maana niliwaona ni majasiri hata kwa wamiliki wa mabasi.

    Kama taasisi zote za serikali zingekuwa kama hawa jamaa wa sumatra nchi ingekwenda mbele kwa kasi

    Mungu ibariki tz na sumatra msirudi nyuma dawa zaidi ni kuongeza maafisa wenu waadifu kila mahala mtaweza sekta ya barabara


    Luteni mstaafu

    ReplyDelete
  7. safi sana Sumatra, moyo huu na uendelezwe...Tz tunaweza tukiamua. Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tz.

    ReplyDelete
  8. TATIZO LA RUSHWA TANZANIA NA NCHI ZA KIAFRICA NI KUWEKEZA KWENYE TECHNOLOGY TUU...MAMBO HAYO YA KUPIGIZANA MAKELELE NA MAKARANI SIJUI WAKATISHA TICKET YANGEKWISHA..WAWAWEKEE WATU TECHNOLOGIA KAMA ONLINE TICKETING AU SELF SERVICE-KIOSKS HAKUNA KUONGEA NA MTU UNAKATA TICKET YA BUS UNALOPENDA UNAINGIA ZAKO KWENYE BUS...ULINZI UWEPO TU KWENYE HIVYO VIOSKS.....TATIZO LA TANZANIA WAKUU WETU HAWAPENDI TECHNOLOGY KWA SABABU WANAENDEKEZA RUSHWA....RUSHWA INAKOMESHWA NA TECHNOLOGY TU...SIO KWAMBA WAZUNGU HAWANA RUSHWA AU HAWAPENDI RUSHWA,RUSHWA WANAYO SANA ILA WAMEJUA JINSI YA KUIDHIBITI

    ReplyDelete
  9. Kama walikwisha tangaza bei ya nauli, mbona kutoka Arusha mjini hadi tengeru elf 2? Ni kweli Arusha hawapo hawa jamaa labda viini macho

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...