Mama Mzazi wa mtoto  Jifti Bi. Adela Kakopayani akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili kutokea Shinyanga ambapo mtoto wake atapatiwa matibabu katika hospitali ya Muhimbili kwa hisani ya Precision Air. Kushoto ni Meneja Mauzo Taifa wa Precision Air Bw. Tuntufye Mwambusi na Bw. Benson Chuwa Afisa Huduma wa Precision Air uwanjani Julius Nyerere.

Shirika la ndege la Precision Air leo imejitokeza kumsaidia mtoto Jifti Shomari (2) kutokea Shinyanga anayekabiliwa na ugonjwa wa kuvimba kwa tumbo kutokana na matatizo ya ini.

Akizungumza katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Meneja Mauzo Taifa wa Precision Air Bw. Tuntufye Mwambusi alisema kwamba shirika hilo liliguswa sana na hadithi ya mtoto huyo aliyeelezea mama yake walipoonekana kwa mara ya kwanza katika vyombo vya habari kama wiki mbili zilizopita.

“Kama shirika la ndege la kibiashara tunatambua kwamba tuna wajibu pia kwa jamii na ndo maana katika moja ya shughuli zetu tumeamua kumsaidia mtoto Jifti kupatiwa matibabu ili naye siku moja aweze kuwa na faraja ya kuishi na kucheza kama watoto wengine,” alisema Mwambusi.

“Tunaamini kwamba usafiri wa ndege wa kwenda na kurudi tuliyoutoa kwa yeye na mama yake mzazi kutokea Shinyanga kuja Dar imewarahisishia sana kazi kutokana na ukweli wa hali ya uvimbe wa tumbo lake. Pamoja na hayo, tunaazimia kwamba zawadi ya fedha taslimu tuliyotoa itasaidia pia katika matibabu yake hospitalini Muhimbili,” aliongeza Mwambusi alipokuwa uwanjani hapo kumpokea mtoto Jifti na mama yake.

Naye mama yake mzazi Jifti Bi. Adela Kakopayani alitoa shukurani zake za dhati kwa shirika la ndege la Precision Air.

“Napenda kusema ahsante sana kwa shirika hili la ndege la Precision Air kwa kuweza kunifikiria mimi na mwanangu Jifti. Mungu awabariki na awazidishie kwa moyo huu mzuri wa kujitolea,” alisema Bi. Kakopoyani.

Wakati huo huo Meneja Mauzo Taifa wa Precision Air pia alitoa rai kwa makampuni mengine na watu binafsi kujitokeza pia kumsaidia mtoto huyo.

Mtoto Jifti anatatizo ya ini inayemsababishia hali ya kuvimba katika tumbo lake. Baada ya kusumbuliwa na matatizo hayo kwa muda wa mwaka mmoja sasa mama Jifti alishauriwa na hospitali ya halmshauri na mkoa wa Shinyanga kuja kupatiwa matatibabu hospitalini Muhimbili ambapo tatizo hilo linaweza tibika.

Mama Jifti anapatikana kwa nambari ya simu 0786 228 284 kwa wasamaria wema wowote wengine watakayeguswa kumsaidia mtoto huyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...